Virusi vya Corona: Ukimya ulivyotanda kumbukumbu ya mauaji ya kimbari Rwanda

Kwibuka

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Kumbukumbu ya 26 ya mauaji ya kimbari zinafanyika watu wakiwa makwao

Tangu mwaka 1994 shughuli za kumbukumbu za mauaji ya kimbari zimekua zikihudhuriwa na umma wa Wanyarwanda, huku baadhi wakifanya matembezi ya kuwakumbuka watu zaidi wa 800,000 waliouawa wakati huo lakini mwaka huu shughuli hizo zimefanyika nyumbani.

Maadhimisho haya ya 26 yanafanyika huku Rwanda ikiwa imetangaza sheria ya kutotoka nyumbani inayowazuwia watu kukaa nyumbani ili kuzuwi maambukizi ya virusi vya corona. Jumla ya watu 105 walithibitishwa kupata maambukizi ya virusi hivyo huku wanne wakiripotiwa kupona.

Viongozi wachache wakiongozwea na rais Pual Kagame pamoja na mkewe wamefika katika eneo la kumbukumbu ya mauaji ya kimbari mjini Kigali kutoa heshima kwa wahanga wa mauji hayo.

Bwana Kagame amewashukuru Wanyarwanda kwa kuheshimu armi ya kukaa nyumbani ili kuzuwia kusambaa kwa virusi vya corona.

Chanzo cha picha, Village Urugwiro/Twitter

Maelezo ya picha, Bwana Kagame amewashukuru Wanyarwanda kwa kuheshimu armi ya kukaa nyumbani ili kuzuwia kusambaa kwa virusi vya corona.

Akihutubia umma wa Wanyarwanda kwa njia ya Televisheni, redio na mitandao ya kijamii Bwana Kagame amewashukuru Wanyarwanda kwa kuheshimu armi ya kukaa nyumbani ili kuzuwia kusambaa kwa virusi vya corona.

Kwa kwaida Kumbukumbu za mauaji ya kimbari nchini Rwanda huendelea kwa muda wa wiki nzima kuanzia tarehe 07 Aprili huku shughuli za mazishi ya masalia ya miili ya watu waliouawa wakati wa mauaji hayo zikifanyika .

Tume ya kupambana na mauaji ya kimbari nchini humo ,CNLG, ilitangaza hivi karibuni kuwa kumbukumbu ya mwaka huu itakua tofauti na miaka iliyopita, kwani watu watawakumbuka wapendwa wao na wanyarwanda wegine waliouliwa 1994 wakiwa majumbani mwao.

Miaka yote kumbukumbu za mauaji ya kimbari zimekua zikiandaliwa na kuhudhudhuriwa na watu wengi huku zikiandaliwa na utawala kuanzia ule wa ngazi za mwanzo (nyumba kumi ) hadi ngazi ya kitaifa.

Wahanga wa mauaji ya kimbari wamekua wakiendeleza shughuli za kufukua na kuzika miili ya wapendwa wao kwa heshima na kuandaa kumbukumbu hizo katika maeneo mbali mbali ya nchi kwa siku mia moja baada ya kumbukumbu rasmi za kitaifa, lakini shughuli hizo zinatazamiwa kusitishwa mwaka huu.

Kila mwaka inapofika siku kama ya leo tarehe 07 Aprili saa sita za mchana Wanyarwanda hukaa kimwa kwa muda wa dakika moja kama ishara ya kuwakumbuka wahanga wa mauaji ya kimbari ya mwaka 1994.

Josiane Uwanyirigira aliyenusurika mauaji hayo ameiambia BBC kuwa: "Sio jambo la kawaida. Sijawahi kushuhudia wakati wowote kumbukumbu za mauaji ya kimbari dhid ya watutsi zikivurugwa hivi''.

"Wakati wote tumekua tukihudhuria mihadhara matembezi ya kukumbuka 'walk to remember', ina hayo yamekua yakitusaidia kuwa pamoja na wenzetu , tunapata fursa ya kuongea juu ya majonzi kuhusu tunaowakumbuka, lakini kwa sasa kumbukumbu ya nyumbani sio rahisi kwasababu ni lazima tukae nyumbani ".

"Hivi virusi ni vikali, lakini hahitanizuwia kuwakumbuka watu wangu leo, nitawakumbuka nikiwa nyumbani ", amesema mauthiriwa mwigine wa mauaji ya kimbari ya Rwanda - Uwanyirigira.

Kwibuka Ntaryamira

Chanzo cha picha, Burundi Presidency

Maelezo ya picha, Nchini Burundi, jana tarehe 06/04 walimkumbuka rais Cyprien Ntaryamira aliyekufa pamoja na rais wa zamani wa Rwanda Juvenari Habyarimana katika ndege moja

Mauaji ya kimbari nchini Rwanda yalianza trehe 07/04/1994 yakadumu kwa muda wa siku 100 kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa ambao ulitenga ''siku ya kimataifa ya kumbukumbu ya mauaji ya kimbari ya Rwanda dhidi ya Watutsi''

Mauaji ya kimbari yalianza baad y kuanguka kwa ndege yatangiye nyuma y'ihanurwa ry'indege yarimo Perezida Juvénal Habyarimana wategekaga u Rwanda wari kumwe na Perezida Cyprien Ntaryamira w'u Burundi mu ijoro rya tariki 06/04/1994.

Balozi za Rwanda katika mataifa mbalimbali duniani pia hyandaa shughuli za kumbukumbu hizo tarehe kama hii

Hata hivyo shughuli hizo hazitagfanyika mwaka huu kwani nchi zote duniani zimetangaza tahadhari ya watu kutosogeleana kutokana na mlipuko wa virusi vya corona huku nyingine kama za Ulaya zikitangaza pia sheria ya kutotoka nyumbani (lockdown).

coronavirus

Taarifa zaidi kuhusu corona:

Hatua za kudhibiti maambukizi zimeimarishwa Rwanda

Mapema mwezi huu serikali ilirefusha muda wa sheria ya kukaa nyumbani kwa siku 21 zaidi baada ya muda wa awali kukamilia ili kuzuwia maambukizi ya virusi.

Serikali iliwasambaza askari kwa ajili ya kuhakikisha kuwa marufuku hiyo inatekelezwa ipasavyo.

Marufuku hiyo uliongezwa na baraza la Mawaziri baada ya idadi ya walioambukizwa kuongezeka kutoka 17 mpaka 82 kwa majuma mawili.

Wakati huu , mipaka itaendelea kufungwa na raia wa Rwanda pekee ndio watakaoruhusiwa kuingia nchini humo.

Mizigo itaendelea kuingizwa nchini Rwanda.

Maduka, shule, maeneo ya kufanya ibada yatafungwa na waajiriwa wataendelea kufanya kazi wakiwa nyumbani, pia vyuo na shule zimetakiwa kutumia teknolojia kuendelea kutoa maelekezo ya masomo.

''Shughuli za kilimo zitaendelea wakati huu wa maandalizi ya msimu wa kilimo huku wakulima wakiamriwa kufuata taratibu na maelekezo kutoka mamlaka za afya'', waraka wa baraza ulieleza.

Unaweza pia kutazama:

Maelezo ya video, Coronavirus: Utajuaje kuwa umeathirika na virusi?

Familia zilizoathirika

Familia zilizoathiriwa na sheria ya kukaa nyumbani , nchini Rwanda zilipokea msaada wa Chakula kutoka kwa serikali ya nchi hiyo.

Familia hizo ni zile zilizoathiriwa na agizo la kukaa nyumbani liliyowekwa nchini humo ili kukabiliana na maambukizi ya coronavirus.

Idadi ya watu walioambukizwa na coronavirus imefikia watu 75.