Coronavirus: Wanasiasa waliojitosa kupambana na corona kwa njia ya nyimbo

Katika wimbo wake Bwana Weah alishauri kwamba jambo kuu muhimu unaloweza kufanya kujilinda mwenyewe ni kunawa mikono

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Katika wimbo wake Bwana Weah alishauri kwamba jambo kuu muhimu unaloweza kufanya kujilinda mwenyewe ni kunawa mikono
Muda wa kusoma: Dakika 3

Tangu mlipuko wa coronavirus ulipoanza juhudi mbali mbali za kuzuwia kusambaa kwa virusi hivyo zimekua zikifanyika, lakini baadhi ya wanasiasa hawa wamejitosa kutumia usanii kuwaelemisha raia juu ya kuepuka virusi.

Rais wa Liberia na mchezaji kandanda maarufu wa zamani George Weah, tayari ametoa wimbo wake wake wa Corona aliourekodi katika studio yake mwenyewe binafsi iliyopo nyuma ya kanisa, katika mji mkuu Monrovia, kulingana na shirika la habari la Ufaransa RFI.

Alianza kuiandaa single yake ya coronavirus hata imewafiki imewafikia Waliberia, amenukuliwa msemaji wake Solo Kelgbeh akisema katika gazeti la the Guardian.

Kwa sasa kuna visa vitatu vilivyothibitishwa vya Covid-19 nchini humo.

Katika wimbo wake Bwana Weah anaongea zaidi kuliko kuimba, ambapo mistari ya maneno yake imejaa taarifa kamili za elimu kuhusu jinsi ya kudhibiti kusambaa kwa virusi vya corona na dalili zake.

Katika wimbo wake alishauri kwamba jambo kuu muhimu unaloweza kufanya kujilinda mwenyewe ni kunawa mikono.

Halafu anaimba nusu ya kibwagizo : "Covid-19 inaweza kusababisha matatizo makubwa ya mfumo wa kupumua."

Kibwagizo cha wimbo huo kinaimbwa na waimbaji wa nyimbo za dini wanaoimba: "Lazima tuamke, njooni tuamke pamoja tupambane na corona ."

Coronavirus

Taarifa zaidi kuhusu coronavirus:

Bobi Wine amejiunga na Weah kuhamasisha umma kuepuka maambukizi

Katika wimbo wake Sanitize mwanamuziki nyota wa muziki wa kufokafoka (pop) na Mbunge wa Uganda Bobi Wine pia ametoa wimbo akiwatahadharisha Waganda na Waafrika juu ya janga la Corona barani Afrika.

Ruka YouTube ujumbe
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa YouTube ujumbe

Wine, ambaye jina lake halisi ni Robert Kyagulanyi, ameshirikiana na msanii mwenzake Nubian Li kutoa wimbo huo Jumatano ulioimbwa kwa mtindo wa rhumba akielezea umuhimu wa usafi binafsi.

" Habari mbaya ni kwamba kila mmoja anaweza kuwa muathiriwa," Wine ameimba. "Lakini habari njema ni kwamba kila mtu anaweza kuwa suluhu."

Wawili hao wametumia wimbo wao kuwahamasisha watu kunawa mikono mara kwa mara, watu kuacha kukaribiana na kuchunguza dalili za virusi kama vile homa na kikohozi.

" Habari mbaya ni kwamba kila mmoja anaweza kuwa muathiriwa," amesema Bobi Wine katika wimbo wake kuhusu corona
Maelezo ya picha, " Habari mbaya ni kwamba kila mmoja anaweza kuwa muathiriwa," amesema Bobi Wine katika wimbo wake kuhusu corona

Mwanamuziki nyota wa muziki wa kufokafoka (pop) na Mbunge wa Uganda Bobi Wine pia ametoa wimbo akiwatahadharisha Waganda juu ya janga la Corona.

Katika wimbo wake mbunge huyo amewataka Waganda kufuata ushauri wa kudhibiti maambukizi huku akiwataka watumie vitakasa mikozo ( hand sanitizer) .

Hali ya Uganda kuhusu coronavirus kwa sasa.

Bobi waine ametoa wimbo wake huku Uganda ikiripoti visa vinne zaidi vya coronavirus, na hivyo kuifanya nchi hiyo kuwa na idadi ya watu 18 wenye visa vya coronavirus.

Maafisa wa usalama nchini Uganda wamelaumiwa kwa kutumia nguvu zaidi kutekeleza marufuku ya usafiri kwa kuwapiga raia kwenye mitaa ya mji wa Kampala

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Maafisa wa usalama nchini Uganda wamelaumiwa kwa kutumia nguvu zaidi kutekeleza marufuku ya usafiri kwa kuwapiga raia kwenye mitaa ya mji wa Kampala

Rais Yoweri Museveni amesema kuwa visa vipya vinakuja baada ya watu 197 wengi wao wakiwa ni wale waliotoka Dubai na Muungano wa kiarabu kupimwa Alhamisi.

Wengi wa watu hao ambao wana maambukizi nchini Uganda wana historia ya kusafiri Dubai na Milki za kiarabu.

Wakati huo huo biashara katika mji mkuu Kampala na vituo vya kote nchini umefutwa baada ya kuanzishwa kwa marufuku ya wiki mbili iliyoanzishwa Jumatano.

Kunahofu kuwa, kudolola kwa uchumi wakati huu kutaathiri pakubwa watu wenye pato la chini ambao bado hawajapata usaidizi wowote kutoka kwa serikali.

Pia kumekua na shutuma ya matumizi nguvu kupita kiasi ya polisi na wanajeshi ambao walionekana wakiwapiga watu kwenye mitaa.

Unaweza pia kutazama:

Maelezo ya video, Coronavirus: Je agizo la kuwa umbali wa mita moja litatekelezwaje katika mitaa ya mabanda