Thai Airways: Mama na watoto wake ni 'wanene sana' kukalia viti vya daraja la kwanza katika ndege

Wanawake watatu waambiwa kwamba ni wanene sana kukalia viti vya kifahari vya Business class

Chanzo cha picha, Supplied

Kukalia viti vya daraja la kwanza katika ndege ya safari iliochukua takriban saa 11 kurudi Aucland kulilenga kuwafurahisha Renell na Tere baada ya kufanyiwa upasuaji wa kupunguza uzani katika mji wa Bangkok.

Badala yake dada hao wawili pamoja na mama yao, Huhana waliwachwa na kiwewe na wafanyakazi wa kampuni ya ndege ya Thai ambao walikuja mbele yao na mkanda wa kipimo na kuwaambia kwamba ni wanene kupita kiasi kwa wao kuketi katika viti hivyo vya kifahari.

Lakini miezi sita baada ya waliopitia Huhana mwenye umri wa miaka 59 ana uchungu mwingi kuhusu kitendo hicho .

''Wafanyakazi walipiga kelele wakisema mara kwa mara wafanyakazi walikuwa wanapiga kelele na kusema tumenenepa sana. Watu walitutazama tukipimwa katika eneo la kuingia ndani ya uwanja wa ndege''.

''Ilikuwa aibu kubwa jinsi tulivyofanyiwa hatua ilionifanya kudondokwa na machozi'', alisema Huhana.

Tatizo la kutojua lugha waliokuwa wakitumia liliwafanya wasifahamu kila neno wallilo tamka lakini wafanyakazi walikataa kuwaruhusu kukalia viti hivyo na kuwalazimu kuketi katika viti vya kawaida.

Huhana anasema kwamba hatosafiri tena kwa ndege, hadi pale atakapopunguza uzani, ili kuzuia uchungu aliohisi yeye na watoto wake, aliongezea.

Kampuni nyingi za ndege huongeza urefu wa mikanda ya viti kwa abiria walio na uzani mkubwa.

Lakini kampuni ya ndege ya Thai ilisema kwamba mikanda katika viti vyake vya kifahari haiwezi kuongezwa urefu. Familia hiyo bado imeshangazwa na maelezo hayo.

Ndege ya kampuni ya Thai Airways

Chanzo cha picha, Getty Images

Tangu kisa hicho cha uchungu mwingi msimu wa joto uliopita , Huhana na wanawe wamekuwa wakijaribu kulipwa fedha zao kutoka kwa kampuni ya ndege ya Thai .

Lakini kampuni hiyo imesema kwamba itawalipa salio kati bei ya viti vya daraa la kwanza na vile vya daraja la pili.

Alimfuata ajenti walienunua tikitiki kwake , ijapokuwa familia hiyo ililazimika kusubiri kwa takriban miezi sita.

Walipowasiliana na BBC, msemaji wa kampuni ya ndege ya Thai alisema kwamba kwa sasa wana mifumo mizuri ya tahadhari zaidi hivyobasi maajenti huelezewa.

'Inahuzunisha'

Familia hiyo ilikuwa katika ziara ilioandaliwa na Destinationa beauty, ambayo husimamia kuwapeleka wateja Thailand ili kufanyiwa upasuaji wa kupunguza uzani.

Martin Olsen , afisa mkuu wa kampuni ya Destination Beauty , alisema kwamba alihuzunishwa sana jinsi kampuni hiyo ilivyolichukulia swala lote.

Pia alishangazwa na vitendo vya wafanyakazi wa Thai Airways , kwa kuwa watu wengi walionenepa kupitia kiasi hukalia viti vya daraja la kwanza badala ya viti vya kawaida.