Mpango wa amani wa Trump mashariki ya kati: Wapalestina wasema kuna 'njama'

Wapalestina wakiandamana katika mji wa Gaza. Picha ya Januari 29, 2020

Chanzo cha picha, AFP/Getty Images

Maelezo ya picha, Wapalestina wakiandamana katika mji wa Gaza

Wapalestina wamepuuzilia mbali mpango mpya wa Rais wa Marekani Donald Trump kuhusu amani ya mashariki ya kati wakitaja kuwa "njama".

Mpango huo unapuuza taifa la Palestina na kutambua mamlaka ya Israel kuhusu makaazi yake katika eneo la ukingo wa magaribi

Jerusalem itasalia kuwa mji mkuu wa Israel bila "pingamizi", lakini mji mkuu wa Palestina utajumuisha "maeneo ya Jerusalem mashariki".

Akijibu tangazo hilo la siku ya Jumamne, rais wa Palestina Mahmoud Abbas alisema: "Jerusalem haitauzwa".

"Haki zetu haziuzwi na wala sio ya kuamua itauzwa kwa fedha kiasi gani ," aliongeza.

Maelfu ya Wapalestina walifanya maandamano katika ukanda wa Gaza, huku majeshi ya Israel yakipelekwa kulinda maeneo yanayokaliwa na raia wake katika eneo la ukingo wa magharibi.

Wanawake wa Palestina wakiwa wamebeba vitambaa wakati vijana wakicheza nje ya kuta za mji wa zamani wa Yerusalemu

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Wanawake wa Palestina wakiwa wamebeba vitambaa wakati vijana wakicheza nje ya kuta za mji wa zamani wa Yerusalemu

Mapendekezo hayo ambayo, yanalenga kusuluhisha mzozo wa muda mrefu duniani, yalitayarishwa chini ya usimamizi mume wa binti ya Trump Jared Kushner.

Rripoti zinasema Bw. Netanyahu anapanga kushinikiza baraza la mawaziri kupiga kura ya kuidhinisha 30% ya makaazi yake katika eneo la ukingo wa Magharibi katika kikao kitakachofanyika siku ya Jumapili.

Israel Iliwapeleka karibu wayahudi 400,000 katika makaazi ya Wapalestina yaliopoukingo wa magharinbi huku wengine 200,000 wakiishi mashariki mwa mji wa Jerusalem.

Makaazi hayo yanachukuliwa kuwa kinyume cha sharia kwa mujibu wa sharia ya kimataifa, japoinapinga hili.

Bw. Abbas alisema nini?

Katia tamko lake la siku ya Jumanne, alisema haiwezekani hakuna Mpalestina, mwarabu,Muislamu au mtoto wa Kikristo atakayekubali " taifa la Palestina bila Jerusalem kuwa mji wake mkuu.

"Tunasema La, La ,La mara elfu moja," alisema. "Tumepinga mpango huu kuanzia mwanzo na msimamo wetu uko sawa."

Kundi la Hamas ambalo la wanamgambo wa kiislam wa Palestina, linalodhibiti ukanda wa Gaza, pia limepinga mpango huo likongeza kuwa ni njama ya "kusambaratisha miradi ya kitaifa ya Palestina".

Rais wa Marekani Donald Trump amewasilisha mpango kazi kuhusu Mataifa ya mashariki ya kati ambao ulikwa ukisubiriwa kwa muda mrefu, ukihaidi kuwa Jerusalem utabaki kuwa mji mkuu wa Israel.

"Tunasema La, La ,La mara elfu moja," alisema. "Tumepinga mpango huu kuanzia mwanzo na msimamo wetuuko sawa."

Waandamaji wa Palestina wakiwa wamekusanyika mjini Ramallah eneo la ukingo wa Magharibi

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Waandamaji wa Palestina wakiwa wamekusanyika mjini Ramallah eneo la ukingo wa Magharibi

Kundi la Hamas ambalo la wanamgambo wa kiislam wa Palestina, linaladhibiti ukanda wa Gaza, pia limepinga mpango huo likongeza kuwa ni njama ya "kusambaratisha miradi ya kitaifa ya Palestina".

Umoja wa Mataifa umeelezea kujitolea kwake kusuluhisha mzozo wa mpaka baina ya mataifa hayo mawili kabla ya mapigano ya mwaka 1967, wakati Israel iliponyakua eneo la wa magharibi na Gaza.

Netanyahu amesema nini?

Waziri mkuu wa Israel Benjamini Netanyahu alielezea mpango wa Bw. Trump kama'' Mpango wa karne.''

Israel "haitapoteza hii fursa ", Bw. Netanyahu alisema.

"Mpla atubariki sote kwa usalama,maisha marefu na amani!" aliongeza.

Jamii ya kimataifa imepokelea vipi pendekezo hilo?

Msemaji wa Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres ailitoa wito wa kufikiwa kwa mkataba wa Amani kwa kuzingatia azimio la Umoja wa mataifa, sharia ya kimataifa na makubaliano ya pande mbili.

Jumiya ya mataifa ya Uarabuni imeema itafanya kikao cha dharura sikuya Jumamosi kujaidili sssuala hilo.

Waziri wa mambo uyanje wa Uingereza Dominic Raab ametoa wito kwa Palestina kutathmini mpango huo "Bila kuegemea upande wowote kama hatua ya kwanza kuelekea mashauriano ya yatakayofikia suluhisho la kudumu."

white space

Mambo gani muhimu ambayo Trump amependekeza?

"Leo Israel inapiga hatua kubwa ya amani," bwanaTrump aliwaambia maofisa na waandishi wa habari katika ikulu ya Marekani.

"Dira yangu ni kuwasilisha fursa ya ushindi katika pande zote mbili, ili kutatua mgogoro huu unaouweka Palestine katika hatari ya kutokuwa taifa huru dhidi ya vikosi vya usalama vya Israel."

Mapendekezo yake ni :

  • Marekani itatambua mamlaka ya Israel katika himaya ambayo iko kwenye mpango wa Trump kuwa ni sehemu ya Israel.
  • Ramani iliyoandaliwa na Trump imeongeza himaya ya Palestina kuwa mara mbili na mji mkuu wa Palestina kuwa mashariki ya Jerusalem, bwana Trump alisema kuwa ubalozi wa Marekani utakuwa wa wazi.
  • Taasisi ya Palestina inayofahamika kama' Palestine Liberation Organisation (PLO)' ilisema kuwa mpango wa Trump ulipaswa kuipa Plaestina zaidi ya asilimia 15 ya sehemu ya kihistoria ya Palestina.
  • Jerusalem "utabaki kuwa mji mkuu ambao haugawanyiki". Israel na Wapalestina wanapaswa kutoa madai yao juu ya kumiliki mji huo mtakatifu. Palestina wamesisitiza kuwa mashariki ya Jerusalem, ilichukuliwa na Israel mwaka 1967 katika vita ya mashariki ya kati hivyo mji huo mkuu unapaswa kuwa wao.
  • Hii ni fursa kwa Wapalestina kuwa taifa huru ingawa alitoa taarifa kidogo juu ya mpango huo.
  • "Si mpalestina wala muisraeli ataondolewa katika makazi anayoishi kwa sasa" - mpango huo umependekeza kuwa himaya ya wayahudi wa Israel itaendelea kubaki eneo la ukingo wa magharibi.
  • Israel watafanya kazi na mfalme wa Jordan kuhakikisha kuwa eneo la takatifu la Jerusalem linalojulikana kama makazi ya wayahudi na kunatunzwa na waislamu pia.
  • Himaya iliyoelezwa na Trump kuwa ya wapalestina katika ramani, inaonyesha kuwa eneo hilo litabaki kuwa wazi na kutoendelezwa kwa chochote kwa muda wa miaka minne.

"Wapalestina wanaishi katika umaskini na ghasia, wanakabiliwa na ugaidi na hawana maisha bora .Wanapaswa kuwa na maisha bora sasa", alisema bwana Trump.

white space

Vilevile alibainisha kuwa ukingo wa magharibi hautagawanywa nusu kwa nusu katika mpango huo.

"Tutatengeza mipaka ya himaya hiyo katika siku za baadae katika taifa la wapalestina, wakati ambao taifa limefikia makubaliano na kujiondoa katika ugaidi", alisema.

Maofisa wa Israel wanasema kuwa bwana Netanyahu ataenda Moscow siku ya jumatano kujadili mapendekezo hayo na rais wa Urusi, Vladimir Putin.

Amependekeza kuwa taifa huru la Palestina na mamlaka ya Israel inapaswa kulitambua taifa hilo kuwa liko katika makazi ya ukingo wa magharibi.

Akiwa amesimama pamoja na waziri mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu katika Ikulu ya Marekani, bwana Trump alisema kuwa hii ni fursa ya mwisho kwa Wapalestina.

Rais wa Palestina, Mahmoud Abbas amehairisha mipango hiyo na kusema kuwa iko kinyume na sheria."

"Nimemwambia Trump na Netanyahu: Jerusalem haiuzwi wala haina mjadala wa kibishara.

Mkataba wao hautapitishwa kwa sababu haukidhi taratibu za kisheria," alitoa tamko hilo katika televisheni ya Ramallah iliyoko katika Makazi ya ukingo wa magharibi.

Palestinian protesters wave the national flag and a portrait of president Mahmud Abbas during a demonstration in the West Bank city of Ramallah on January 28, 2020

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Wapalestina waandamana kupinga mpango huo

Mpango huo unaofahamika kama 'The blueprint' umelenga kutatua tatizo moja duniani ambalo limekuepo kwa muda mrefu, ni mgogoro wa muda mrefu.Mpango huo uliandikwa na mkwe wa rais Trump bwana -law Jared Kushner.

Maelfu ya wapalestina waliandamana katika mji wa Gaza mapema Jumanne, wakati jeshi la Israel lilipovamia eneo la ukingo wa magharibi.

Tamko hilo la pamoja kutoka kwa bwana Trump na bwana Netanyahu limepata changamoto za kisiasa katika mataifa yao.

Trump akiwa bado na mashtaka dhidi ya matumizi mabaya ya madaraka, na huku waziri mkuu wa Israel akikabiliwa na madai ya rushwa.

Viongozi wote wawili wakanusha madai dhidi yao.

Presentational grey line

Balozi wa Marekani nchini Israel bwana David Friedman, alisema kuwa muda ambao wametangaza mabadiliko hayo hawakuhusisha maendeleo yeyote ya kisiasa na kuongeza kuwa mpango huo ulikuwa umekamilika muda kidogo.

Ripoti zinasema kuwa bwana Netanyahu alikuwa amepanga kuendelea kuchukua asilimia 30 ya eneo la ukingo wa magharibi, ukisubiri kura ya wabunge siku ya jumapili.

Zaidi ya Waisraeli 400,000 ambao wanaishi eneo la ukingo wa magharibi , makazi hayo yanadaiwa kuwa kinyume na sheria kwa mujibu wa sheria za kimataifa, ingawa Israel wanapuuzia jambo hilo.

Bwana Friedman alisema kuwa Israel haipaswi kusubiri bali wanapaswa kuondoka katika himaya hiyo.