Mapigano ya Libya: Tulifikaje hapo?

Wanajeshi wakiwa kwenye kifaru

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Libya imekumbwa na mapigano tangu kuanguka kwa utawala wa Muammar Gaddafi

Kwa mara nyengine tena, Libya imetumbukia kwenye mapigano huku juhudi za kimataifa za kupatikana kwa amani zikiendelea kati ya makundi hasimu.

Kuna wapinzani wawili nchini Libya kwa sasa: Umoja wa Mataifa ilitambua serikali inayoongozwa na Waziri Mkuu Fayez al-Serraj, na kuna utawala uliongozwa na vikosi vya waasi chini ya Jenerali Khalifa Haftar.

Wiki hili pekee, pande mbili zilikuwa zimekubaliana kusitisha mapigano baada ya shinikizo kutoka kwa Urusi na Uturuki.

Lakini wengi walitarajia kwamba, hilo lingemalizika baada ya siku chache tu, hasa baada ya Jenerali Haftar alipokataa kuweka rasmi makubaliano ya kusitisha vita, na kurejesha nchi hiyo katika enzi za wasiwasi wa kutokea kwa machafuko.

Lakini ilikuwaje hadi Libya ikafikia hapo ?

Ahadi za haraka

Urusi na Uturuki zinatakuwa kuwa na ushawishi nchini Libya katika siku za baadaye

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Urusi na Uturuki zinatakuwa kuwa na ushawishi nchini Libya katika siku za baadaye

Makubaliano hayo yanalenga kusitisha vita vilivyodumu kwa miezi tisa ambavyo vilianza wakati vikosi vya Jenerali Haftar vilipoanza kufanya mashambuli mapya.

Zaidi ya mizi 6 iliyopita peke yake, karibia watu 2,000 wameuawa huku 146,000 wakitoroka makazi yao.

Berlin ndiyo mwenyeji wa mkutano wa Amani utakaofanyika Januari 19, japo haijafahamika iwapo matokeo ya hivi karibuni huko Libya yataathiri mkutano huo.

Lakini kupata uhalisia wa kwa nini ni vigumu kufikiwa kwa makubaliano ya kusitisha vita, kinachohitajika kufanywa ni kurejelelea chimbuko la mapigano.

Tulifikaje hapo?

Kama ilivyotokea kwa Syria, ilianza tu kwa maandamano ya wakati wa vuguvugu la mapinduzi ya Arabuni 2011.

Vikosi vinavyoungwa mkono na Nato vilipindua utawala wa muda mrefu wa Muammar Gaddafimwaka huo, huku raia wakiwa na matumaini mengi tu si raia wa Libya pekee badi hata jamii ya kimataifa.

A member of Libyan National Army (LNA), commanded by Khalifa Haftar, is seen as he heads out of Benghazi

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Libya imekuwa katika vita tangu kuuawa kwa kiongozi wa muda mrefu Muammar Gaddafi, 2011

Tangu wakati huo, nchi hiyo imekuwa katika vita vya wenywe kwa wenyewe.

Baada ya miaka kadhaa ya mapigano, Umoja wa Mataifa ilisaidia kuanzishwa kwa utawala ulioongozwa na waziri mkuu Serraj.

Serikali yake ya Muungano wa Kitaifa ilikuwa mjini Tripoli na ilitarajiwa kuunganisha nchi hiyo.

Japo siyo kila mmoja aliyeunga mkono makubaliano hayo na Jenerali Haftar alitaka kuwa nguvu zaidi ya madaraka.

Aliunda jeshi lake la taifa mashariki mwa nchi hiyo kwa kuzingatia miji ya Tobruk na Benghazi.

Pia alidai kwamba anaweza kurejesha usalama na kupiga vita kile alichokiita ugaidi wa makundi ya kiislamu.

Vikosi vya Jenerali Haftar vimekuwa vikiingia kuelekea mji mkuu wa Tripoli tangu April 2019. Mwezi huu, vilifanikiwa kuteka mji wa kimkakati wa pwani wa Sirte.

Lakini ili kuchanganya mambo zaidi, wanamgambo wapo katika miji mbalimbali, wakipigana vita vyao na wakati hayo yakiendelea, kundi linalojiita Islamic State limejitokeza na kuendeleza shughuli zake katika maeneo mbalimbali ya jagwani.

Kina nani wanaochochea vita

Vita vya Libya kwa kiasi kikubwa vinafanan na vya Syria: makundi hasimu hayatokei tu nchiniLibya.

Pande zote za mgogoro wa Libya umevutia washirika wenye nguvu wa eneo na kimataifa.

Gen Haftar

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Gen Haftar has recruited powerful regional allies to his side

UAE na Saudi Arabia wanasema kwamba wanataka kumaliza makundi ya Kiislam katika eneo hilo. Kwa kujitokeza kama adui wa makundi ya Kiislamu yenye msimamo mkali, Jenerali Haftar alifanikiwa kuvutia nchi hizi upande wake.

Pamoja na Jordan, UAE imekuwa ikitoa silaha na usaidizi wa anga kwa Jeshi la taifa la Libya, na Umoja wa Mataifa imelaumu UAE kwa kusambaza silaha za kijeshi ambako kulisababisha mauaji ya raia wengi wakati Jenerali Haftar alifanya mashambulizi.

Misri, majirani wa Libya upande wa mashariki, wanamuunga mkono Jenerali Haftar na pia imekuwa ikiisaidia kwa masuala ya usafiri.

Na kwa wakati huu Urusi ambayo pia inatafuta kuwa na ushawishi pia imeingia kwenye vita hivyo. Inasemekana kwamba mamluki wa Urusi wamekuwa wakipigana na vikosi vya Jenerali Haftar ingawa Urusi imekanusha madai hayo.

Turkish members of parliament vote to send Turkish troops to Libya, in Ankara

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Wabunge wa Uturuki walipiga kura ya upande mmoja kutuma vikosi vya Uturuki Libya

Upande mwengine Uturuki, imetuma vikosi vyake kumuunga mkono waziri mkuu Serraj.

Kama ilivyo kwa Urusi, Uturuki pia inataka kuwa na ushawishi sku zijazo na kuonekana kama wenye nguvu katika eneo hilo. Serikali ya Uturuki imesema kwamba vikosi vyake vimepelekwa Tripoli kutoa mafunzo na ushauri.

Lakini chanzo katika serikali ya Haftar kimeithibitishia BBC kwamba vikosi vya Uturuki ni pamoja na wapiganaji wa waasi wa Syria wanaungwa mkono na Uturuki.

Kulingana na mwanahabari wa BBC Jonathan Marcus, nia ya Uturuki huenda ikawa inataka raslimali za baharini.