Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Trump ametishia kuiwekea vikwazo Iraq ikiwafukuza wanajeshi wa Marekani
Rais Trump ametishia kufanya mashambulizi kadhaa dhidi ya Iraq baada ya bunge lake kutaka Marekani kuondoa majeshi yake nchini humo.
"Tumewekeza kiasi kikubwa sana cha fedha katika jeshi la anga huko. Kujenga msingi wake imetugharimu mabilioni ya dola. Hatutaondoka labda kama watatulipa gharama tuliyotumia", aliwaambia waandishi wa habarai.
Mvutano bado ni mkubwa baada ya Marekani kuusika kumuua kiongozi wa jeshi wa Marekani jenerali Qasem Soleimani huko Baghdad wiki iliyopita.
Iran iliapa kulipiza kisasi.
Soleimani ambaye alifariki akiwa na umri wa miaka 62, alikuwa akiongoza operesheni za vita katika nchi za mashariki ya kati na alikuwa anatambuliwa na wamarekani kama gaidi.
Mabaki ya mwili wa jenerali sasa yamerejeshwa katika nchi yake Iran, eneo ambalo waombolezaji wamekusanyika barabarani katika mitaa ya Tehran.
Kiongozi mpya wa kikosi cha jeshi la Iran la Quds - ambacho Soleimani aliongoza - aliapa kuwaondoa Wamarekani katika mataifa ya mashariki ya kati.
"Tumehaidi kuendelea kuwa mashaidi wa Soleimani kwa kufuata muongozo wake... na kile ambacho tunaweza kukifidia dhidi ya kifo chake ni kuwaondoa wamarekani katika ukanda wetu,"radio ya taifa ilimnukuu Esmail Qaani.
Shambulio lililomuua Soleimani liliweza kumuua Abu Mahdi al-Muhandis, kiongozi wa juu wa jeshi a Iraqi ambaye aliwataka wairan kupambana na kundi la Kataib Hezbollah.
Ni mambo gani ambayo Trump ameitishia Iraq?
Akizungumza akiwa katika ndege ya rais, Trump alisema kuwa kama Iraq inataka majeshi ya Mareani yaondoke nchini mwake kwa nguvu, "Tutalipiza kwa kufanya mashambulizi ambayo hayajawahi kutokea kabla . Na kufanya vikwazo ambavyo Iran imeviweka kuwa vya kawaida sana."
Wanajeshi wa Marekani wapatao 5,000 wapo Iraq kama sehemu ya makubaliano ya kimataifa ya kupambana na kundi la kigaidi la kiislamu 'Islamic State' (IS).
Siku ya jumapili, azimio lilifikiwa na wabunge wa Iraqi kuwa majeshi yote ya kigeni yaondoke nchini humo.
Azimio hilo pia lilipitishwa na bunge la waislamu wa Shia ambao wako karibu na Iran.
Ni namna gani Iran imeijibu Marekani?
Iran imetangaza kuwa haitazingatia tenza vizuizi vilivyowekwa katika mkataba wa nyuklia kimataifa ulioanza mwaka 2015,
ambao ulikuwa unawapa fursa wakaguzi wa kimataifa kuweka kikomo cha matumizi ya nyukia kwa makubaliano ya kuondoa vizuizi vya kiuchumi.
Rais wa Marekani Donald Trump alipuuzia mkataba huo mwaka 2018, na kusema kuwa inataka kuwalazimisha Iran kujadili upya mkataba huo kwa madai kuwa itazingatia kuondoa vizuizi na kuboresha silaha zake za nuklia .
Iran ilitangaza kutozingatia makubaliano ambayo yapo kwenye mpango ambao walikubaliana.
Iran ilisema kuwa kuanzia sasa haitazingatia kikomo ambacho wamepangiwa kutumia katika utajiri wao kuanzia kwenye malighafi , utafiti na maendeleo .
Viongozi wa Ujerumani, Ufaransa na Uingereza ambao walikuwa ndio waliweka saini zao katika mkataba huo wa mwaka 2015 wakiwa pamoja na e China na Urusi - wamejibu kwa pamoja na kupinga kauli ya Iran na kudai kuwa itasababisha vurugu.
"Ni ngumu kwa sasa kujiondoa .Tunataka wahusika wote waliohusika katika mpango huu kuweka vizuizi na uwajibika," walisema.
Trump aliwaambia nini Iran?
Trump aliapa kushambulia Iran kwa namna kubwa zaidi katika malipizi hayo ya kifo cha Soleimani.
Vilevile siku ya jumapili alirejea kutishia kuvamia eneo la utamaduni la Iran, licha ya kukosolewa na mataifa mengine na hata ndani ya Marekani.
"Wanaruhusiwa kuwauwa watu wetu. Wanaruhusiwa kuwatesa watu wetu. Wanaruhusiwa kurusha mabomu na kuuwa watu wetu .Na haturuhusiwi kugusa sehemu yao ya utamaduni? Hatuendi hivyo," rais Trump alisema.
Siku ya jumamosi , Trump aliandika kwenye Tweeter kuwa Marekani imebainisha maeneo 52 ya Iran, baadhi yakiwa muhimu sana "Maeneo haya ni muhimu sana kwa Iran na utamaduni wa Irani", na kuwaonya kuwa atawapiga kwa haraka na nguvu zaidi kama Tehran itajaribu kuwachokoza.
Seneta wa Marekani Elizabeth Warren, ambaye ni mjumbe wa chama cha Democratic alijibu ujumbe wa tweet : "Unatishia kuanzisha uhalifu wa kivita."
Waziri wa mambo ya nje wa Iran Mohammad Javad Zarif alifananisha na uharibifu ambao kundi la IS limekuwa likiufanya katika utamaduni wa nchi za mashariki ya kati.
" Hii inakumbusha vita ya ISIS uhalifu uliolenga urithi wa utamaduni wetu," aliandika katika Tweet. "Katika historia ya MILLENNIA , barbarians ambao walikuja kuharibu miji yetu,kuharibu sanamu zetu na maktaba yetu. Wako wapi sasa? sisi bado tuko hapa imara."
Muda gani ambao Iran wanaweza kutumia kutengeneza bomu la nuklia?
Nchi hiyo imekuwa ikisisitiza kuwa mpango wake wa nyuklia huwa ni wa amani-lakini sasa kuna wasiwasi kuwa nyuklia itatumika kutengeneza bomu , walionya kitengo cha usalama cha Umoja wa mataifa, Marekani na Umoja wa ulaya ambayo ilitaka kuweka kikomo mwaka 2010.
Katika mkataba wa mwaka 2015 , mpango maalum ulibuniwa ili kuweka kikomo kwa makubaliano ya kuondoa vizuizi vya kiuchumi.
Iliweza kuwawekea vizuizi matumizi ya urani, ambayo pia yanatumika kutengeneza mafuta lakini pia kutengeneza silaha za nyuklia kwa 3.67%.
Iran ilitakiwa pia kutengeneza mfumo wa umeme wa maji ambao utatumia mafuta ambayo yangefaa kutengeneza bomu na kuruhusu ukaguzi wa kimataifa.
Kabla ya Julai 2015, Iran iliwekeza kiwango kikubwa cha urani chenye uwezo wa kutengeneza mabomu 10, kwa mujibu wa Ikulu ya Marekani wakati huo.
Wataalamu kutoka Marekani wakatik huo walikadiria kuwa kama Iran itaamua kutengeneza bomu basi itawachukua muda wa miezi miwili mpaka mitatu kutengeneza silaha za nyuklia.
Ila Iran kwa sasa kama itajaribu kutengeneza bomu la nyuklia inakadiriwa kuwa inaweza kumchuua karibu mwaka.