Wabunge wa Iraq wataka majeshi ya Kigeni kuondoka nchini humo

Wabunge wa Iraq wamepitisha azimio la kutaka vikosi vyote vya kigeni kuondoka nchini humo baada ya Marekani kumuua kiongozi wa juu wa jeshi la Iran, Jenerali Qasem Soleimani katika shambulio la anga lililofanywa kwenye uwanja wa ndege wa Baghdad, wiki iliyopita.

Bunge la Baghdad pia limetoa wito kwa wanajeshi wote wa kigeni wanaotumia ardhi ya Iraqi, maeneo ya anga au maji kwa sababu zozote kuondoka haraka.

Marekani ina wanajeshi 5,000 Iraq, kama washauri.

Maelfu ya raia wa Iraq walihudhuria ibada ya mazishi ya Soleimani kabla mwili wake haujapelekwa Iran.

Iraq imejikuta katika wakati mgumu kwa kuwa mshirika wa jirani yake Iran na wakati huohuo kuwa mshirika wa Marekani.

Maelfu ya wanajeshi wa Marekani wamebaki nchini humo kwa ajili ya kusaidia kuimarisha usalama dhidi ya wanamgambo wa kiislamu- Sunni Muslim Islamic State (IS).

Lakini hata hivyo serikali ya Washngton imeona kuwa mauaji hayo kama ni ukiukwaji wa masharti ya uwepo wao nchini Iraq.

Wakati huohuo makundi kadhaa ya wanamganbo wa Ki shia waliopo Iraq yamekuwa yakiungwa mkono na Iran, na kuna madai kuwa baadhi ya watu walihusika katika mauaji hayo na hivyo makundi ya kigaidi yanaweza kulipiza kisasi.

Bunge la Iraq limekutana wakati ambao mamia ya maelfu ya watu wmejitokeza nchini Iran i kuomboleza kifo cha Soleimani.

Azimio la kutofungamana na nchi nyingine lilipitishwa na bunge hii leo mara baada ya waziri mkuu Adel Abdul Mahdi, kutaka majeshi yote ya nje kuondoka.

Suala la kulipiza kisasi limekuwa likijirudia rudia Iran tangu mauaji ya Soleimani, ambayo yalifanya kuhoji sera za Marekani katika mataifa ya mashariki ya kati.

Azimio linataka nini haswa ?

Azimio hilo linatana serikali kufuta ombi lake la kutaka usaidizi wa kimataifa kupambana na wanamgambo wa IS ili kuweza kutokomeza operesheni za kijeshi na kupata ushindi wa mapambano hayo.

Linasema kuwa serikali ya Iraqi lazima ifanyie kazi suala la kuondosha vikosi vya kijeshi vya kigeni katika maeneo ya Iraqi na kuwakataza kutumia ardhi , anga au maji ya Iraq kwa sababu zozote.

Vilevile serikali lazima ipeleke malalamiko kwa umoja wa mataifa dhidi ya Marekani kwa kukiuka masharti na kuhatarisha usalama.

Waziri wa nchi hiyo baada ya kura kupigwa, alisema kuwa majeshi ya Marekani yanapaswa kutokuwepo Iraq haraka iwezekanavyo.

Kusitisha uwepo wa jeshi la Marekani nchi Iraq, waziri mkuu alisema kuwa ni jambo bora zaidi ili kusahihisha uhusiano wa nchi yake na Marekani na mataifa mengine.