Mti wa Krismasi uliotengenezwa kwa visu, risasi, na viberiti vya kuwashia sigara

Chanzo cha picha, Martynas Jaugelavicius
Kama unahisia za sherehe za Krismasi huenda unafikiria kutengeneza mti wa Krismasi katika sebule yako na kuupamba kwa taa zinazometameta.
Lakini bila shaka hatutarajii uwe mti unaoning'ingia visu, risasi na viberiti vya kuwasia sigara.
Uwanja wa ndege wa Vilnius nchini Lithuania umefichua mti mbadala wa msimu wa sherehe za Krsimasi- Uliotengenezwa na vifaa vilivyokamatwa kutoka kwa wasafiri pekee.

Chanzo cha picha, Martynas Jaugelavicius
Mti huo wenye urefu wa kimo cha mita 1.5 au (futi 5) ulichukua wiki mbili tu kuutengeneza, lakini maana ya thamani yake bado haijakamilika.
"Lengo ni kutuma ujumbe wa kuelimisha juu ya umuhimu wa usalama wa safari za anga," alisema msemaji wa uwanja wa ndege wa Vilnius Airport.
"Vifaa hivi vinazuiwa kubebwa katika mabegi ya wasafiri ya mkononi na vilichukuliwa kutoka kwa wasafiri walipokuwa wakikavuliwa. visu, mikasi,viberiti vya kuwasha sigara, na kila aina ya vifaa vingine hatari.
"Kwa hiyo kama hautaki vifaa vyako vya kibinafsi, ambavyo vimezuiwa, visiishie katika mti wa Krismasi ya mwaka ujao, ni bora uangalie masharti ya ubebabi wa begi la mkononi unaloingia nalo kwa ndege kabla ya safari yako ya ndege ."

Chanzo cha picha, JANE BARLOW/PA WIRE
Na sio uwanja wa ndege wa Lithuanian apekee ulioonyesha ubunifu wa dhana ya mti wa krismasi mwaka huu .
Kijiji cha Ullapool, kilichopo kwenye mwambao wa West Highlands, kimesimamaisha 'mti'' wa mita 9 uliotengenezwa kwa nyavu za kunasia samaki..
Umetengenezwa kwa vifaa hivyo vilivyoundwa kwa nyavu 340 vinavyotumiwa kunasa samaki baharini -na ni mtindo wa hivi karibuni wa utamaduni wa Ullapoo ulionza mwaka 2016.

Chanzo cha picha, Getty Images
Umaarufu wa kutotumia miti asilia inayotumiwa kwa ajili ya Krismasi unaweza pia kupungua kwa watu ambao ni makini katika kuhakikisha shere za krisimasi pia zinaendana na utunzaji wa mazingira.
Kwamujibu wa shirika la Marafiki wa Dunia, zaidi ya miti milioni 8 ya Krismasi hununuliwa nchini Uingereza pekee kila mwezi Disemba. Hicho ni kiwango kikubwa kinachoweza kuathiri mazingira.
Njia mbadala ya kudumu ya kuhifadhi mazingira ni pamoja na kupanda miti yako mwenyewe, kukodisha mti mmoja au kuhakikisha tu unaichoma , ipande au uipatie serikali unapomaliza kuitumia ili kuhifadhi mazingira.

Chanzo cha picha, Getty Images
Na katika jimbo la Florida lenye jua nchini Marekani, ambako wastani wa joto mwezi Disemaba ni takribani nyuzijoto 22°C, timu ya mpira wa magongo iliamua iliamua kuvaa nguo za msimu wa baridi uwanjani wakati wa jua
yote ni katika kusherehekea Krismasi he, heh. he'
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe













