Aung San Suu Kyi: Kwanini Gambia imeishutumu Myanmar kwa mauaji ya jinai dhidi ya ‘Warohingya’? Gambia yaishtaki Myanmar

Kiongozi wa Myanmar, Mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobeli, Aung San Suu Kyi, amekanusha madai ya kwamba nchi yake ilitekeleza mauaji ya kimbari dhidi ya kundi la Waislamu waliowachache la Rohingya, akisema kwamba hakuna ushahidi wowote wa nia ya utekelezaji mauaji ya kimbari katika oparesheni iliyotekelezwa na jeshi la Myanmar.

Alikuwa akijibu mashtaka yaliyowasilishwa na Gambia kwenye Mahakama ya kimataifa ya ICC huko The Hague wakati wa kusikilizwa kwa kesi hiyo iliyoanza jana Jumatatno.

"Leo hii Jahuri ya Gambia inataka mahakama hii isikilize kilio cha Warohigya kutaka usaidizi na malalamiko yao ya utekelezwaji wa mauaji ya kimbari," amesema Aboubacarr Tambadou alianza kwa kusema hivyo katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ).

Kesi ya mauaji ya kimbari dhidi ya serikali ya Myanmar inaungwa mkono na wanachama 57 wa Muungano wa vyama vya Kiislamu na Timu ya Mawakili ya Kimataifa lakini waziri wa haki ya Gambia ndiye aliyewasilisha keshi hiyo.

"Kwanini Gambia imechukua hatua hii?"

Maelfu ya Warohingya waliuawa huku wengine zaidi ya 700,000 wakitorokea nchi jirani ya Bangladesh wakati wa oparesheni ya kijeshi iliyotekelezwa mwaka 2017.

Hatua iliyochukuliwa na jeshi la Myanmar na kiongozi wa nchi hiyo Aung San Suu Kyi imekosolewa vikali.

Baadhi hata wanataka kamati ya Nobeli imvue tuzo la amani ambalo ilikuwa imempatia.

Lakini nchi ya Afrika Magharibi ya Gambia iliyo kilomita elfu kadhaa kutoka Myanmar, ndio ambayo imeamua kuchukua jukumu la kuishtaki Myanmar.

"Kwanini Gambia imechukua hatua hii? Kwanini tuachie nchi zingine jukumu hili?" Amesema Aboubacarr Tambadou.

"Sheria ya Kimataifa siyo tu ya nchi matajiri bali ya watu wote. Huna haja ya kuwa na uwezo mkubwa wa kijeshi au kiuchumi ili utafute haki, ama ufanye kile kilicho sawa," ameiambia BBC.

Kushindwa kuwajibika kwa mara nyengine tena

Wakili huyo ambaye amekuwa mwanasiasa anafahamika kwa kazi yake ya kushtaki wahalifu walihusika na mauaji ya kimbari nchini Rwanda

"Gambia inatumia maadili yake kushtumu mauaji ya kimbari ya Myanmar kwa raia wake wenyewe. Nafikiri jamii ya kimataifa inastahili kufanya hivyo. Dunia iliisaliti Rwanda mwaka 1994. Na wakati pia tunasaliti jamii ya Warohingya."

Hii ndiyo mara ya kwanza nchi ambayo haina uhusiano wa moja kwa moja na madai yanayodaiwa kutekelezwa kuwasilisha kesi katika mahakama ya ICJ kwa kutumia uanachama wake kwenye mkutano wa mauaji ya kimbari wa Umoja wa Mataifa.

Unaweza pia kutazama video hii

"Uvundo wa mauaji ya kimbari"

Tambadou alitembelea Bangladesh Mei mwaka 2018 kisha akatembelea kambi ya Warohingya na hali aliyokutana nayo ilimpa nguvu ya kupigania wakimbizi hao.

"Wakati nasikiliza simulizi za wakimbizi wakiwa kambini, nilihisi yaliyotokea katika mpaka wa Myanmar," ameiambia BBC.

Anasema alikasirika zaidi baada ya kujionea na kusikia yale waliyopitia wakimbizi hao na kuchukulia utafutaji wa suluhu kama jukumu lake.

"Na papo hapo nikawaza kwamba kuna kitu ambacho kinastahili kufanywa," akasema.

Kilio cha wengi

Alisikiliza simulizi za wengi za kukosa matumaini wakati wa mauaji hayo, ubakaji, mateso na watoto kuchomwa moto wakiwa hai wakiwa majumbani mwao na maeneo ya kuabudu.

Mabaya dhidi ya Waislamu wa Rohingya halikuwa jambo geni kwa Myanmar - walikuwa wametengwa na kushuhudia ghasia tangu nchi hiyo ilipojipatia uhuru.

Lakini miaka miwili iliyopita oparesheni ambayo iliratibiwa na jeshi iliharibu vijiji vyote na kuwafurusha zaidi ya watu milioni moja na kuwa wakimbi za ndani ya nchi ama kulazimika kukimbilia nchi za Malaysia, Thailand au Indonesia, pamoja na Bangladesh.

Ghadhabu na ushahidi uliopo

Kiwango cha wakimbizi kilichoingia Bangladesh kilisababisha mgogoro wa kibinadamu

Baadhi ya nchi zilipeleka msaada kwa haraka. Mataifa mengine yalitoa onyo.

Picha za setilaiti, zilitoa hofu kuhusu ukubwa wa uharibu uliofanyika na kupelekea shtuma dhidi ya Myanmar lakini hakuna kilichositisha oparesheni ya jeshi la Myanmar.

Gambia inataka jamii ya kimataifa kuchukua hatua.

"Nasimama mbele yenu kuleta wazi dhamira ya dunia na kupaza sauti z jamii ya kimataifa. Katika maeneno ya Edmund Burke... 'Kwa adui kupata ushindi kinachohitajika ni watu kutofanya chochote peke yake'" Tambadou aameiambia ICJ.

"Wahamiaji Haramu"

Myanmar, nchi ambayo wengi wao ni waumi wa kibuddha, waliwachukulia watu wa jamii ya Rohingya kutoka Bangladesh, kama wahamiaji haramu na kuwanyima uraia.

Pia unaweza kusoma:

Tangu mwaka 1962, serikali ya Myanmar imekuwa ikikandamiza haki za kisiasa na kiraia kwa Waislamu wa Rohingya ikiwemo haki yao ya kupata uraia, kulingana na Umoja wa Mataifa.

Hizo ni baadhi ya zilizokuwa hoja za waziri wa Gambia wakati wa kusikilizwa kwa kesi hiyo kwenye mahakama ya ICJ.

"Mauaji ya kimbari hayatokeo bila sababu. Huyatokei tu bila msingi. Hutanguliwa na historia yenye kutiliwa mashaka, ukosefu wa uaminifu, propaganda za chuki ambazo zinadunisha wengine na kujijenga hadi kuwa machafuko ambapo kundi moja linataka kudhuru ama kuangamiza kabisa kundi jengine."