Masaibu ya msichana aliyebakwa na ''marafiki za baba yake''

Wall of the girl's house

Chanzo cha picha, NEBULA MP

Maelezo ya picha, Msichana huyo aliandika michoro kwenye ukuta wa nyumba yao.

Kila mwishoni mwa juma kwa miaka miwili , wanaume walikua wakija na kumbaka, aliwaambia washauri msichana mwenye umri wa miaka 12 , baadhi wakifahamiana na baba yake, na baaadhi hawakua wanafahamiana nae.

Onyo: Tarifa hii ina baadhi ya maelezo ambayo yanaweza kuwaogofya baadhi ya wasomaji.

Yote yalianza, anasema kwa baba yake kwa kuwakaribisha wageni nyumbani kwao kwa vinywaji. Wanaume hao walikua wakimtania kwa maneno ya mzaha mbele ya wazazi wake . Anasema wakati mwingine wanaume hao walikua wakitoweka na kuingia na mama yake katika chumba cha wazazi cha kulala.

Halafu siku moja, msichana huyo anakumbuka, baba yake alimsukuma ndani ya chumba cha kulala na mmoja wa marafiki zake wa kiume na kufunga mlango wa chumba kwa nje. Mwanaume akambaka.

Mara moja utoto wake ukageuka kuwa balaa. Baba yake alikua akiwaita wanaume, akipanga muda wao na binti yake, na kuchukua pesa kutoka kwao. Mshauri nasaha anaamini kuwa alibakwa na wanaume takriban 30 tangu wakati huo.

Tarehe 20 Septemba, maafisa wa masuala ya watoto, waliopata taarifa kutoka kwa waalimu, walimuoko msichana huyo kutoka shuleni na kumpeleka katika nyumba ambako alihifadhiwa. Uchunguzi wa kimatibabu ulithibitisha kuwa alibakwa , kulingana maafisa wa masuala ya watoto.

A protest in India against child sex abuse

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Crime figures show a child is abused every 15 minutes in India

Wanaume wanne, akiwemo baba yake ,wamekamatwa kuhusiana na tukio hilo. Wameshtakiwa kwa ubakaji, kumtumia mtoto kwa madhumuni ya ponografia na unyanyasaji wa kingono. Wote wamenyimwa dhamana.

Polisi wanawaska wanaume watanozaidi ambao wanafahamiana na baba yake ambao wanadaiwa kumbaka na kumnyanyasa jingono msichana huyo. Wapelelezi wanaorodha ya majina na picha za wanaume wapatao 25 wanaofahamiana na familia yao ambao wamekua wakipelekwa kwa msichana huyo.

"Sikumbuki sura yoyote. Ni giza tu,'' aliwambia.

Familia iliishi katika mji wenye mafanikio kusini mwa India, wenye milima, hewa safi na maji safi. Lakini utajiri huo mzuri unaonekana kutoifikia familia yake.

Katika siku ile mwezi wa Septemba, shule ilipokea taarifa kutoka kwa waalimu kadhaa ambao wanaishi karibu na familia ya msichana .

"Kuna kitu ambacho sio kizuri katika familia yake na kuna kitu kinaendela katika nyumba yao.Jaribu kuzungumza nae," walisema.

Utawala wa shule mara moja ulimuita mshauri nasaha kutoka kikundi cha usaidizi cha wanawake.

Asubuhi iliyofuatia, mshauri nasaha akafika.

The girl's notebook

Chanzo cha picha, NEBULA MP

Waliketi ana kwa ana katika chumba cha walimu. Katika chumba cha juu gorofani , mama yake hakujua ni nini kinachoendelea katika ofisi ya walimu, alifikiri anahudhuria mkutano wa kawaida wa waalimu na wazazi.

"Niambie kuhusu familia yako na maisha yako."mshauri nasaha alimwambia msichana

Waliongea wa saa nne.

Msichana alisema kuwa alikua anapitia kipindi kigumu nyumbani kwao kwasababu baba yao hakuwa na ajira. Familia inaweza kufukuzwa wakati wowote kwa kushindwa kulipa nyumba, akaanza kulia.

Halafu akakaa kimya kwa muda. Mshauri nasaha alimwambia kuhusu masomo ya jinsia katika shule yao na namba tatizo la unyanyasaji wa watoto lilivyo la kawaida.

"Kuna kitu pia kinachofanyika katika nyumba yetu. Baba yangu anamnyanyasama mama yetu," alisema msichana huyo.

Mshauri alimuomba kama anaweza kumshirikisha zaidi kitu hicho.

Unaweza pia kusoma:

Alisema aliwahi kupigwa na mwanaume ambaye alikua amekuja kumuona mama yake. Mama yake alikua amemuonya mwanaume huyo. Lakini mwanaume huyo akaja kumuona mama yake alipokua ameenda shuleni, alisema.

Wanaume zaidi zaidi wakaanza kuwa wanakuja nyumbani kwao. Bada ya kunywa pombe, walikuwa wanamnyanyasa kingono, alisema msichana huyo.

Mshauri nasaha alimuuliza ikiwa alifahamu kuhusu dawa za kuzuwia ujauzito ambazo zilimsaidia kuepuka kubeba mimba na magonjwa.

"Hapana, hapana, tunatumia mipira ya kondomu," alisema msichana huyo.

Hiyo ilikuwa ni mara ya kwanza, katikati ya mazungumzo, alikiri kufanya ngono.

People take out protest march against the brutal rape case in Kathua from Galleria market to sector 29, Rangbhoomi open-air theatre on April 18, 2018 in Gurgaon, India

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Recent cases of child sex abuse in India have prompted public outrage and protests

Baada ya hayo alielezea hadithi ya kutisha ya kupoteza utoto wake.

"Wanaume huwa wanakuja na kumchukua mama yangu katika chumba cha kulala. Nilifikiri lilikuwa ni jambo la kawaida. Halafu mama yangu alinisukuma chumbani na wanaume ambao nilikuwa siwajui ,"alisema.

Wakati mwingine baba yake alimlazimisha kupiga picha zake za utupu na kuzituma kwa wanaume ambao walimtembelea.

Mapema mwaka huu, wazazi wake waliingiwa na hofu alipokosa damu yake ya mwezi kwa miezi mitatu. Walimpeleka kwa daktari , ambao waliagiza afanyiwe uchunguzi wa tumbo na akapatiwa dawa.

Wakati huo, mshauri nasaha aliamini kuwa amekuwa muhanga wa ubakaji sugu. Aliwaita maafisa wa maslahi ya watoto, na akamwambia msichana kuwa wanampeleka katika makazi ya kumuhifadhi. Alionekana mwenye wasi wasi.

Mama yake alipotoka kwenye mkutano na waalimu wake, alipomuona akipelekwa ndani ya gari alipiga kelele.

"Mnawezaje kumpeleka mtoto wangu mbali na mimi?"

Mshaurinasaha alimwambia kuwa wanampeleka kwasababu ana "matatizo ya hisia" na anahitaji kupewa ushauri nasaha.

"Wewe ni nani kumpatia binti yangu ushauri nasaha bila ruhusa yangu?"

Binti yake alikuwa tayari njiani kuelekea nyumbani. Kwa miezi miwili iliyopita, amekuwa akiishi na wasichana wengine- wote waathiriwa wa unyanyasaji wa kingono.

India inarekodi ya aibu ya unyanyasaji wa kingono dhidi ya watoto. Wingi wa unyanyasaji huo hufanywa na watu wanaofahakika kwa waathiriwa , kama vile ndugu, majirani na waajiri, kwa mujibu wa rekodi rasmi.

Mwaka 2017, kulikuwa na visa 10,221 vya ubakaji wa watoto vilivyorekodiwa nchini India. Uhalifu dhidi ya watoto nchini humo umekuwa ukiongezeka katika miaka ya hivi karibuni.

graphic
Maelezo ya picha, Visa vilivyorekodiwa vya unyanysaji dhidi ya watoto hadi 2017
Presentational white space

Washauri nasaha wanasema kuwa visa vya kutisha hadithi ya aina hiyo vya kutisha sio vya kawaida. Katika makazi ambako wasichana wamekuwa wakiishi, kuna wasichana watatu wenye umri kati ya miaka 12 na 16, ambao wamekuwa wakinyanyaswa kingono na baba zao.

Mshauri nasaha alisema kuwa alimsaidia kumsafirisha msichana mwenye ujauzito mkubwa wa miaka 15- ambaye alikuwa amebakwa na baba yake kufika kwenye chumba cha mtihani.

"Tulipomuomba msichana aache mtoto wake alipozaliwa, alisema , 'Ni kwanini nimgawe mtoto wangu?. Huyu ni mtoto wa baba yangu. Nitamlea mtoto ,'" alisema mshauri nasaha.

Katika makazi, msichana tunayemzungumzia katika taarifa hii alilala usingizi mzito mfulurizo katika siku chache za mwanzoni alipoletwa. Halafu akachora mchoro juu ya ni kwa kiwango gani alimpenda (mama yake)Amma.

Mama yake anasema binti yake "aliunga hadithi hiiya kunyanyaswa kingono, kwasabu amekuwa akipambana na sisi na alitaka kutoa funzo ".

Kulikuwa na wakati , mama yake alisema, wakati mambo yalipokuwa mabaya sana. Mume wake wakati mwingine alikuwa akitengeneza hadi rupia 1,000 (taktiban $14; ) kwa siku katika kazi yake.

Door of the house

Chanzo cha picha, NEBULA MP

Maelezo ya picha, After an argument with her mother, the girl wrote she was sorry on the front door

Kwa sasa anaishi peke yake ndani ya nyumba- mume wake yuko gerezani, akisubiri kesi , binti yake yuko katika makazi ya hifadhi.

"Mimi ni mama anayejali, Ananihitji," mama yake msichana aliiambia BBC.

Mchoro unafutika kwenye kuta za nyumba. huku binti yake akiwa hayupo, mchoro ndio kitu kinachomkumbusha mwanae. "Alikuwa anachorakwenye kuta. Hilo ndilo alilokuwa akilifanya," alisema mama yake.

"Marafiki . Kama ningeweza kuelezea wazi hisia zanguza ndani yangekuwa ni mafanikio ," msichana alikuwa ameandika kwnye karatasi na kuibandika kwenye mlango.the girl had written on paper and

Miezi michache iliyopita, mama na binti yake walikuwa wamezozana.

Wakati msichana alipotoka shuleni, alichukua kalamu ya blu, akachora picha ya mti wa mawesena nyumba ikiwa na moshi unaofuka mbele kwenye mlango wa nyumba. Ni kitu ambacho wasichana wenye umri wake wangekichora akilini kutoka katika fikra zao.

Halafu akaandika ujumbe wa msamaha haraka katika mlango na akaenda nje.

"Sorry Amma," aliandika msichana.