Maandamano ya Hong Kong: Trump atia saini muswada wa haki na demokrasia kuwa sheria

Chanzo cha picha, Reuters
Rais wa Marekani Donald Trump ametia saini muswada wa sheria unaounga mkono waandamanaji wa Hong Kong.
Sheria ya haki za binaadamu na demokrasia inataka kufanyika kwa tathimini ya mwaka, kutazama kama Hong Kong ina uhuru wa kutosha.
Wizara ya mambo ya nje ya China imesema '' itachukua hatua kali'' - ikiishutumu Marekani kwa ''nia yake mbaya''.
Trump hivi sasa anatafuta makubaliano na China ya kumaliza vita ya kibiashara kati ya nchi hizo mbili.
Serikali ya Hong Kong pia imezungumzia hatua hii ya Trump na kusema kuwa muswada wa Marekani unapeleka ishara mbaya na hautasaidia lolote katika kutatua hali hii.
Unaweza pia kusoma
Lakini mmoja wa viongozi wa maandamano ya Hong Konga, Joshua Wong, amesema sheria ya Marekani ni '' mafanikio makubwa'' kwa wakazi wote wa Hong Kong''
Trump awali hakuwa akizungumza kama atatia saini muswada au la, akisema alikuwa ''pamoja'' na wakazi wa Hong Kong lakini pia Bwana Xi alikuwa ''mtu mzuri ''
Trump pia alitia saini muswada, ambao unapiga marufuku usafirishaji wa silaha zinazokabili makundi ya watu kwa polisi wa Hong Kong- ikiwemo gesi za kutoa machozi, risasi za mpira na silaha za kushtua.
''(miswada) hiyo imepitishwa kukiwa na matumaini kuwa viongozi na wawakilishi wa China na Hong Kong wataweza kumaliza tofauti zao kwa amani ya kudumu na ustawi kwa wote,'' Alisema Trump.
Sheria inasema nini?
Muswada ulitambulishwa mwezi Juni wakati wa hatua za mwanzo kabisa za maandamano ya Hong Kong, muswada ukapitishwa na bunge la wawakilishi mwezi uliopita.
Unasema: ''Hong Kong ni sehemu ya China lakini kwa kiasi kikubwa zinatofautiana kwa mifumo ya kisheria na kiuchumi.
''Mapitio ya mwaka yatatathimini kama China imezingatia utawala wa sheria.
Miongoni mwa mambo mengi, biashara ya Hong Kong haita athiriwa na vikwazo vya Marekani na kodi zilizowekwa dhidi ya eneo la bara.
Muswada huo unasema Marekani itawaruhusu wakazi wa Hong Kong kupata Viza za Marekani, hata kama waliwahi kukamatwa kwa kushiriki maandamano ya amani.

Chanzo cha picha, Reuters
Hali ikoje Hong Kong?
Maandamano ya Hong Kong yalianza mwezi Juni dhidi ya sheria iliyopendekezwa kuruhusu watu kwenda kuhukumiwa China, mapingamizi ambayo yalizusha maandamano ya kuunga mkono demokrasia.
Maandamano yamesababisha makabiliano, polisi wakishambuliwa, na maafisa wakifyatua risasi.
Waandamanaji wamerusha mabomu ya petroli na kuharibu biashara.
Waandamanaji, wamewashutumumu polisi kufanya mashambulizi ya kikatili dhidi yao.













