Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Ndege ya abiria 18 yaanguka katika mji wa Goma mashariki mwa DR Congo
Takriban watu 24 wanaaminika kufariki baada ya ndege waliokuwa wakiabiri kuangukia katika mji wa Goma mashariki mwa jamhuri ya kidemokrasia ya Congo.
Gavana wa jimbo la Kivu kaskazini Nzanzu Kasivita Carly amesema kwamba watu wamefariki lakini hakutoa idadi kamili .
Ndege hiyo ilianguka juu ya nyumba katika eneo jirani la Mapendo baada ya kushindwa kupaa katika uwanja wa ndege wa mji huo , aliongezea.
Wakaazi wa eneo hilo ni miongoni mwa waathiriwa wa ajali hiyo, kulingana na vyombo vya habari vya eneo hilo.
Ndege hiyo aina ya Doenier 228 ilikuwa ikimilikiwa na kampuni binafsi ya Busy Bee.
Ilitarajiwa kuelekea Beni yapata kilomita 350 kutoka kaskazini mwa Goma, wakati ilipoanguka dakika moja baada ya kupaa kulingana na chanzo kimoja katika mji wa Goma kilichozungumza na BBC.
Ajali za ndege hutokea mara kwa mara nchini DR Congo , kutokana na viwango vya chini vya usalama na kutorekebishwa kwa ndege hizo.
Ndege zote za kibiashara za taifa hilo zimepigwa marufuku kufanya biashara katika Muungano wa Ulaya.