Ni kwanini rais wa Ufaransa Emmanuel Macron anasema Muungano wa Nato una ubongo uliokufa?

Rais wa ufaransa Emmanuel Macron ameuelezea Muungano wa Nato kama "ubongo" uliokufa, akisisitiza kile anachokiona kama kutowa na utashi wa mdhamini mkuu wa Marekani kwa Muungano huo wa kujihami wa nchi za magharibi.

Akihojiwa na gazeti la Economist, alielezea kushindwa kwa Marekani kuomba ushauri kwa Nato kabla ya kuondoa vikosi vyake kaskazini mwa Syria.

Aidha pia alionyesha kuwa na wasi wasi juu ya ikiwa wajumbe wa Nato bado wana utashi wa kuwa na ushirikiano wa pamoja wa kiulinzi.

Unaweza pia kusoma:

Nato inaadhimisha miaka 70 tangu ilipoanzishwa katika mkutano utakaofanyika mjini London mwezi ujao.

"Tunachokishuhudia kwa sasa ni kufa kwa ubongo wa Nato ,"Bwana Macron aliliambia gazeti hilo lenye makao yake mjini London.

Tuliwaonya wanachama wa Muungano wa Ulaya kwamba hawawezi tena kuitegemea Marekani kuulinda Muungano wa Nato , ulioanzishwa katika mwanzo wa Vita baridi kwa ajili ya kuboresha usalama wa Ulaya magharibi na Marekani.

Ibara ya Tano ya malengo ya kuanzishwa kwa Nato inaelezea kwamba shambuli dhidi ya mjumbe mmoja litalipizwa kwa jibu la kijeshi kutoka kwa wajumbe wa Muungano huo kwa pamoja.

Lakini Bwana Macron anaonekana kuwa hana uhakika ikiwa bado kipengele hicho kinathamani tena , alipoulizwa alisema:"Sijui ,"

Bwana Macron amenukuliwa akisema ''Muungano unafanya kazi tu kama mdhamini au mtu mwenye maamuzi ya mwisho anafanya kazi ya aina hiyo . Ninasema kwamba tunapaswa kutathmini upya ukweli kuhusu Nato ni nini.

Unaweza pia kusoma:

Rais wa Ufaransa ameitaka Ulaya kuanza kjifikiria binafsi katika muktadha "nguvu yake ya kisia kwa kuzingatia uwajibikaji wa Marekani ".sa kijiografia " ili kuhakikisha inabakia "katika udhibiti " wa mustakbali wake.

Ni kwanini wasiwasi juu ya Nato?

Uamuzi wa ghafla wa rais Donald Trump wakuondoa vikosi vya Marekani kaskazini mashariki mwa Syria mwezi Oktoba kuliwashangaza wajumbe wa Nato kutoka Muungano wa Ulaya.

Hatua hiyo ilifungua njia kwa Uturuki - yenyewe ambayo ni mjumbe mwenye mamlaka wa Nato - kuingia nchini Syria na kubuni kile ilichokiita eneo la usalama kwenye mpaka wake . Vikosi vya Wakurdi ambavyo vimekuwa vikiisaidia Marekani kupigana na kundi la Islamic State (IS) walifukuzwa katika eneo hilo.

Bwana Macron wakati mmoja alikosoa kufeli kwa Nato kujibu mashambulio ya Uturuki .

Bwana Trumo mara kwa mara amekuwa akiwatuhumu wajumbe wa Muungano wa Nato wa Ulaya kwa kushindwa kutoa michango yao ya matumizi ya kijeshi na kuitegemea sana Marekani katika ulinzi wa Mataifa yao.

Kwa upande wake Bwana Macron amekuwa mstari wa mbele katika hatua za kuinua ushirikiano wa ulinzi miongoni mwa mataifa ya Ulaya. Hata hivyo , Taifa kubwa la Muungano wa Ulaya Uingereza inasisistiza juu ya umuhimu wa Nato kwa ulinzi wa Ulaya.

Haifai tena kwa malengo yake?

Huku wiki mbili tu zikiwa zimesalia kabla ya kikao cha Nato, kauli za Macron zinaonyesha kuwa hautakuwa sherehe ya amani.

Moja ya kasoro kuu lililopo limekuwa ni uwazi wa Trump ambaye mara kwa mara amekuwa akiwa akiwabeza washirika wake wa Muungano wa Nato allies.

Aliwaelezea wengi wao hivi karibuni kama ''wadanganifu'' kwa kutogarimia ipasavyo ulinzi wao wenyewe.

Bwana Macron alisema kuwa Marekani inaipa kisogo Ulaya. Ukosefu wa uratibu na kufanya maamuzi ya kimkakati baina ya Marekani na washirika wake wa Nato umedhihirishwa na maamuzi ya kipekee ya hivi karibuni ya Marekani na uturuki ndani ya Syria.

Hatua ya Uturuki , alisema kuwa iliibua maswali mengi , kuhusu hakikisho la kimsingi la usalama linalotolewa na Nato kwa wajumbe wake. Ni nini kitakachotokea kwa mfano , aliuliza, kama serikali ya Syria itaishambulia Uturuki kutokana na uvamizi wake ndani ya Syria ?

Ikiwa na wajumbe wengi kuliko wakati wote na ikikakakabiliwa na changamoto ngumu za kiusalama , Nato inaonekana kwa mtizamo wa Bwana Macron haifai kwa malengo yake.

Hii ni zaidi na zaidi ya rais mmoja wa marekani . Nato lazima ijilinde dhidi ya vitisho ambavyo nchi mbali mbali zinaviona kwa njia tofauti. Na washirika kadhaa wanaonekana hawako makini kuonyesha maadili ya uhuru wa kidemokrasia ya Nato.