Mmusi Maimane: Kiongozi wa upinzani Democratic Alliance ajiuzulu

Chanzo cha picha, Getty Images
Kiongozi wa kwanza mweusi wa chama rasmi cha upinzani Afrika kusini amejiuzulu kufuatia mzozo unaotokana na ubaguzi wa rangi ndani ya chama chake Democratic Alliance.
Mmusi Maimane amesema chama hicho hakiweza tena kuwa chombo stahiki kwa malengo yake ya kuwepo taifa lenye umoja.
Maimane ameeleza kwamba alipata tabu katika kukifanya chama hicho ambacho kwa muda mrefu kimekuwa na wafuasi weupe wa kiberali - kuwavutia wapiga kura weusi.
"Nitajiuzulu kama kiongozi wa DA... lakini nitasalia kama mbunge," amesema.
"Kuna muda wa viongozi kukaa kando na kufanya ukaguzi wa kisawasawa," aliongeza.
Kujiuzulu kwake kunajiri siku tatu baada ya Herman Mashaba kujiuzulu kutoka chama hicho na pia kama meya wa mji wa Johannesburg.
Hii inafuata uteuzi wa kiongozi wa zamani wa chama hicho, Helen Zille, kama mwenyekiti wake, na wadhifa wa pili wenye nguvu ndani ya chama hicho.
Maimane alizozana na Bi Zille mnamo 2017 baada ya Zille kutukuza kwa kiasi fulani utawala wa kikoloni.
Kituo cha televisheni nchini kimeweka video ya tangazo la Maimane kujiuzulu:
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe


Chanzo cha picha, AFP
Mambo saba kuhusu Mmusi Maimane
- Alizaliwa mwaka 1980 kitongoji cha Soweto, Johannesburg ambapo Nelson Mandela aliishi kwa miaka mingi.
- Amesoma vyuo vikuu nchini Afrika Kusini na Wales, ana Shahada ya Uzamivu katika masomo ya Teolojia na Saikolojia.
- Ameoa mwanamke wa kizungu Natalie, ambaye walikutana kanisani, na kukiri kuwa ilimchukua muda kukubaliana na jamii inavyochukulia tofauti yao.
- Anaongea lugha sita.
- Amekuwa akihubiri kanisani jijini Johannesburg mwishoni mwa wiki kwa miaka kadhaa sasa.
- Alikuwa mshauri wa kibiashara kabla ya kuingia kwenye siasa, na kuwa msemaji wa DA mwaka 2011.
- Alichaguliwa kuwa kiongozi wa kwanza mweusi wa DA mwaka 2015 akiwa na miaka 34.

Hatua hii ina maana gani kwa upinzani Afrika kusini?
Mwandishi wa BBC anasema hii ni hatua ya kushangaza, huenda pia ni pigo kwa upinzani rasmi nchini Afrika kusini.
Mmusi Maimane amesema anajiuzulu kutokana na kukosa imani ndani ya chama ambacho amekiongoza kwa miaka minne iliyopita.
Hakulieleza bayana, lakini ameashiria kuwa iadi ndogo ya watu weupe ndani ya chama hicho inazuia jitihada zake kuwafikia wapiga kura zaidi weusi na kushughulikia wasiwasi wao kuhusu dhulma za ubaguzi wa rangi.
Chama cha DA kilipoteza uungwaji mkono katika uchaguzi uliopita na kinagubikwa kwa mizozo tata ya ndani ya chama.
Raia wengi wa Afrika kusini wanaamini demokrasia changa inahitaji upinzani wenye nguvu kukabiliana au hata pia kukiondoa madarakani na chama tawala cha ANC.
Katika muda wa miaka ishirini na tano, chama cha Democratic Alliance ndicho kilichoikaribia nafasi hiyo.
Lakini kuondoka sasa kwa kiongozi wake wa kwanza mwuesi ni pigo, au angalau, hatua inayokirudisha nyuma chama hicho.















