Sakata la Escrow: Mahakama yaidai serikali ya Tanzania ambayo inasema haidaiwi

Mahakama ya migogoro ya kimataifa, ICSID imeiamuru serikali ya Tanzania kuilipa benki ya Standard Chartered (Hong Kong) dola milioni 185.4 kwa kwenda kinyume na mkataba.
Benki hiyo ilipeleka malalamiko yake dhidi ya serikali ya Tanzania katika kituo cha kusuluhisha migogoro ya uwekezaji mnamo mwaka 2015.
Mara baada ya amri hiyo ya mahakama kutolewa , msemaji wa serikali ya Tanzania, Dkt.Hassan Abbasi amesema kupitia ukurasa wake wa twitter kuwa mdaiwa wa kesi hiyo si Serikali wala Tanesco, ni deni la Benki dhidi ya shirika la usambazaji umeme Tanzania yaani IPTL ambao walilirithi miaka mingi kutoka kwa wakopeshaji wa Malaysia.
Msemaji huyo amewataka watanzania kutokuwa na hofu kuhusu maamuzi hayo kwa sababu serikali ya Tanzania haidaiwi na benki hiyo na wala haikuchukua fedha kutoka katika benki hiyo.
"Serikali haidawi au haijawahi kukopa Standard Charterd ya Hong Kong, ila kama Baraza la usuluhishi lilivyoamua, tutahakikisha tunasimamia utawala wa sheria kwa kuona IPTL wanalipa deni lao", Msemaji ameandika kwenye kurasa yake ya Twitter.
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe, 1
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe, 2
Dkt.Abbasi amefafanua kuwa kisheria serikali na kampuni ya umeme ya Tanesco ziliunganishwa tu kama kanuni za kisheria zinavyomruhusu mdai kuwaunganisha wahusika wengine kwenye kesi ili kuhakikisha kupata uhakika kuwa analipwa madai yake.
Hukumu hiyo imekuja wakati ambao mmiliki wa kampuni hiyo ya IPTL, akiwa gerezani.
Ingawa Oktoba 10,2019 , mmiliki wa kampuni ya Shirika la Kuzalisha na Kusambaza Umeme Tanzania, IPTL, Habinder Singh Seth ambaye anakabiliwa na mashtaka ya uhujumu uchumi aliandika barua kwa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) kukiri makosa na kuomba msamaha.
Miongoni mwa mashtaka yake ni kula njama, kujihusisha mtandao wa uhalifu , kughushi na kutoa nyaraka za kughushi, kujipatia fedha kwa njia za udanganyifu, kutakatisha fedha na kuisababisha serikali ya Tanzania hasara ya Dola milioni 22 na Shilingi za Tanzania bilioni 309.


Miongoni mwa mashtaka hayo ni kudaiwa, kati ya oktoba 18 ,2011 na Machi 19 , 2014 jijini Dar es Salaam ,Rugemarila na Sethi walikula njama katika nchi za Afrika Kusini, Kenya na India ya kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.
Washtakiwa wote, wanadaiwa kuwa kati ya Novemba 28/29, 2011 na Januari 23,2014 makao makuu Benki ya Stanbic kinondoni na Benki ya Mkombozi tawi la St .Joseph kwa ulaghai washtakiwa hao walijipatia kutoka Benki Kuu ya Tanzania (BOT), walijipatia USD 22,198,544.60 na Tsh 309, 461,300,158.27.
Sakata la Escrow liliitikisa serikali ya awamu ya nne ya Tanzania chini ya Raisi Jakaya Kikwete mwishoni mwa mwaka 2014 na mwanzoni mwa mwaka 2015 baada ya kamati maalumu ya Bunge kuchunguza tuhuma za rushwa.
Ripoti ya bunge ilipelekea maafisa kadhaa waandamizi wa serikali ikiwemo mawaziri na mwanasheria mkuu kupoteza nafasi zao.












