Mauaji ya Jamal Khashoggi: Kanda za siri za mauaji hayo zafichuliwa.

Jamal Khashoggi na ubalozi wa Saudi mjini istanbul

Chanzo cha picha, Getty Images

Onyo: Picha za kuogofya

Presentational white space

Nilitembea katika barabara iliojaa miti katika eneo tulivu mjini Istanbul na kukaribia nyumba moja iliopakwa rangi ya maziwa ikiwa na kamera za CCTV.

Mwaka mmoja uliopita mwandishi wa Saudia ambaye yuko mafichoni alitembea katika eneo hilo hilo.

Jama Khashoggi alionekana katika kamera za CCTV. Ilikuwa picha yake ya mwisho. Aliingia katika ubalozi wa Saudia na aliuawa na kundi moja la wauaji.

Presentational white space
Jamal Khashoggi anawasili katika ubalozi wa Saudia Istanbul

Chanzo cha picha, Reuters

Presentational white space

Lakini ubalozi huo ulikuwa na kamera zilizojifichwa za CCTV ambazo zilikuwa zimewekwa na majasusi wa Uturuki.

Kanda hizo zilizorekodiwa zimesikika na watu wachache sana, wawili kati ya watu hao sasa wamezungumza na kipindi cha BBC cha Panorama.

Jasusi wa Uingereza Baroness Hellena Kennedy alisikia wakati Jamal Khashoggi alipokuwa akifariki.

''Tisho la kusikiliza sauti ya mtu, hofu katika sauti ya mtu na kwamba unamsikiza mtu aliye hai . Inakufanya uogope mwilini''.

Presentational white space
Baroness Helena Kennedy QC
Maelezo ya picha, Baroness Helena Kennedy QC
Presentational white space

Kennedy aliandika maelezo ya mazungumzo aliosikia kati ya wanachama wa kundi hilo la wauaji wa Saudia.

''Unaweza kuwasikia wakicheka. Ni biashara ya kuogofya. wanasubiri hapo wakijua kwamba huyu mtu ataingia na kwamba atauwawa na kukatwa katwa''.

Kennedy alialikwa kujiunga na kikosi kinachoongozwa na Agnes Callamard , mjumbe maalum wa Umoja wa mataifa kuhusu mauaji ya kiholela.

Callamard , mwanaharakati maalum wa haki za kibinadamu aliniambia kuhusu jukumu la kutumia uwezo wake kuchunguza mauaji hayo , wakati Umoja wa Mataifa ilipochelewa kuanzsisha uchunguzi wa kimataifa.

Presentational white space
Agnès Callamard, Mjumbe maalum wa UN kuhusu mauaji ya kiholela
Maelezo ya picha, Agnès Callamard, Mjumbe maalum wa UN kuhusu mauaji ya kiholela
Presentational white space

Ilimchukua takriban wiki kadhaa kuwabembeleza majasusi wa Uturuki kumruhusu yeye na Kennedy , pamoja na mkalimani wao wa Kiarabu kusikiliza kanda hizo.

''Lengo la Uturuki kuniruhusu kuzisikiliza ilikuwa kuthibitisha mipango iliofanywa kabla ya mauaji hayo'', anasema.

Waliweza kusikiliza dakika 45 zilizotolewa katika kanda hiyo iliorekodiwa kwa siku mbili.

Maelezo ya video, British barrister Helena Kennedy and UN special rapporteur Agnes Callamard describe the Jamal Khashoggi secret tapes
Presentational white space
Presentational grey line
Presentational white space

Jamal Khashoggi alikuwa mjini Istanbul - mji ambao wapinzani wa serikali kadhaa mashariki ya kati wamekuwa wakijificha kwa wiki chache kabla ya kuuawa.

Baba huyo mwenye umri wa miaka 59 aliyetalakiana na mkewe alikuwa amechumbiana na mpenziwe mpya Hatice Cengiz, mtafiti msomi wa Uturuki.

Walikuwa na matumani ya kuanzisha maisha yao pamoja katika mji huo ulio na mchanganyiko wa raia, lakini ili kufunga ndoa tena Khashoggi alihitaji hati za talaka.

Mnamo tarehe 28 mwezi Septemba , yeye na Cengiz walielekea katika ofisi ya mji wa Uturuki lakini waliambiwa kwamba walihitaji kupata makaratasi hayo kutoka kwa ubalozi wa Saudi.

Hiyo ndio ilikuwa njia ya mwisho. Alilazimika kwenda ili kujipatia makaratasi yake kutoka kwa ubalozi ili kufunga ndoa rasmi kwasababu hakuweza kurudi kwao Saudia, Cengiz alianiambia tulipokutana katika mkahawa mmoja.

Presentational white space
Mchumba wa Jamal Khashoggi Hatice Cengiz
Maelezo ya picha, Mchumba wa Jamal Khashoggi Hatice Cengiz
Presentational white space

Khashoggi hajawahi kuwa mkimbizi , lakini alilitoroka taifa lake.

Nilikutana naye miaka 15 iliyopita kwenye ubalozi wa Saudi huko Mayfair mjini London. Wakati huo alikuwa moyoni mwa utawala wa Saudia - msaidizi aliyekuwa mpole sana wa ubalozi huo.

Tulijadiliana kuhusu shambulio la hivi karibuni la kigaidi lililotekelezwa na al-Qaeda.

Khashoggi alikuwa akimjua kiongozi wake Saudia, Osama bin Laden kwa miongo kadhaa.

Awali Khashoggi alikuwa akilihurumia sana lengo la kundi la al-Qaeda kupindua utawala wa kimabavu wa mataifa ya mashariki ya kati. Lakini baadaye alizungumzia kuhusu ukatili wa kundi hilo baada ya maoni yake kuwa huru na kupigania demokrasia.

Presentational white space
Jamal Khashoggi akiwa na Jane Corbin mwaka 2004
Maelezo ya picha, Jamal Khashoggi akiwa na Jane Corbin mwaka 2004
Presentational white space

Mwaka 2007, alirudi nyumbani kua muhariri wa gazeti linalounga mkono serikali kwa jina al-Watan.

Lakini alifutwa kazi miaka mitatu baadaye kwa kile alichoelezea kusababisha mijadala kupita mipaka ya serikali hadi katika jamii.

Lakini 2011, alishinikizwa na tukio la mapinduzi ya Arab Spring , Khashoggi alikuwa akizungumzia kile alichotaja kuwa serikali dhalimu ya Saudia .

Kufikia 2017, alikuwa amepigwa marufuku kutoandika na akelekea mafichoni nchini Marekani. Mkewe alilazimishwa kumpatia talaka.

Khashoggi alikuwa mchangiaji wa gazeti la The Washington Post ambalo aliliandikia machapisho 20 makali mwaka mmoja kabla ya kifo chake.

Wakati alipokuwa muhariri nchini Uingereza alikuwa akivuka mipaka, kulingana na David Ignatius mchangiaji mkuu wa maswala ya kigeni wa gazeti hilo na mwandishi mpekuzi.

Kile nilichoona kwa Jamal ni kwamba alikuwa akijiweka katika matatizo kila mara kwa kuzungumza kilichokuwa akilini mwake.

Presentational white space
Picha ya 2017 baada ya habari ilioandikwa na Jamal Khashoggi
Presentational white space

Ukosoaji mkubwa wa Khashoggi ulimlenga mwanamfalme mpya Mohammed bin Salman.

MBS, kama anavyojulikana , alipendwa na wengi katika mataifa ya magharibi. Alionekana kama mwanaharakati mkubwa wa mabadiliko akiwa na maono mapya ya taifa hilo.

Lakini nyumbani Saudia alikua akiwasaka na kuwakabili wapinzani na Khashoggi alikuwa akionekana katika machapisho yake.

Presentational white space
Mwanamfalme Mohammed bin Salman

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Mwanamfalme Mohammed bin Salman
Presentational white space

''Hii haikuwa picha ambayo mwanamfalme Muhammed alikuwa akitaka ionekane. Nadhani hilo lilimkasirisha sana mwanamfalme na alikuwa akiwataka wasaidizi wake kufanya kitu kuhusu swala hili la Jamal'', alisema Ignatius , ambaye mara kwa mara alikuwa akizuru nchini Saudia na kuandika kuhusu siasa.

Mjini Istanbul, Wasaudi walipata fursa ya kufanya kitu kuhusu Khashoggi.

Presentational grey line
Presentational white space

"Alisema kwamba hakuna kitu cha kuogopa , aliitamani nchi yake sana na kwamba mazingira kama hayo yalimfanya kuhisi vyema.

Khashoggi aliambiwa arudi siku nyengine. lakini muda tu alipokwenda , simu zilianza kupigwa mjini Riyadh nchini Saudia - zote zikirekodiwa na majasusi wa Uturuki.

Kile kilichovutia kuhusu simu hizo ni kwamba zilikuwa zikimtaja Khashoggi kama mtu aliyekuwa akitafutwa , kulingana na Callamard.

Simu ya kwanza inaaminika kumwendea msaidizi wa Saudia mwenye uwezo mkuu katika afisi ya mawasiliano kwa jina Saud al-Qatani.

Mtu mmoja katika afisi ya mawasiliano alikuwa ameuruhusu ubalozi huo. Sasa inaeleweka kwamba simu zote katika ofisi hiyo ya mawasiliano zilikwenda kwa Saud al-Qatani, anaendelea.

Ametajwa moja kwa moja katika kampeni tofauti dhidi ya watu binafsi. Wakati wa ziara yake ya kwenda katika ubalozi, Cengiz alilazimika kusalia nje.

Anakumbuka Khashoggi akirudi kutoka ndani ya jengo hilo akiwa na tabasamu. Alimawambia kwamba maafisa walishangazwa kumuona na kwamba walimpatia chai na kahawa.

Presentational white space
Saud al Qahtani

Chanzo cha picha, Twitter

Maelezo ya picha, Saud al Qahtani
Presentational white space

Al-Qahtani tayari alikuwa ametuhumiwa kuhusika katika kuwazuia watu na kuwatesa wapinzani nchini Saudia kama vile mwanaharakati wa kike aliyejaribu kuendesha gari kabla ya marufuku hiyo kuondolewa pamoja na maafisa wengine wakuu waliokataa kuitii serikali ya nchi hiyo.

Katika maandishi yake , Khashoggi alimshutumu al-Qahtani kwa kuongoza kundi la wauaji wa mwanamfalme huyo.

Qahtani alianza kufanya hudumu zisizo za kawaida - zenye siri , kulingana na Ignatius ambaye amewahi kumchunguza mshauri huyo wa Ufalme wa Saudia.

Hiyo ndio ilikuwa kazi yake na aliisimamia bila huruma. Kuna rekodi za takriban simu nne tarehe 28 Septemba kati yake na ubalozi na Riyadh.

Simu hizo ni pamoja na mazungumzo kati ya balozi mkuu na mkuu wa usalama katika wizara maswala ya kigeni, ambaye alimwambia siri kubwa ya ubalozi huo - jukumu la kitaifa.

''Sina wasiwasi akilini mwangu ,ulikuwa mpango mkubwa ulioandiliwa kutoka juu'', alisema Kennedy. ''haikuwa operesheni ndogo''.

Presentational grey line
Presentational white space

Mchana wa tarehe mosi Oktoba . Maafisa watatu wa Ujasusi walisafiri hadi mjini Istanbul. Inajuliakana kwamba wawili walikuwa wakifanya kazi katika afisi ya mwanamfalme wa Saudia.

Callamard anamini kwamba walikuwa na mradi waliotarajiwa kutekeleza. Walichunguza jumba la ubalozi huo wakajua ni kipi kinaweza kufanyika na kipi hakiwezekani.

Nikiwa mjini Istanbul nilikutana na afisa mmoja aliyekuwa jasusi wa Uturuki aliyefanya kazi kwa takriban miaka 27.

Metin Ersoz ni mtaalamu kuhusu Saudia na misheni zake maalumu. Anasema kwamba hudumu za ujasusi zilianza kuwa na nguvu baada ya Mohammed bin Salman kuwa mwanamfalme.

Presentational white space
Metin Ersöz
Maelezo ya picha, Metin Ersöz
Presentational white space

"Walianza operesheni za kuteka watu na kuwakabili wapinzani'', anasema. Khashoggi alichelewa kutambua tisho hilo na kuchukua tahadhari na mwisho alilipa.

Mapema tarehe 2 Oktoba , ndege ya kibinafsi ilitua katika uwanja wa ndege wa Istanbul. Ndani ya ndege hiyo walikuwa raia tisa wa Saudia , akiwemo mwanapatholojia kwa jina Dkt Salah al-Tubaigy.

Presentational white space
Dkt Salah al-Tubaigy
Maelezo ya picha, Dkt Salah al-Tubaigy
Presentational white space

''Baada ya kugundua ni akina nani na wanakotoka, Callamard anaamini hilo ndio kundi lililotekeleza mauaji'', anasema.

Wawili kati yao waikuwa na pasipoti za ubalozi. Erosz anasema kwamba ujumbe kama huo -wenye operesheni maalum ungehitaji ruhusa kutoka kwa mfalme wa Saudia ama mwanamfalme.

Raia hao wa Saudia waliigia katika hoteli ya Movenpick, ambayo haipo mbali na ubalozi huo.

Presentational white space
Waliingia katika hoteli ya Mövenpick

Chanzo cha picha, Reuters

Presentational white space

Kabla ya mwendo wa saa nne kanda za video za CCTV zinamuonyesha afisa mmoja wa kundi hilo la mauaji akiingia katika ubalozi huo wa Saudia.

Ukisikiliza kanda hizo , Kennedy anaamini kwamba Maher Abdulaziz Mutreb ndio mtu aliyesimamia operesheni hiyo.

Mutreb alionekana mara kwa mara akisafiri na mwanamfalme , akiwa nyuma nyuma pamoja naye kama afisa wake wa usalama.

''Katika simu hizo zilizopigwa kati ya balozi na bwana Mutreb , tulipata ujumbe kwamba Khashoggi atakuwa akizuru ubalozi huo siku ya Jumanne'', kulingana na Kennedy.

Presentational white space
Maher Abdel Aziz Mutreb

Chanzo cha picha, Getty Images

Presentational white space

Jioni ya tarehe 2 mwezi Oktoba , Khashoggi alipokea simu kuja katika ubalozi ili kupata makaratasi yake aliyohitaji.

Huku yeye na Cengiz wakielekea katika ubalozi huo, kulikuwa na mawasiliano ya kushangaza ya simu yaliokuwa yakiendelea kati ya bwana Mutreb na mwanapatholojia huyo kwa jina al-Tubaigy .

''Anazungumzia kuhusu jinsi atakavyochunguza mwili wa marehemu . Unaweza kuwasiki wakicheka'', kennedu anasema.

Anasema kwamba yeye husikiliza muziki anapokata wafu ''na mara nyengine mimi huvuta sigara na kunywa chai'' .

''Baadaye kanda hizo zinafichua kile daktari huyo anachofaa kufanya'' , kulingana na Kennedy.

''Ni mara ya kwanza maishani mwangu , nitalazimika kukata vipande vipande chini',anakumbuka akisema. Hata iwapo wewe ni mchinjaji unamtundika mnyama mahali kabla ya kumchinja''.

Afisi ya juu katika ubalozi huo ilikuwa tayari imetayarishwa . Sakafu yake ilifunikwa kwa kutumia plastiki . Maafisa wote wa ubalozi wa Uturuki walipewa siku ya kupumzika.

''Walikuwa wakizungumza je ni lini Khashoggi atawasili na walikuwa wakisema , Je mnyama huyo wa sadaka amwewasili? hivyo ndivyo walivyokuwa wakumuita'', alisema Kennedy.

Alikuwa ananisomea kutoka katika kitabu chake , Tisho katika sauti.

Presentational white space
Jamal Khashoggi

Chanzo cha picha, Reuters

Presentational white space

Mwendo wa saa saba , kanda hizo za , CCTV zilimuonyesha Khashoggi akiingia katika jengo hilo. Nakumbuka tulielekea huko tukiwa tumeshikana mikono na tupofika katika jumba la ubalozi huo Jamal alinipatia simu zake na kusema: Tuonane baadaye mpenzi, nisubiri hapa, alisema Cengiz.

Khashoggi alijua kwamba simu zake zitachukuliwa katika eneo la mlango wa ubalozi huo na hakutaka Wasaudi kuwa na simu yake ili kusoma habari yake ya Faragha.

Kanda hizo zinafichua kwamba anapokelewa ndani ya ubalozi na kuambiwa kuna agizo la polisi wa kimataifa ambao wanataka kumkamata na kwamba ni sharti arudi Saudia.

Anasikika akikataa kumtumia ujumbe mwanawe ili kuhakikisha kuwa familia yake ipo salama.

Kunyamazishwa kwa Jamal baadaye kunaanza.

Presentational white space
Nembo ya Panorama
Presentational white space

"Kuna wakati ambapo ungeweza kumsikia Khashoggi mwenye hofu na baadaye kugundua kwamba kitu hatari kilikuwa karibu kifanyike'', alisema Kennedy.

Anaendelea: Kuna kitu kinachotisha hususan sauti yake inapobadilika. Unyama huo utausikia vizuri unaposikiliza kanda hizo.

Callamard hajui iwapo Khashoggi alifahamu njama hizo za Saudi. Sijui kama alifikiria kwamba anaweza kuuawa, lakini nadhani alikuwa akifikiri kwamba huenda wakamteka

Anauliza je munataka kunidunga sindano? ambapo anajibiwa ndio. Kennedy anasema kwamba alimsikia Khashoggi akiuliza mara mbili iwapo anatekwa na baadaye anaendelea kusema Vipi jambo kama hili linaweza kutokea katika ubalozi?.

''Sauti utakazosikia baada ya hilo ni kana kwamba ananyimwa pumzi. Pengine kwa kutumia karatasi ya Plastiki katika kichwa chake'', anasema Callamard.

''Mdomo wake pia ulifungwa - kwa kutumia nguvu pengine kwa kutumia mkono ama kitu chengine. Kennedy anaamini kwamba baadaye daktari huyo wa kupasua mfu anachukua zamu kufuatia agizo la kiongozi wa operesheni hiyo.

Unasikia sauti kwamba wacha amkate, na anasikika kama bwana Mutreb. Baadaye mtu anapiga kelele, Kwisha na mtu mwengine anapiga kelele ondoa ondoa. Weka hii katika kichwa chake funga. Nilifikiri kwamba walimkata kichwa chake.

Presentational grey line
Presentational white space

Kwa Cengiz, ilikuwa nusu saa pekee tangu Khashoggi alipomuacha nje wa ubalozi.

''Wakati huo, nilikuwa nikiota kuhusu hatma yangu - jinsi ndoa yetu itakavyokuwa . Tulikuwa tukipanga sherehe ndogo'', alisema.

Mwendo wa saa tisa CCTV zinaonyesha gari la ubalozi likiondoka na kuwasili katika makao ya balozi ambapo ni barabara mbili kutoka hapo.

Presentational white space
Ramani ya eneo karibu na ubalozi wa saudia mjini Istanbul
Presentational white space

Watu watatu wanaonekana wakiingia na sare za ofisini wakibeba mifuko ya plastiki. Callamard anaamini walikuwa wakibeba vipande vya mwili wake. Baadaye gari linaondoka.

Mwili wa Khashoggi haujapatikana. Na je maelezo ya kutisha wakati wa mauaji hayo - msumeno wa kukata mifupa uliotumiwa kumkatakata vipande vidogo vidogo?.

Kennedy anasema kwamba hakusikia sauti za kukata na msumeno angefananisha na kifaa cha kukata kinachotumika wakati wa upasuaji.

Lakini anasema kwamba kulikuwa na sauti kama ile ya nyuki. Majasusi wa Uturuki wanaamini kwamba hiyo ndio iliokuwa sauti ya msumeno . Mwendo wa saa tisa na dakika 53, kanda za CCTV ziliwaonyesha maafisa wawili wa mauaji hayo wakiondoka katika ubalozi huo.

''Nilifuata nyayo zao katika barabara kupitia kamera zilizokuwepo ambazo zilionyesha njia iliokuwepo kati ya ubalozi na katikati ya mji wa zamani wa Istanbul.

''Mtu mmoja anaonekana amevalia mavazi ya Khashoggi , lakini akiwa na viatu tofauti. Mwengine ambaye sura yake imejificha anaonekana akibeba mfuko wa plastiki''.

Presentational white space
Jamal Khashoggi na mtu aliyevalia kama yeye isipokuwa viatu

Chanzo cha picha, Reuters

Presentational white space

Wanaelekea katika msikiti maarufu mjini Istanbul kwa jina Blue Mosque. Wanapotoka mtu aliyevalia nguo za Khashoggi amebadilisha nguo hizo. Wanapanda teksi na kurudi katika hoteli yao, wakitupa mifuko ya plastiki iliodaiwa kubeba nguo za Khashoggi katika jaa moja karibu kabla ya kuelekea katika barabara ya chini na kurudi katika hoteli ya Movenpick.

''Kuna kiwango cha juu cha mipango ya mauaji hayo ili kuonyesha kwamba hakuna kitu kibaya kilichotokea dhidi ya Khashoggi'' , alisema Callamard.

Wakati wote huu Cengiz alikuwa akisubiri nje ya ubalosi huo.

''Nilisubiri na kusubiri hapo hadi saa tisa na nusu. halafu nilipogundua kwamba ubalozi umefungwa , nilianza kukimbia ili niingie. Nilijiuliza kwa nini Jamal hakutoka.

Bawabu mmoja aliniambia kwamba haelewi ninachozungumzia. Mwendo wa saa kumi na dakika 41 , Cengiz alikuwa na wasiwasi na kumpigia simu rafiki wa zamani wa Khashoggi.

Alimpatia nambari yake iwapo pengine alikuwa katika tatizo lolote. Dkt Yasin Aktay ni mwanachama wa chama tawala cha Uturuki akiwa na mawasiliano na watu maarufu.

''Nilipokea simu kutoka kwa mtu mwenye nambari nisiojua, sauti yenye wasiwasi mkubwa kutoka kwa mwanamke ambaye sikuwa nikimjua'', alisema. '

''Mchumba wangu Jamal alienda katika ubalozi wa Saudia na hakutoka tena''.

Presentational white space
Dkt Yasin Aktay
Maelezo ya picha, Dkt Yasin Aktay
Presentational white space

Yasin alipiga simu kwa afisi ya ujasusi ya uturuki na kuielezea afisi ya rais Tayyip Erdogan. Kufikia mwendo wa saa kumi na mbili unusu jioni , wanachama wa kundi hilo la mauaji walikuwa ndani ya ndege ya kibinafsi iliokuwa ikielekea Riyadh , chini ya saa 24 baada ya kuwasili.

Siku iliofuata, Serikali za Saudi na Uturuki zilitoa taarifa tofauti zinazokinzana kuhusu kile kilichotokea katika ubalozi huo.

Saudia ilisisitiza kuwa Khashoggi alikuwa ameondoka ubalozi huo . Uturuki ilisema kwamba bado yungali ndani.

Maafisa wa ujasusi wa Uturuki walikuwa tayari wakishutumu kuhusu rekodi hizo ikiwemo simu zilizopigwa siku nne kabla ya Khashoggi kutoweka.

Presentational white space
Ubalozi wa Saudia mjini Istanbul

Chanzo cha picha, Getty Images

Presentational white space

Je walijua kwamba maisha yake yalikuwa hatarini , na iwapo ni kweli kwa nini hawakuomuonya?

Sidhani walijua, hakuna ushahidi kwamba walikuwa wakisikiliza moja kwa moja kile ambacho kilikuwa kikitokea.

Kulingana na Callamard. Ujasusi kama huu hufanyika kila siku , na ni wakati ambapo kuna tukio kubwa ambapo kanda kama hizo huchunguzwa .

Ni kwa sababu bwana Khashoggi aliuawa na kutoweka ndio maana walichunguza kanda hizo. Ersoz ananiambia kwamba mwenzake wa Ujasusi alisikiliza kanda hizo moja baada ya nyengine na kusikiliza kati ya saa 4,000 na 5000 ili kutafuta siku muhimu na dakika 45 zilizowasilishwa kwa Callamard na Kennedy.

Siku nne baada ya kifo cha Khashoggi , kikosi chengine cha Saudia kiliwasili kikidai kiliwasili kuchunguza kilichotokea. Callamard anaamini kilikuwa kikosi kilichowasili ili kufagia na kuficha yaliotokea.

Ubalozi huo ni eneo la Saudia kulingana na sheria ya kimataifa na kwa wiki mbili Saudia haitaruhusu wachunguzi wa Uturuki kuingia.

''Kufikia wakati ambapo walikuwa wakikusanya ushahidi, hakukuwa na kitu , hata chembechembe za DNA za bwana Khashoggi hazikuwepo licha ya yeye kuwepo ndani yake''.alisema Callamard.

Kitu pekee ni kwamba eneo hilo lilisafishwa kabisa.

Presentational white space
Maafisa wa polisi wa Uturuki katika ubalozi wa Saudia

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Maafisa wa polisi wa Uturuki katika ubalozi wa Saudia
Presentational white space

Jioni hiyo , mamlaka ya Uturuki iliambia vyombo vya habari kwamba Khashoggi aliuawa katika ubalozi wa Saudia.

''Jamal hakuhitaji kufanyiwa hivyo, alihitaji mema zaidi'', alisema Cengiz. Jinsi walivyomuua kuliua matumaini yangu yote''. mauaji yaliofanyika Istanbul.

Ndani ya ubalozi kukiwa na kinga ya kidiplomasia , kunauweka utawala wa Uturuki katika hali ngumu.

Kwa wiki kadhaa sasa licha ya shinikizo kutoka kwa mamlaka ya Uturukji , Saudia ilikataa kukiri mauaji hayo , ikisema kwamba kulikuwa na vita ndani ya ubalozi huo na kuamua ilikuwa operesheni ngumu.

Presentational white space
Maandamano nje ya Ubalozi wa saudia nchini Uturuki baada ya kuroweka kwa Jamal Khashoggi.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Maandamano nje ya Ubalozi wa saudia nchini Uturuki baada ya kuroweka kwa Jamal Khashoggi.
Presentational white space

Mchakato wa Uturuki ilikuwa kufichua kile ilichojua kwa vyombo vya habari vya kimataifa.

Baadaye waliwaalika wawakilishi wa CIA na mashirika mengine machache ya ujasusi , ikiwemo M16 , kusikiliza kanda hizo , na kuthibitisha kwamba Khashoggi aliuawa na raia wa Saudia.

Baadaye shirika la kijasusi la CIA lilitamatisha kwa kusema kwamba kulikuwa na uwezekano kwamba huenda Mohammad bin Salama aliagiza mauaji hayo.

Waliwaelezea wabunge ambao walibaini kilichotokea.

Mwezi Januari , serikjali ya Saudia iliwashtaki watu 11 mjini Royadh , ikiwemo Mutreb na Dkt al-Tubaigy lakini sio aliyepanga mauaji hayo Saud al-Qahtani.

''Hajawahi kuhojiwa wala kuchunguzwa kutoa ushahidi. Nimeambiwa kwamba ametengwa na kila mtu ikiwemo familia yake lakini bado anawasiliana na mwanamfalme''.

Presentational grey line
Presentational white space

''Ripoti ya Callamard kwa baraza la haki za kibinadamu katika umoja wa kimataifa ilifikia hitimisho lake. Hakuna ishara chini ya sheria ya kimataifa kwamba uhalifu huu unaweza kuchukuliwa kivyovyote vile isipokuwa mauaji ya serikali'', alisema.

Kennedy anasema kuwa ufichuzi wa kanda za mauaji ya Khashoggi unapaswa kuchukulkiwa hatua.

''Kitu kibaya kinachoogofya kilifanyika katika ubalozi huo. Jamii ya kimataifa ina jukumu la kusisitiza uchunguzi wa kiwango cha juu kufanyika'', alisema.

Uturuki imetaka kurudishwa kwa wale waliohusika ili kushtakiwa mjini Istanbul . lakini Saudia imekataa.

Serikali ya Saudia ilikataa kufanya mahojiano na kipindi cha BBC cha Panorama , lakini ilisema ilishutumu mauaji hayo na kwamba ilikuwa tayari kuwawajibisha waliohusika.

Ilisema kwamba mwanamfalme wa Saudia hahusiki kamwe na uhalfu ilioutaja kuwa mbaya zaidi

Presentational white space
Mwanamfalme wa Saudia Mohammed bin Salman

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Mwanamfalme wa Saudia Mohammed bin Salman
Presentational white space

Mwaka mmoja baadaye , tulipokuwa tukiendoka katika mgahawa , naweza kuona uchungu uliokuwa ukimkumba mwanamke aliyewachwa nyuma wakati ambapo maisha ya mchumba wake yalikatizwa mara moja na vibaya.

Katika maneno yake ya mwisho, Hatice Cengiz alionya kuhusu umuhimu wa mauaji ya Jamal Khashoggi.

''Sio janga tu kwangu - lakini kwa umma wote , watu wote wanaofikiria kama Jamal na waliokuwa na msimamo kama yeye''.

Presentational white space
Kumkumbuka Jamal Khashoggi

Chanzo cha picha, Getty Images

Presentational white space

All images subject to copyright