Barua kutoka Afrika: Kizungumkuti cha namna ya kutuliza pepo la Robert Mugabe kiongozi wa zamani Zimbabwe

Chanzo cha picha, Reuters
Katika barua kutoka kwa waandishi wa Afrika, Brian Hungwe anaandika kwamba raia wengi wa Zimbabwea wameshutushwa kusikia kuwa mjane wa rais wa zamani wa Zimbabwe Robert Mugabe, alikua akikaa na mwili wa marehemu nyumbani kabla ya mazishi yake Jumamosi ya wiki iliyopita.
Unakula vipi, unalala na kunywa vipi ukiwa umekaa na maiti nyumbani mwako kwa wiki kadhaa?
Swali hilo limekuwa kitendawili kwa raia wengi nchini tangu kufichuka kwamba mwili wa kiongozi huyo wa zamani - aliyefariki zaidi ya wiki tatu zilizopita akiwa na umri wa miaka 95 - unahifadhiwa katika nyumba yake ya kifahari Blue Roof mansion katika mji mkuu Harare.
Wakati kukishuhudiwa mvutano baina ya serikali na familia yake kuhusu iwapo azikwe katika makaburi ya mashujaa au kijijini alikotoka Zvimba, kaskazini magharibi mwa Harare.

Chanzo cha picha, AFP
wakati kukiwa hakuna taarifa rasmi kuhusu ulikowekwa mwili wa marehemu Mugabe, wengine walieneza uvumi kwamba Mugabe - kama mrithi wa chifu wa Zvimba, kijijini alikotoka, alikuwa tayari keshazikwa katika pango kwa mujibu wa tambiko za ukoo wake wa Gushungo, kufuatia mazishi yake ya kitaifa Harare na maombolezi na hafl aya kuutazama mwili wake huko Zvimba.
Lakini picha za jeneza lililokuwa nyumbani kwake zilichipuka Jumatatu (Septemba 23) wakati mwanasiasa wa upinzani Julius Malema alipofika kutoa heshima zake za mwisho kwa Grace Mugabe.
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe
"Mugabe alipumzika kwa amani...anapumzika," Bi Mugabe alisema wakati wa ziara ya Malema.
Hili lilifuatwa kwa kuutazama mwili wa marehemu alafu chakula cha mchana kilichoandaliwa katika chumba cha pili kutoka alikolazwa maiti.
Baadhi ya raia sasa wanamithilisha na tambiko na tamaduni katika eneo la Tana Toraja nchini Indonesia, ambako huchukua muda mrefu kumzika maiti.
Maiti huwekwa nyumbani. waliofiwa huuosha na kuusafisha. Humletea maiti chakula mara mbili kwa siku pamoja na kahawa na hata siagara za kuvuta.
Ni njia ya waliofiwa kukabiliana na majonzi na huzuni wa kuondokewa. watu huamini maiti husikia, na iwapo hawatomshughulikia maiti, pepo abaye yupo miongoni mwao atawasumbua.
Hofu ya maiti
Tamaduni za watu wa kabila la Shonaambapo ukoo wa Gushungo unaangukia- unahitaji tambiko kadhaa kutekeleza wkati kunakuwa na kifo.
Tambiko hizo zinashinikiza utambulisho wa pamoja na kuzisaidia familia na jamii kukabiliana na kuodnokewa na mpendwa wao.

Chanzo cha picha, AFP
Wataalamu wa masuala haya nchini Zimbabwea wanasema tambiko za kabila la Shona mara nyingi hutokana na hofu ya maiti.
Pepo wa marehemu huaminika kuwana nguvu, na mwenye hisia kama za binaadamu. aanaweza kuwaandamana walio hai iwapo maiti hatoshughulikiwa ipasavyo.
Baada ya kuitawala Zimbabwe tangu uhuru mnamo 1980, Mugabe alikuwa na uzito - alikuwa ni taasisi ya kisiasa.
Karibu na mama yake
Baadhi ya raia Zimbabwe wanasema huenda pepo wake Mugabe alikuwa hayupo tayari kwa mazishi na pengine ndio sababu mwili wake uliwekwa nyumbani kwake kwa muda mrefu.
Familia yake ilionekana kutokuwana tatizo na hilo, baadhi yao wakisema mojawapo ya mambi yake Mugabe ni kwamba mkewe asiondoke kamwe karibu na mwili wake mpaka atakapozikwa.
Haijulikani wazi kwanini ametoa ombi kama hilo. Pengine familia inahofia mwili wake utaharibiwa kwa sababu za kitambiko.
Kwa mujibu wa familia, Mugabe alikuwa na ombi jingine - azikwe kijijini alikotoka, karibu na marehemu mamake, Bona.
Kwa kawaida ombi la marehemu huheshimiwa, lakini alipokuwa hai, Mugabe aliwakaidi baadhi ya wapiganiaji uhuru wenzake waliotaka wasizikwe katika makaburi ya mashujaa mjini Harare.

Zaidi kuhusu Robert Mugabe:

Mhadhiri wa Historia profesa Gerry Mazarire anasema kumweka Mugabe juu ya mashujaa wengine waliopigania uhuru wa nchi itakuwa ni kueneza uongo - kwamba yeye ndiye aliyeidhinisha nchi.
Pia inadunisha mchango wa wengine - na huenda ingeashira kuwa serikali inashikiliwa mateka kwa kiburi cha mtu aliyefariki, anasema.

Chanzo cha picha, AFP
Raia wengi wa Zimbabweans chawakuweza kuelewa uamuzi wa kutozikwa kwa Mugabe katika makaburi hayo ya mashujaa - unapokiuka maombi ya marehemu , unakasirisha pepo wake na ni vigumu kulituliza.
Huenda familia ilihisi shinikizo hilo na hatimaye Robert Mugabe amezikwa kijijini alikotoka huko Zvimba.

















