Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Iran yaonya kuwaangamiza wachokozi wake baada ya Marekani kutangaza kupeleka majeshi Saudia
Marekani imetangaza mipango ya kutuma vikosi vya kijeshi nchini Saudia kufuatia mashambulizi dhidi ya hifadhi za mafuta za taifa hilo.Marekani kutuma wanajeshi Saudia
Waziri wa ulinzi Mark Esper aliambia wanahabari kwamba wanajeshi hao wataelekea katika taifa hilo ili kuimarisha ulinzi . Hatahaivyo idadi yao bado haijajulikana.
Waasi wa Houthi nchini Yemen wanaoungwa mkono na Iran wamesema kwamba walihusika na mashambulizi ya visima viwili vya mafuta wiki iliopita. Lakini Saudia na Marekani zimelaumu Iran kwa mashambulizi hayo.
Siku ya Ijumaa , rais Trump alitangaza vikwazo vipya dhidi ya Iran huku akisema kwamba alipendelea kuzuia mgogoro wa kijeshi.
Vikwazo hivyo vipya ambavyo rais Trump alivitaja kuwa vya kiwango cha juu vitalenga benki ya Iran na mali yake iliopo ugenini.
''Nadhani kujizuia ni muhimu'' , aliambia afisi ya White House.
Lakini siku ya Jumamosi. Kamanda wa jeshi la Iran Revolutionary Guard IRGC alisema kwamba taifa hilo litamuangamiza mchokozi yeyote.
''Tahadharini '', alisema Meja Jenerali Hossein Salami katika runinga ya taifa hilo. ''Tuko tayari kumuadhibu mtu na tutaendelea hadi kuwaangamiza wachokozi''.
Je Pentagon imesemaje?
Saudi Arabia imesema kwamba UAE iliomba msaada, kulingana na bwana Esper.
Amesema kwamba vikosi vya Marekani vitaangazia kupiga jeki wanajeshi wake wa angani mbali na kujilinda dhidi ya silaha za angani na kwamba itapeleka silaha kwa nchi zote mbili.
Mwenyekiti wa wanajeshi jenerali Joseph Dunford aliunga mkono upelekeji wa wanajeshi hao akidai kwamba hatasema idadi yao. hatahivyo hakutoa maelezo zaidi kuhusu aina ya vikosi hivyo vitakavyotumwa.
Kulingana na gazeti la New York Times , wakati maripota walipomuuliza bwana Esper iwapo mashambulizi ya kijeshi dhidi ya Iran yalikuwa yanapatiwa kipau mbele alijibu: Kwa sasa hatujafikia uamuzi huo.
Je ni nini kilichotokea Saudia
Mashambulio yaligonga visima vya mafuta vya Abqaiq na kile cha Khurais nchini Saudia wiki moja iliopita na kuathiri usambazaji wa mafuta duniani.
Siku ya Jumatano , wizara ya ulinzi ya ufalme huo ilionyesha mabaki ya ndege zisizo na rubani na silaha ikithibitisha kwamba Iran ndio iliohusika.
''Taifa hilo lilikuwa linafanya uchunguzi kujua ni wapi mashambulio hayo yalitekelezwa'', alisema msemaji.
Marekani pia imesema kwamba Iran ndio iliohusika .
Maafisa waandamizi wameambia vyombo vya habari vya Marekani kwamba wana ushahidi kwamba mshambulizi hayo yalitekelezwa kusini mwa Iran.
Iran imekana kuhusika katika mashambulio hayo , huku rais Hassan Rouhani akiyataja kuwa kisasi cha raia wa Yemen.
Marekani haiamini kwamba waathiriwa wa vita vya Yemen vya miaka 4 na nusu hawawezi kutekeleza mashambulio kama hayo.
Siku ya Jumatano waziri wa maswala ya kigeni nchini Marekani aliyataja mashambulio hayo kama kitendo cha vita.
Bwana Zarif alionya katika mtandao wake wa Twitter kwamba ''Iran haipendi vita lakini hatutasita kujilinda''.
Wakati huohuo kampuni ya mafuta ya Saudia , Aramco imesema kwamba inatarajia kiwango cha mafuta kurudi kufikia kiwango cha kabla ya shambulio kufikia mwezi Septemba.
Marekani kuzipa mwanya wa ulinzi wa Saudia
Na mchanganuzi Frank Gardner.
Mshamabulizi kadhaa ya ndege za rubani dhidi ya hifadhi za mafuta za Saudia yameonyesha uwezo wa Saudia kiulinzi.
Kwa sasa Marekani ambayo ndio mshirika wake wa kimkakati imejitolea kuziba mwanya. Meli ya kijeshi ya Marekani The Destroyer imeegeshwa kaskazini mwa Ghuba ili kuzuia makombora yanayotoka upande huo.
The Pentagon pia imetangaza upelekaji wa vikosi zaidi Saudia ili kusaidia kuimarisha ulinzi wake dhidi ya makombora.
Vifaa zaidi ya kujilinda vinatumwa kote Saudia na UAE kufuatia hali ya wasiwasi na jirani yao Iran.
Lakini kuwepo kwa kambi za vikosi vya Marekani Saudia kumezua utata katka siku za nyuma.
Licha ya kwamba vilialikwa na mfalme wa Saudia, uwepo wao ulitumika na Osama bin Laden kuwavutia wapiganaji wa kijihadi kupinga kile alichokitaja kuwa uvamizi wa rasi ya Arabuni.
Ni nini chanzo cha yote hayo?
Waasi wa Houthi mara kwa mara wamerusha makombora na ndege zisizo na rubani katika maeneo yanayokaliwa na raia nchini Saudia.
Wanapigana dhidi ya vikosi vya muungano wa Saudia ambavyo vinamuunga mkono rais ambaye waasi hao walimtimua wakati mgogoro huo wa Yemen ulipochacha mnamo mwezi Machi 2025.
Iran ndio mpinzani wa Saudia na ndio mpinzani mkuuu wa Marekani ambayo iijiondoa katika makubaliano ya kinyuklia ya Iran baada ya Trump kuchukua mamlaka. Wasiwasi kati ya Marekani na Iran umezidi mwaka huu.
Marekani ilisema kwamba Iran ilihusika na mashambulio ya meli mbili za mafuta katika Ghuba mwezi juni na Julai , pamoja na meli nyengine nne mwezi Mei.
Tehran ilipinga madai hayo katika visa vyote viwili.