Rubani wa ndege ya jeshi aangukia kwenye nyaya za umeme baada ya kujirusha kutoka kwenye ndege yake aliyopata hitilafu angani

Belgian Air Force F-16 AM fighting jet, a military war aircraft on an aerobatic air show display during the 53rd Paris Air Show in Le Bourget Airport LBG in France.

Chanzo cha picha, Getty Images

Muda wa kusoma: Dakika 1

Ndege ya kijeshi iliyoanguka huko kaskazini magharibi mwa Ufaransa, ilisababisha rubani mmoja kuruka na kuangukia katika nyaya za umeme.

Rubani wote waliruka katika ndege hiyo katika eneo la Brittany .

Vyombo cha habari vya kifaransa vimeripoti kuwa tukio hilo lilitokea karibu na Pluvigner.

MAXPPP/PA IMAGES

Chanzo cha picha, MAXPPP/PA IMAGES

Rubani huyo aliyeangukia umeme, sasa anaendelea vizuri na kunusurika kupigwa shoti na umeme .

Rubani wote wawili wako salama na wanaendelea vizuri.

Nyaya za umeme ambazo mtu yule aliziangukia zilikuwa na nguvu za volts 250,000, vyombo vya habari nchini humo vimetaarifu.

Map of Brittany

Vyombo vya habari vya Ufaransa vimeonyesha picha ya namna parachuti ilivyokuwa inashuka karibu na nyaya za umeme.

Picha nyingine zimeonyesha moshi ukiwa unatokea karibu na eneo ndege hiyo ilipopata itilafu katika paa la nyumba moja.

Picha nyingine , inaonyesha ndege ikiwa inawaka moto.

Ndege hiyo ya jeshi inaripotiwa kuwa haikuwa imebeba silaha.

Presentational white space