Watu wawili wapoteza maisha kutokana na vurugu nchini Afrika Kusini

Mtu akitazama uharibifu uliofanyika

Chanzo cha picha, Reuters

Muda wa kusoma: Dakika 2

Watu wawili wamepoteza maisha kutokana na vurugu mpya zilizofanywa na mgenge ya watu nchini Afrika Kusini.

Vurugu hizo zilianza baada ya hotuba iliyotolewa mjini Johannesburg na mwanasiasa mkongwe, dhidi ya vitendo vya chuki dhidi ya wageni.

Mangosuthu Buthelezi alizomewa na kundi la watu siku ya Jumapili, ambapo vikosi vya usalama viliingilia kati.

Watu kumi, wakiwemo wageni wawili, waliuawa mjini humo juma lililopita, baada ya makundi ya watu kuvamia biashara zinazofanywa na raia wa kigeni.

Vurumai hizo zimesababisha mvutano wa kidiplomasia na nchi nyingine za kiafrika, hasa Nigeria.

Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa amekemea vitendo vya vurumai za siku ya Jumapili, akisema mamlaka hazitaruhusu '' vurugu hizo na vitendo vya uvunjaji sheria kuhatarisha usalama wa mamilioni ya raia wa Afrika Kusini na raia wa kigeni nchini mwetu ambao wana haki kwa mujibu wa sheria kuishi na kufanya biashara kwa amani''.

Siku ya Jumapili watu kadhaa wakiwa wamebeba marungu waliandamana mjini Johannesburg wakiimba '' wageni ni lazima warudi walikotoka'', kilieleza chombo cha habari cha Soweten.

Ruka X ujumbe, 1
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa X ujumbe, 1

Kundi hilo lilielekea kwenye bustani ya Jules mjini Johannesburg mahali ambapo Buthelezi, Kiongozi wa zamani wa upinzani wa chama cha Inkatha Freedom na waziri wa serikali ya umoja baada ya ubaguzi wa rangi alikuwa akitarajiwa kutoa hotuba kuhusu mashambulizi ya hivi karibuni.

Amesema amefika kama msuluhishi na kusema kuwa amekuwa akijisikia vibaya kutokana na machafuko ya hivi karibuni ambayo amesema yameharibu sifa ya Afrika Kusini barani Afrika.

Lakini alizomewa wakati wote na video ilichapishwa kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter ikionesha makundi ya watu wakitoka nje ya mkutano.

Ruka X ujumbe, 2
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa X ujumbe, 2

Kisha watu walianza kushambulia magari na majengo, na kuchoma moto, Mkuu wa idara ya polisi mjini Johannesburg, David Tembe alieleza chombo cha habari cha Eyewitness.

''Nafikiri ni uhalifu kabisa kwa sababu baadhi ya maduka yaliyochomwa si mali ya raia wa kigeni, yanamilikiwa na raia wa Afrika Kusini, '' alinukuliwa.

Juma lililopita, polisi wamesema kuwa wamewakamata watu zaidi ya 240 na fujo hizo zilipugua. Mamlaka ziliwakamata watu 16 baada ya fujo za siku ya Jumapili, taarifa ya raisi wa nchi hiyo ilieleza.

Makundi ya watu wakiwa na fimbo

Chanzo cha picha, Getty Images

Machafuko yalianza jumamoja lililopita baada ya madereva wa malori raia wa nchini Afrika kusini kuanzisha mgomo wakipinga ajira zinazotolewa kwa raia wa kigeni.

Nchi hiyo imekuwa ikiwavuta wahamiaji kutoka sehemu mbalimbali za Afrika kwa kuwa ni moja kati ya nchi zilizo na maendeleo makubwa ya kiuchumi.

Hata hivyo kuna changamoto kubwa ya ukosefu wa ajira nchini humo na baadhi ya watu wanahisi raia wa kigeni wanachukua ajira zao.