Tanzia: Harakati na mapambano ya Robert Mugabe

Chanzo cha picha, AFP
Kama waziri mkuu wa kwanza wa Zimbabwe na baadae rais, Robert Gabriel Mugabe alihidi kuleta Amani na usuluhishi.
Lakini matumaini yaliyoleta uhuru mwaka 1980 yakasababisha migogoro, rushwa na kuanguka kwa uchumi.
Rais Mugabe akawa mkosoaji mkubwa wa nchi za magharibi, sana ikiwa Uingereza nchi iliyotawala Zimbabwe na aliita ni nchi adui.
Mbali na mkono wake wa chuma kwa viongozi wa upinzani na jinsi alivyokuwa akiendesha uchumi bado baadhi ya viongozi wa Afrika waliendelea kumuunga mkono.
Robert Gabriel Mugabe alizaliwa katika koloni la Uingereza la Rhodesia (Zimbabwe ya sasa), tarehe 21 ya mwezi Februari mwaka 1924, alikuwa mtoto wa fundi seremala na miongoni mwa kabila la wengi la Washona.
Alisoma katika shule ya msaada ya kikatoliki na akahitimu kuwa mwalimu.
Alishinda nafasi ya masomo katika chuo cha Fort Hare huko Afrika Kusini, alipata shahada yake ya kwanza kati ya saba kabla hajaelekea Ghana kufundisha, alivutiwa sana na fikra za kiafrika na Kwame Nkurumah.
Mke wake wa kwanza Sally alikuwa ni Mghana.
Mwaka 1960 Mugabe alirudi Rhodesia, na kwanza alianza kazi katika harakati za ukombozi wa Afrika na Joshua Nkomo kabla hajawa mwazilishi wa chama cha ZANU.
Mwaka 1964, baada ya kutoa hotuba yake na kuwaita waziri mkuu wa Rhodesia na serikali nzima ''Cowboys'' Mugabe alikamatwa na kufungwa bila kufunguliwa mashtaka.

Chanzo cha picha, Getty Images
Mtoto wake alikufa akiwa bado jela na akakataliwa ruhusa ya kwenda kuzika.
Mwaka 1973 alikua bado kizuizini na alichaguliwa kama rais wa ZANU.
Baada ya kuachiwa aliongoza mashambulizi dhidi ya Rhodesia mafichoni.
Chama chake cha ZANU kiliungana na umoja wa Afrika Zimbabwe ama ZAPU.
Wakati wa makubaliano ya uhuru wa Rhodesia alionekana kuwa kiongozi mkakamavu wa Kiafrika na mwenye mahitaji yasiyopingika.
Mwaka 1976 alitembelea London, alisema kuwa huru kwa watu wa Zimbabwe ni kwa njia ya mtutu wa bunduki tu.
Wakati wa makubaliano
Namna yake ya kufanya majadiliano ilimletea heshima kwa wakosiaji wake, vyombo vya habari vilimsifia kama mwanamapinduzi mwenye kufikiri.
Mwaka 1979 yalifikiwa makubaliano ya kuicha huru na kutengenezwa kwa katiba mpya ya Jamhuri ya Zimbabwe na mwezi wa pili mwaka 1980 uchaguzi wa kwanza wa serikali mpya ulifanyika.
Uchaguzi ulimalizika kwa ushindi mkubwa sana kwa Mugabe ingawa kulikua na malalamiko kutoka kwa baadhi ya watu, ZANU ilipata ushindi wa kutosha.
Ushindi wa Mugabe ulimaanisha Wazungu wengi waanze kufunga mizigo yao tayari kwa kuondoka Rhodesia, wakati wafuasi wake wakicheza mitaani.
Lakini hotuba zake za mwanzo ziliweka mambo sawa, Mugabe aliahidi serikali yenye ushirikiano, kusingekua na namna yoyote ya kutaifisha mali binafsi, lengo lake alisema litakua ni makubaliano.

Chanzo cha picha, Getty Images
Baadae mwaka huo, alitoa sera yake ya kiuchumi, ikiwa na mchanganyiko wa biashara kati ya serikali na sekta binafsi.
Wakati huo waziri mkuu Nkomo alikua akisisitiza utawala wa Chama Kimoja. Uhasama baina yake na Mugabe ukaongezeka.
Baada ya kugundulika kwa mali kufichwa zinazomilikiwa na ZAPU, Nkomo na wenzake walipunguzwa na akaondolewa serikalini.
Wakati akiendela kubana demokrasia, Mugabe alihakikisha wapinzani wake hawapumui vizuri.
Katikati ya mwaka 1980 yalifanyika mauaji ya maelfu ya wafuasi wa Nkomo kutoka kabila la Ndebele eneo la Matabaleland.
Ubinafsishaji
Mugabe alihusishwa na mauaji hayo ambao yalitekelezwa na kundi la jeshi lilipata mafunzo Korea Kaskazini, lakini hakuchukuliwa hatua zozote.
Kwa msukumo mkubwa Nkomo alilazimishwa kukubali chama cha cha ZAPU kuungana na ZANU na kuwa chama kimoja kikubwa ZANU-PF.
Baada ya kuvunjwa kwa ofisi ya waziri mkuu, Mugabe akawa rais tena 1987 na kisha akashinda tena muhula wa tatu mwaka 1996.
Mwaka huo huo akamuoa mkewe Grace Marufu, baada ya mke wake wa kwanza kufariki kwa ugonjwa wa kansa.
Mugabe alikua tayari na watoto wawili na watatu akazaliwa wakati mugabe akiwa na miaka 73.

Chanzo cha picha, AFP
Alipata mafanikio ya kuweka jamii isiyo na ubaguzi, lakini mwaka 1992 alitambulisha sheria ya ardhi ambao ilipelekea ubinafshwaji wa adhri bila kukata rufaa.
Mpango huo, ulilenga kupokonywa ardhi ya zaidi ya wakulima wa kizungu 4,500 ambao walikua wakimiliki maeneo mazuri ya nchi hiyo.
Mapema mwaka 2000, huku uraisi wake ukiwa katika mashaka baada ya kuundwa kwa chama kipya cha MDC kilichoongozwa na kiongozi mwenzake wa zamani wa vyama vya wafanyakazi Morgan Tsvangirai, Mugabe akawaondoa wakulima
Wafuasi wake waliokua wakijiita ''mashujaa wa kivita'' walivamia maeneo hayo yaliyomilikiwa na wazungu, baadhi wa wakulima waliuawa na wafanyakazi wao weusi.
Misaada ya kimataifa
Suala hili lilisababisha uchumi wa Zimbabwe uzidi kudidimia, wakosoaji wa Mugabe walilalamika kuwa kitendo chake kimesababisha uharibifu.
Zimbabwe ikaporomoka haraka sana kutoka kuwa moja ya nchi zenye uchumi mkubwa hasa katika kilimo hadi kutegemea misaada kulisha wananchi wake.
Uchaguzi wa mwaka 2000 wa wabunge, MDC ilishinda viti 57 kati ya 120 huku viti 20 vikashikiliwa na walioteuliwa na Mugabe.
Miaka miwili baadae, katika uchaguzi wa Urais Mugabe alipata 56%.2 dhidi ya mpinzani wake Tsvangirai akiwa na 41%.9. idadi kubwa ya watu maeneo ya vijijini walipata vikwazo kwenye kupiga kura kutokana na vituo vya kupigia kira kufungwa.

Chanzo cha picha, AFP
MDC, pamoja na Marekani, Uingereza na Umoja wa Ulaya hawakutambua matokeo ya uchaguzi kutokana na vurugu lakini pia malalamiko ya wizi wa kura.
Mugabe na Zimbabwe ikazidi kutengwa na mataifa ya nje. Jumuiya ya madola pia ilizuia Zimbabwe kushiriki mikutano yake hadi pale demokrasia itakaporudi.
Mwezi wa tano mwaka 2015, Mugabe alitambulisha operesheni ya kuleta amani na kuondoa biashara haramu.
Wafanyabiashara ndogo ndogo za mtaani zaidi ya 30,000 walikamatwa na vibanda vyao kubomolewa na kuacha zaidi wa wazimbabwe 70,000 wakiwa hawana makazi.
Mzozo
Mwezi machi 2008, Mugabe alishindwa katika awamu ya kwanza ya uchaguzi wa uraisi, ingawa baadae mwezi June, alishinda baada ya Mpinzani wake Tsvangirai kujiondoa kwenye kinyang'anyiro hicho.
Baada ya ushindi huo, Tsvangira alieleza kwamba , ni vigumu kuwa na uchaguzi huru na wa haki nchini humo.
Uchumi wa Zimbabwe uliendelea kushuka huku bei ya bidhaa ikiongezeka maradufu.
Baada ya watu kuanza kupoteza maisha kutokana na ugonjwa wa kipindupindu kufuatia serikali kushindwa kugharamia kutibu maji kwa kutumia kemikali raisi Mugabe alifiakiana na adui zake wa muda mrefu kushiriki madaraka.

Chanzo cha picha, Getty Images
Baada ya miezi kadhaa ya mazungumzo, hatimaye mwezi februari 2009 bwana Tsvangirai aliapishwa kuwa waziri mkuu wa Zimbabwe.
Haikuwa ni kitu cha kushangaza pamoja na mabadiliko yaliyofanywa kutokana na mzozo na mashitaka ya mara kwa mara kutoka kwa taasisi za haki za binadamu kuwa wapinzani wa kisiasa wa Mugabe walikuwa wakikamatwa na kuteswa.
Sifa ya bwana Tsvangirai pia ilishuka kutokana na kujihusisha na utawala wa Mugabe kama waziri mkuu pamoja na kuwa hakuwa na nguvu kwenye utawala huo.
Kwenye uchaguzi mkuu 2013 ambao raisi Mugabe alishindwa kwa 61% ya kura zote alivunja makubaliano ya kuchangia madaraka na bwana Tsvangirai na Huku bado kukiwa na malalamiko ya wizi wa kura katibu mkuu wa umoja wa mataifa Ban Ki-Moon aliingilia kati kutaka uchunguzi ufanyike. Kwa kipindi hicho hakuna machafuko makubwa yaliyotajwa katika chaguzi zilizofanyika nchini Zimbabwe.
Warithi
Kwa kadiri miaka yake ilivyozidi kuongezeka huku na matatizo ya kiafya pia yakizidi kuongezeka yalileta minong'ono ya nani wa kuichukua nafasi yake.
Lakini fitna ziliendelea kufanyika kwa wale walioonekana wanaweza kuchukua nafasi ya yake na hivyo kuthibitisha namna uongozi wa Zimbabwe unashikiliwa na Mugabe pekee.
Na hata Mugabe alionekana kuvunja nguvu ya utawala wowote uliokuwa kinyume nae.
Kufuatia uvumi wa mkewe Grace kutaka kutawala pale mume wake atakapofariki akiwa madarakani Mugabe alitangaza nia yake ya kugombea tena mwaka 2018 ambapo angekuwa na umri wa miaka 94.

Chanzo cha picha, AFP
Na katika kuondoa maswali yaliyokuwa yamebaki kati ya wale waliokuwa wakidhaniwa huenda wangekuwa warithi, mwezi Februari Mugabe alitangaza rasmi kuwa ataendelea kuwa madarakani mpaka pale Mungu atakapomuita.
Kufuatia tukio hilo haikuwa tena Mungu ila ni umoja wa majeshi wa Zimbabwe ndiyo yaliyomuita Mugabe. Mnamo mwezi Novemba 2017 aliwekwa kizuizini kwa siku nne huku aliyekuwa makamo wake Emmerson Mnangagwa akichukua nafasi yake kama kiongozi wa Zanu-PF.
Novemba 21 spika wa bunge la Zimbabwe alitangaza rasmi kujiuzulu kwa raisi Mugabe baada ya muda mrefu kukataa kibabe kufanya uamuzi huo.
Mugabe alifikia makubaliano ya kupata ulinzi kwake na familia yake kutokana na hofu ya kuuawa na kuendeleza biashara yake. Pia alipatiwa nyumba, wafanyakazi, usafiri na hadhi yake ya kidiplomasia.
Kama ilivyo tabia yake ya kutopenda anasa Robert Mugabe alivaa kawaida na hakutumia kilevi.
Mtu ambaye alikua akitukuzwa kama mshindi katika mapigano ya Afrika kuushinda ukoloni amegeuka kuwa dikteta, akikiuka haki za binadamu na kugeuza nchi ambayo ilikuwa ni yenye utajiri
Mchango wake utaendelea kukumbukwa miaka na miaka.













