Robert Mugabe amefariki dunia akiwa na miaka 95

Robert Mugabe
Maelezo ya picha, Robert Mugabe
Muda wa kusoma: Dakika 2

Rais wa zamani wa Zimbabwe, Robert Mugabe amefariki dunia.

Mmoja wa wanafamilia ameithibitishia BBC kuwa, Robert Mugabe amefariki dunia akiwa na miaka 95.

Mugabe alikuwa nchini Singapore akipokea matibabu kwa muda mrefu.

Ameiongoza Zimbabwe kutoka 1980 mpaka 2017, alipong'olewa madarakani na makamo wake kwa msaada wa jeshi.

Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa tayari amethibitisha kupitia mtandao wa twitter juu ya taarifa za kifo hicho.

Ruka X ujumbe, 1
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa X ujumbe, 1

"Kamarada Mugabe alikuwa ni mwanga wa mapinduzi, mwana umajui wa Afrika ambaye aliyatoa maisha yake katika ukombozi na kuwawezesha watu wake. Mchango wake kwa taifa letu na bara (la Afrika) hautasahaulika..." ameandika Mnangagwa.

Magufuli, Kenyattawamlilia Mugabe

"Nimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo cha Rais Mstaafu na Baba wa Taifa la Zimbabwe Mzee Robert Mugabe. Afrika imepoteza mmoja wa viongozi Jasiri, Shupavu, Mwanamajumui wa Afrika na aliyekataa ukoloni kwa vitendo. Mungu aiweke roho yake mahali pema peponi, Amina," ameandika raisi wa Tanzania John Pombe Magufuli kupitia ukurasa wake wa twitter.

Ruka X ujumbe, 2
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa X ujumbe, 2

Naye raisi wa Kenya, Uhuru Kenyatta ametuma salamu za rambirambi akisema hana maneno ya kutosha kuelezea uzito wa kuachwa na kiongozi shupavu, shujaa na mzalendo wa Afrika ambaye alitekeleza jukumu muhimu katika kutetea maslahi ya bara la Afrika.

Maelezo ya video, Enzi ya kisiasa ya Mugabe

Kwa wakati huu wa majonzi, mawazo na maombi yangu ni kwa jamaa, ndugu na watu wa Zimbabwe ambao kwa miaka mingi aliwatumikia kwa kujitolea na kwa bidii...Bila shaka, tutamkumbuka Rais huyo wa zamani Robert Mugabe kama mtu jasiri ambaye kamwe hakuogopa kuelezea msimamo wake kwa jambo lolote hata kama wengi hawakumuunga mkono. Kwa familia yake, Serikali na raia wa Zimbabwe, Mola awafariji na ailaze roho ya Rais wa zamani Robert Mugabe mahala pema peponi," ameeleza Mugabe.

'Kinara wa mapinduzi'

Mugabe

Chanzo cha picha, Getty Images

Mugabe alizaliwa Februari 21, 1924 kwenye koloni la Rhodesia.

Alitupwa jela kwa miaka 10 bila ya kufunguliwa mashtaka kwa kuukosoa uongozi wa Rhodesia mwaka 1964.

Mwaka 1973, yungali gerezani alichaguliwa kuwa raisi wa chama cha Zimbabwe African Union (Zanu), ambacho alikuwa ni mwanachama mwanzilishi.

Baada ya kuachiwa kutoka gerezani, alikimbilia Msumbiji na kuongoza mapambano ya kijeshi ya kudai uhuru.

Licha ya kuwa mpiganaji wa vita vya kushtukiza, alisifika kwa kuwa mzuri kwenye majadiliano.

Mwaka 1980 akafanikiwa kuingia madarakani baada ya uchaguzi uliomaliza utawala wa walowezi wachache wa kizungu.