Kenya: Ni nani anayewaua vijana 'kiholela' katika mitaa ya mabanda?

Katika vitongoji vya jiji la Nairobi, nchini Kenya inaelekea kuwa jambo la kawaida kupata miili ya vijana wengi wao maskini ikiwa imetupwa barabarani.
Vyombo vya usalama vimekua vikiendesha kampeini ya chini kwa chini ya kupambana na uhalifu lakini sasa jamii inadai kuwa vijana hawa wanawauwa na polisi.
Ikiwa Ulimwengu leo unaadhimisha siku ya waathiriwa wa mauaji ya kiholela BBC ilizuru mtaa wa mabanda wa Mathare viungani mwa Nairobi kuangazia hali ya ilivyo.
Lucy(si jina lake la kweli) alimpoteza mwanawe miaka mitatu iliyopita, kijana huyo,tuliyempatia jina la Paul(kwa sababu za kiusalama) alikuwa na umri wa miaka 22,alipodaiwa kuuawa na askari akiwa njiani kwenda kumtembelea mwanawe mgonjwa hospitalini.

Mama yake anasema walioshuhudia tukio la kuua kwake wanasema ni askari aliyekuwa amevalia kofia isiyokuwa rasmi.
''Nilisikia ni askari alitokezea na kumwelekezea bunduki, Paul alipoinua mikono juu kusalimu amri haikuwezekana akampiga tu risasi na akaanguka chini,'' Mama yake aliiambia BBC.
Japo ni miaka mitatu sasa anasema kifo cha Paul kiliiacha familia yake na huzuni na kiwewe.
Mama yake mzazi anasema kila wakati anawazia kumuona, mwanawe na kila anapojaribu kukubali kuwa mwanawe ameuawa anashikwa na majonzi. ''Kiifo chake kimenirudisha nyuma sana,'' anasema.
Lucy na mumewe waliponea ajali ya barabarani na kulazimika kutoendelea kufanya kazi kutokana na majeraha.
Paul alikua akifanya kazi ya kuwafunza vijana wenzake jinsi ya kujipatia kipato kupitia kilimo katika shirika ambalo lilikuwa linafadhiliwa na wahisani kutoka Sweden.
Kupitia kazi hiyo alikuwa akisaidia familia yake: ''Hata alikuwa akiniambia mama ukitoka kazi pitia hapa uchukue kitu kidogo ukapike chakula'' anasema mama Lucy.

Katika eneo hilo la Matahre Area 4, BBC pia ilikutana na mama Magdalane (sio jina lake halisi) ambaye mume wake aliuawa kwa madai ya kuwa mwizi.
Walikuwa wakilala kwenye nyumba yao ya mabati walipovamiwa na vijana chini ya uongozi wa polisi usiku wa manane.
''Waliingia na mlangowakamchukua kitandani wakmfunga pingu na kutoka nae sikujua walikompeleka'' alisema Magdaline.
Katika hiyo harakati helmet ya mmoja wa polisi iliaanguka nikamtambua huyo askari kwasababu nishawahi kumuona tena namjua''
Muda mfupi baadaye alipatiakana amewauwa mume wake alipatikana ameuawa.
Magadalene anadai kuwa polisi huyo aliwatumia vijana hao kwani tayari alikuwa na kesi nyingine ya mauaji.

Mamake pole anadai licha ya madai ya mwanawe kuwa mwizi hakufaa kuwauwa kinyama.
''Ni uchungu kwa maisha yangu, angeenda afungwe hata kama ni ni miaka 30 sina shida kulingana na ile kosa walimpata nayo.. si ni ukweli?'' aliuliza huku akisimulia kwa masikitiko mauji hayo.
Ingawa uchungzi umeanzishwa na Tume Huru inayochunguza mauaji ya polisi,mama huyu anadai kuwa amekuwa akitishiwa na watu fUlani wanaomtaka kuchana na kesi hiyo.
Vijana katika mtaa huo sasa wanadai polisi wanataka kumaliza kizazi kizima, lakini msemaji wa polisi Charles Owino anapinga madai hayo.
''Sheria iko wazi kabisa.Tuna mazingira ambayo polisi anaruhusiwa kutumia silaha yake.Moja wakati anapolinda maisha yake na pili anapolinda maisha ya raia'' Owino aliiambia BBC.
''Tuna bahati kama nchi kwa kuwa kando na kuwa na kitengo cha ndani kuchunguza malamishi dhidi ya polisi,tuna kitengo cha kiraia cha kupokea malalamishi ya raia na kufanya uchunguza huru'' aliongezea kusema

Chanzo cha picha, AFP/GETTY
Kituo cha kijamii cha Mathare social Justice kimekuwa kikirekodi mauaji yote yanayofanyika na kinasema kuwa njia hii imesaidia kupunguza mauaji yanayodaiwa kutekelezwa na polisi.
''Kufikia sasa rekodi zetu zinaonesha kuna vifo 69 ambavyo tumeandikisha ikilinganishwa na 264 tulivyonakili miaka miwili iliyopita'' alisema afisa wa kituo hicho Kennedy Chindi.
Japo idadi ya mauji yamepungua ikilinganishwa na hali ilivyokuwa mwaka 2017 na 2018 kibarua ni kuhakikisha mauaji ya kiholela yanakomeshwa katika mitaa ya iliyopo viungani mwa jiji la Nairobi.
Sasa nini kifanyike? Swali hilo linaendelea kutafutiwa ufumbuzi na wanaharakati wa kutetea haki za binadamu.













