Kashmir yalishutumu jeshi kutesa raia

Vikosi vya usalama nchini India vinavyosimamia upande wa Kashmir vimeshtumiwa kwa kuwapiga na kuteswa watu kwa muongozo waliopewa na serikali ili kuwanyima uhuru watu wa eneo hilo .
BBC ilisikia kutoka kwa baadhi ya wanakijiji wakisema kuwa walikuwa wanapigwa na fimbo na kuteswa kwa kutetemeshwa na umeme.
Wakazi wa vijiji kadhaa walionyesha majeraha waliyoyapata ingawa BBC ilishindwa kuthibitisha madai hayo kwa upande wa maofisa wa serikali.
Jeshi la India liliwaita watu hawa kuwa ni watu wasio na umuhimu wala hawana msaada wowote.
Kashmir imewekewa vizuizi ambavyo vimewafunga zaidi ya wiki tatu sasa na taarifa ilibainika tangu Agosti 5 kufuatia ibara ya 370 kuwapa hadhi maalum ya kujitawala, kupingwa.
Silaha zaidi ya elfu kumi zimewasili katika eneo hilo na watu wapatao 3000 wakiwemo wanasiasa, wafanyabiashara na wanaharakati wameripotiwa kushikiliwa na jeshi la polisi.
Wengi wamehamishiwa katika magereza yaliyopo nje ya Kashmir.
Mamlaka inasema kuwa hatua hiyo imekuja ili kuhakikisha kuwa sheria na utaratibu unafuatwa katika eneo hilo , ambalo lina waislamu wengi katika taifa hilo lakini sasa wamegawanyika katika sehemu mbili.
Jeshi la India limekuwa likiendesha mapigano hapa kwa zaidi ya miongo mitatu.
India inailaumu nchi jirani ya Pakistan kwa kuchochea vurugu katika eneo hilo kwa kuwaunga mkono wapiganaji- lakini nchi hiyo imepinga kuhusika na mzozo huo.
Watu wengi waliovuka kwenda India wamekubali mabadiliko yaliyoandikwa katika ibara ya 370 na kusifia maamuzi ya waziri mkuu Narendra Modi .
Maamuzi hayo yaliungwa mkono na vyombo vingi vya habari.
Jinsi baadhi ya wanakijiji walivyoteswa


"Walinipiga kila eneo la mwili wangu, walitufukuza kwa fimbo, na kututetemesha kwa waya za umeme".
"Walitupiga nyuma ya miguu kwa fimbo, tulipiga kelele sana hivyo waliamua kutuziba midomo yetu kwa matope.
Tuliwaambia kuwa sisi hatuna hatia lakini hawakutusikiliza? Waliendelea kutupiga, niliomba Mungu anichukue kwa sababu ya mateso nilikuwa nayapata niliyokuwa nashindwa kuyavumilia,"
Mwanakijiji mwingine alidai askari hao walimtaka atoe miwani yake, avue nguo zake na viatu, "nilikuwa hiari kufanya kila kitu walichoniambia lakini wakinifanyia hivyo tena niko radhi kuchukua bunduki na kujiua siwezi kuvumila tena".
Kijana mwingine aliongeza kuwa askari waliwaonya kutofanya maandamano tena na wakirudia watapata changamoto hiyo hiyo.

Jeshi la India liliwaandikia BBC kukanusha vitendo hivyo na kudai kutomtesa raia yeyote.
"Hakuna madai yoyote yaliyoletwa kwetu. Inawezekana kabisa hicho wanachokidai imchochewa na vurugu, alisema msemaji wa jeshi Aman Anand .
Hatua za kuwalinda wananchi zinachukuliwa lakini hakuna raia ambaye ameteswa na jeshi", msemaji huyo aliongeza.
Jeshi hilo limekataa kuhusika na matukio yoyote ya kunyanyasa raia.
Katika barua waliyoiandikia BBC wamedai kuwa wao wanafanya kazi kitaaluma na wanaelewa umuhimu wa kuwalinda na kuhesimu haki za binadamu, madai yote juu yao watayafanyia uchunguzi haraka.
Umoja wa mataifa pia imejipanga kufanya ucunguzi huru dhidi ya madai hayo ya kukiukwa kwa haki za binadamu.
Kwanini Kashmir ni eneo tata?
Kashmir ni eneo lililopo kwenye safu za milima ya Himalaya na nchi zote mbili India na Pakistani zinadai kuwa ni eneo lao.
Katika kipindi cha ukoloni wa Mwingereza jimbo la Jammu na Kashmir lilikuwa na hadhi ya kujitawala kupitia kiongozi wa makabila, lakini likajiunga na India mwaka 1947 katika kipindi ambacho Bara Hindi lilipatiwa uhuru na kugawanywa katika mataifa mapya ya India na Pakistani.
Nchi hizo mbili huenda zikatumbukia vitani na kujikuta kila mmoja akishikilia sehemu ya eneo hilo baada ya makubaliano ya kusimamisha mapigano yalipoafikiwa.
Kumekuwa na ghasia katika upande wa jimbo hilo utakaotawaliwa na India kwa kipindi cha miaka 30 iliyopita.
Makundi ya wanaharakati wanaotaka kujitenga na India yamekuwa yakishinikiza kupewa uhuru wao.


Kashmir ni eneo lililopo kwenye safu za milima ya Himalaya na nchi zote mbili India na Pakistani zinadai kuwa ni eneo lao.
Katika kipindi cha ukoloni wa Muingereza jimbo la Jammu na Kashmir lilikuwa na hadhi ya kujitawala kupitia kiongozi wa makabila, lakini likajiunga na India mwaka 1947 katika kipindi ambacho Bara Hindi lilipatiwa uhuru na kugawanywa katika mataifa mapya ya India na Pakistani.
Ibara hiyo ndiyo inayoipa Kashmir upekee na hadhi ya kujitawala.
Serikali ikashangaza kila mmoja kwa kufuta ibara nzima ya 370 ambapo 35A ni ibara ndogo, na sehemu hiyo ya katiba ndiyo imekuwa mwongozo wa sera za nchi hiyo juu ya Kashmir kwa miongo saba iliyopita.















