Picha za mkewe mfalme Maha Vajiralongkorn wa Thailand akiendesha ndege ya kivita zasambaa

Sineenat Wongvajirapakdi, pictured here piloting a fighter jet, was appointed the king's royal consort in July

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha, Sineenat Wongvajirapakdi, akiendesha ndege ya kivita

Picha adimu za mkewe mfalme wa Thailand aliyepewa wadhifa hivi karibuni zimetolewa na kasri, na inaarifiwa kusambazwa pakubwa mitandaoni.

Sineenat Wongvajirapakdi, mwenye umri wa miaka 34, anaonekana akiendesha ndege ya kivita , akiwa amevalia magwanda ya vita na kufyetua bunduki.

Wadhifa wa 'consort' aliopewa Sineenat hutolewa na mfalme kwa mkewe au na Malkia kwa mumewe.

Mfalme Maha Vajiralongkorn, mwenye umri wa miaka 67, alimpa heshima hiyo Sineenat mnamo Julai, miezi miwili baada ya kumuoa Malkia Queen Suthida, mkewe wa tatu.

Sineenat ni mwanamke wa kwanza kushikilia wadhifa huo katika karibu karne nzima, shirika la habari la AFP linaripoti.

Sineenat Wongvajirapakdi pictured taking part in the Royal Cremation ceremony of Thailand's late King Bhumibol Adulyadej

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Sineenat Wongvajirapakdi akishiriki katika hafla ya kuteketeza mwili wa marehemu mfalme Bhumibol Adulyadej

Mtandao uliokuwa na picha hizo ulikabiliwa na matatizo baadaya watu wengi kujaribu kuingia kuzitazama pica hizo kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters.

Wasifu wake umechapishwa karibu napicha hizo zake.

Thai King Maha Vajiralongkorn (L) holding a poodle next to royal consort Sineenat Wongvajirapakdi (R)

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha, Mfalme Maha Vajiralongkorn akimshikilia mbwa akiwa karibu na Sineenat Wongvajirapakdi

Katika taarifa yake, Kasri la Thailand linasema mfalme "aliagiza kuundwa kwa maelezo ya maisha ya kifalme" ya Sineenat, ambaye ni rubani wa kusomea, mhudumu wa afya na mlinzi binafsi.

Malkia Suthida - aliye na miaka 41- ni mhudumu wa zamani wa ndege na naibu mkuu wa kitengo cha ulinzi wa mfalme - ni mpenzi wa muda mrefu wa Mfalme Vajiralongkorn na ameonekana hadharani naye kwa miaka mingi.

Alitawazwa kuwa mfalme baada ya babake kufariki mnamo 2016.

Mfalme anaonekana akimwaga maji ya baraka kwenye kichwa cha Malkia Suthida

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha, Mfalme anaonekana akimwaga maji ya baraka kwenye kichwa cha Malkia Suthida
Sineenat Wongvajirapakdi aims a weapon at a firing range

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Sineenat Wongvajirapakdi akilenga silaha