Marekani yatoa amri ya kukamatwa kwa meli ya Iran iliyoachiliwa Gibraltar

Meli ya mafuta ya Iran

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Meli ya mafuta ya Iran

Marekani imetoa amri ya kukamatwa kwa meli ya mafuta ya Iran siku moja baada ya jaji wa Gibraltar kuagiza meli hiyo iachiliwe.

Grace ambayo ilikuwa ikibeba tani milioni 2.1 ya mafuta, ilizuiliwa Julai tarehe nne kwa kushukiwa kusafirisha mafuta kimagendo nchini Syria.

Uamuzi wa dakika za mwisho ya kutaka meli hiyo iendelee kuzuiliwa ilipingwa na Gibraltar siku ya Alhamisi.

Iran ilisema kuamatwa kwa meli yake Grace 1 ni "kinnyume cha sheria".

Wiki mbili baada ya meli ya Grace 1 kuziliwa, Julai 19 Iran iliteka meli iliyokuwa na bendera ya Uingereza kwa jina Stena Impero katika eneo la Hormuz.

Japo Iran inasema meli hiyo meli hiyo ''ilikiuka sheria ya kimataifa ya mpaka wa baharini ", kukamatwa kwa Stena Impero inaaminiwa kuwa hatua ya kilipiza kisasi .

Meli ya kijeshi katika mkondo wa Hormuz

Marekani ilisema nini ?

Marekani iliomba taifa hilo kufikiria tena huku kesi yake iliyokuwa ikitarajiwa kusikilizwa saa tisa muda wa Uingereza.

Gibraltar imesema kuwa ombi hilo la Marekani linatokana na baadhi ya madai ambayo yanaangaziwa kwa sasa.

Wizara ya maswala ya kigeni nchini Uingereza imesema kuwa haiwezi kuzungumza kuhusu ombi hilo la Marekani.

Gibraltar ilipokea barua rasmi ya hakikisho kutoka kwa Iran kwamba meli hiyo haitapeleka mafuta yake nchini Syria

Idara ya haki nchini Marekani iliwasilisha ombi la dakika za mwisho kwa mamlaka nchini Gibraltar kuzuia kuachiliwa kwa meli hiyo ya Iran

Meli hiyo kwa jina Grace 1 iliokuwa ikibeba mafuta ilikamatwa na wanamaji wa Uingereza tarehe 4 Julai hatua iliosababisha mgogoro na Iran.

Maelezo ya video, Hormuz: Kwa nini eneo hili linaweza kuathiri maisha yako duniani

Uingereza ilitaka meli hiyo ya Iran kuachiliwa?

Mwandshi wa maswala ya ulimwengu wa BBC Marcus Jonathan anasema kwamba Uingereza imekuwa ikitumai kwamba kuachiliwa kwa Grace 1 kutasababisha kuachiliwa kwa meli inayopeperusha bendera ya Uingereza ya Stena Impero iliokamatwa na Iran katika Ghuba.

Msemaji wa serikali ya Gibraltar pia alithibitisha kwamba uchunguzi wa polisi dhidi ya wafanyakazi wote wa nne wa meli hiyo akiwemo nahodha raia wa India umekamilika.

Mawakili wa wafanyakazi hao waliambia BBC kwamba maafisa wa polisi walisema kwamba hilo linatokana na vitendo vya serikali ya Iran na kwamba haikuwa hamu ya umma kuendelea nayo.

Meli hiyo ya mafuta ilikamatwa baada ya serikali ya Gibraltar kusema kwamba ilikuwa inaelekea Syria ikiwa ni ukiukaji wa vikwazo vya Muungano wa Ulaya.

Takriban wanamaji 30 walisafirishwa kutoka Uingereza kuelekea Gibraltar ili kuwasaidia maafisa wa polisi kuizuia meli hiyo ya mafuta na mizigo yake kufuatia ombi la serikali ya Gibraltar.

Kukamatwa kwa meli hiyo kulizua mgogoro wa kidiplomasia kati ya Uingereza na Iran ambao umeongezeka katika wiki za hivi karibuni.

Meli ya mafuta ya Grace 1

Chanzo cha picha, Reuters

Hofu yatanda kati ya Iran na mataifa ya magharibi

Wiki iliopita , Uingereza ilitangaza kwamba itajiunga na jopo la Marekani la kulinda meli za kibiashara zinazosafiri kupitia njia muhimu ya meli katika mkondo wa Hormuz.

Hali ya wasiwasi kati ya Iran na magtiafa ya magharibi inatokana na mpango wa kinyuklia wa Iran.

Mwaka uliopita , Washington ilijiondoa katika mpango huo wa 2015 ili kupunguza vitendo vya kinyuklia vya Iran huku kukiwa na madai kwamba taifa hilo lilikuwa likijaribu kutengeza silaha za kinyuklia, kitu ambacho Iran imekuwa ikikana.

Tangu wakati huo hofu imetanda kati ya Iran na Marekani baada ya Washington kuimarisha vikwazo dhidi ya taifa hilo.

Uingereza na mataifa ya Ulaya yamesema kwamba bado yamesalia katika mkataba huo.