Mshambuliaji mmoja alivamia duka la jumla la Walmart Texas mjini El Paso huku mwengine akishambulia huko Dayton Oregon

Shambulio la Walmart Texas
Muda wa kusoma: Dakika 4

Takriban watu 20 wameuawa huku wengine 26 wakijeruhiwa katika ufyatuliaji wa risasi katika duka la jumla mjini El Paso jimbo la Texas .

Gavana wa jimbo hilo Greg Abbot amelitaja shambulio hilo kuwa mojawapo ya siku mbaya zaidi katika historia ya jimbo la Texas. Maafisa wa polisi wanachunguza iwapo shambulio hilo ambalo lilifanyika maili chache kutoka kwa mpaka wa Marekani na Mexico lilikuwa la uhalifu wa chuki.

Mtu mwenye umri wa miaka 21 kwa sasa anazuiliwa na maafisa wa polisi.

Wakati huohuo Watu tisa wameuawa na wengine 26 kujeruhiwa katika shambulio jingine la watu wengi katika eneo la Dayton Ohio.

Meya Nan Whaley alisema waliojeruhiwa walipelekwa katika hospitali kadhaa kati mji huo.

Dayton Oregon

Chanzo cha picha, CBS

Shambulio hilo lilianza mwendo wa saa saba na dakika saba saa za Marekani katika wilaya ya Oregon mjini humo.

Maafisa wa polisi walithibitisha mshambuliaji aliuawa katika eneo hilo baada ya kufyatuliana risasi na maafisa wa polisi.

Meya Nan Whaley aliambia ripota kwamba alishangazwa na hatua za haraka zilizochukuliwa na maafisa wa polisi ambayo anasema walizuia vifo zaidi , lakini pia akashinikiza kwamba itakuwa wakati mgumu sana kwa familia za waathiriwa.

Ninini kilichotokea Dayton?

Kanda za video katika mitandao ya kijamii iliwaonyesha watu wakikimbia huku milio mingi ya risasi ikisikika katika barabara.

Inadaiwa kwamba shambulio hilo lilifanyika nje ya klabu ya burudani ya Red Peppers katika barabara ya tano ya E .

Klabu hiyo baadaye ilichapisha katika mtandao wa twitter ikisema wafanyakazi wake wako salama.

Polisi wanasema kuwa wote walioathirika walikuwa barabarani.

Polisi wanasema kwamba mshukiwa huyo alikuwa akiishi katika eneo la Allen , Dalla yapata kilomita 1,046 mashariki mwa El Paso. Ametajwa na vyombo vya habari vya Marekani kuwa Patrick Crusius.

Kanda za video za CCTV zilizodaiwa kuwa za mshambuliaji huyo ambazo zilionyeshwa katika vyombo vya habari vya Marekani zinaonyesha mtu aliyekuwa amevalia Tishati nyeusi pamoja na vilinda masikio.

kanda ya video ya CCTV ikimuonysha mshukiwa wa shambulio hilo

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, kanda ya video ya CCTV ikimuonysha mshukiwa wa shambulio hilo

Shambulio hilo la Texas linaaminika kuwa la nane katika historia ya sasa nchini Marekani.

Linajiri chini ya 24 baada ya shambulio jingine la kuwafyatulia risasi watu waliokongamana, mjini Dayton Ohio na chini ya wiki moja baada ya mshambuliaji kijana kuwaua watu watatu katika tamasha la chakula mjini California.

Maafisa wa polisi na wenzao wa ujasusi wa shirika la FBI wanafanya uchunguzi iwapo manifesto ya kitaifa iliochapishwa katika kundi moja la mtandao iliandikwa na mshambuliaji huyo.

Chapisho hilo linadai kwamba shambulio hilo lililenga jamii ya Uhispania.

Mwathiriwa wa shambulio la Walmart

Duka hilo ambalo liko karibu na duka jingine kubwa kwa jina Cielo Vista Mall lilikuwa limejaa wateja waliokuwa wakinunua bidhaa za wanao wao kurudi shule wakati wa shambulio hilo.

Rais wa Marekani Donald Trump alielezea shambulio hilo kama kitendo cha uoga.

''Najua kwamba tunaungana na kila mtu katika taifa hili kushutumu kitendo hiki cha chuki, hakuna sababu ambazo zinaweza kukufanya kuwaua watu wasio na hatia'' , alindika katika mtandao wake wa Twitter.

Waathiriwa bado hawajatajwa lakini rais wa Mexico Andres Manuel Lopez Obrador alisema kuwa raia watatu wa Mexico ni miongoni mwa waliofariki, kulingana na chombo cha habari cha Reuters.

"Sisi kama taifa tunaungana kuwaunga mkono waathiriwa na familia zao'' , alisema bwana Abbot.

Lazima tufanye kitu kimoja , leo chengine kesho na kila siku baada ya hili - lazima tushirikiane.

Nini kilifanyika?

Afisa mkuu wa polisi wa El Paso Greg Allen alisema kwamba ripoti za mtu aliyekuwa akiwafyatulia watu risasi kiholela ndani ya duka hilo ziliripotiwa mwendo wa saa za Marekani 10:39 na maafisa walitumwa katika eneo la mkasa huo chini ya dakika sita.

Mtu huyo mwenye umri wa miaka 21 ndiye mshukiwa pekee anayezuiliwa, na polisi inasema kwamba hakuna afisa aliyefyatua risasi wakati walipomkamata jamaa huyo.

Ruka X ujumbe
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa X ujumbe

Presentational white space

Kianna Long alisema kwamba alikuwa katika duka hiyo na mumewe wakati waliposikia mlio wa risasi.

''Watu walikuwa na wasiwasi na kukimbia , wakisema kwamba kulikuwa na mtu aliyekuwa akiwafyatulia risasi, Bi Long aliamba Reuters. Walikuwa wakikimbilia sakafu na kujiangusha''.

Bi Long alisema kwamba yeye na mumewe walikimbia ndani ya chumba cha kuhifadhi bidhaa ambapo walijificha na wateja wengine wa duka hilo.

Kianna Long (Kulia) akifarijiwa na mtu wa familia yake

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha, Kianna Long, kulia alizungumzia kuhusu wasiwasi uliokuwa katika duka la Walmart

Shahidi mwengine kwa jina Gleondon Oakley aliambia CNN alikuwa katika duka la bidhaa za michezo karibu na duka jingine la jumla lililopo karibu wakati mtoto mdogo alipotoroka na kuingia ndani na kutuambia kuna mtu anafyatua risasi kiholela katika Walmart.

Bwana Okley alisema kwamba hakuna hata mtu mmoja aliyejali matamshi ya kijana huyo lakini dakika moja baadaye alisikia milio miwili ya risasi.

''Nilifikiria kuwaondoa watoto katika eneo hilo''

Wateja walioshangazwa na tukio hilo walisaidiwa kutoka katika eneo hilo

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Wateja walioshangazwa na tukio hilo walisaidiwa kutoka katika eneo hilo

Je watu wamekuwa wakisema nini?

Kisa hicho cha hivi karibuni kimevutia huruma lakini bado kuna wito wa udhibiti wa bunduki.

Walmart ilituma ujumbe wa twitter ikisema kwamba ilishangazwa na tukio hilo na kwamba ilikuwa ikishirikiana na maafisa wa polisi.

Presentational white space
Ramani inayoonyesha eneo la tukio hilo
line