Unyanyapaa unavyowasukuma wanawake wenye hedhi India kutoa vizazi

An Indian man looks on as he walks along a wall painting about menstruation in Guwahati on May 28, 2019

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Kuna unyanyapaa mkubwa kuhusu hedhi India

Taarifa za kuogofya zinazowahusu wanawake wanaofanya kazi na walio kwenye hedhi zimeibuka India katika miezi ya hivi karibuni.

Hedhi ni suala linalokabiliwa na unyanyapaa mkubwa nchini, wanawake walio kwenye hedhi huaminika kuwa ni wachafu na wanatengwa katika jamii na shughuli z akidini.

Katika miaka ya hivi karibuni, fikra hizi potofu zimekuwa zikipingwa, hususan na wanawake waliosoma wanaoishi katika maenoe ya mjini.

Lakini visa viiwili vinadhihirisha ukubwa wa tatizo hili la unyanyapaa kwa wanawake India. Idadi kubwa ya wanawake, wengi wao kutoka familia masikini, ambao hawakusoma wanalazimika kufanya maamuzi yalio na athari za muda mrefu na zisizoweza kurekebishika kwa afya na maisha yao.

Mkasa wa kwanza umetokea katika jimbo la magharibi la Maharashtra ambapo maelfu ya wanawake wadogo wamefanyiwa upasuaji kutoa vizazi vyao katika miaka mitatau iliyopita - katika kinachoonekana kuwa visa vya kuwaruhusu kupata kazi katika mashamba ya miwa.

Kila mwaka, maelfu ya famili maskini kutoka wilaya za Beed, Osmanabad, Sangli na Solapur huhama na kuelekea katika wilaya tajiri zinazojulikana kama "the sugar belt" - kufanya kazi kwa miezi sita kama wakataji miwa katika mashamba.

Wanapofika huko, wamo mikononi mwa wakandarasi wanaopatiliza nafasi yoyote kuwatumia vibaya.

Mwanzoni, walisusia kuwaajiri wanawake kwasababu ukataji miwa ni shughuli inayohitaji nguvu na huenda mwanamke akakosa siku moja au mbili kazini kutokana na kuwa kwenye hedhi.

Na wakikosa siku moja kazini inawabidi watoe malipo.

Presentational grey line

Huenda pia ukavutiwa na taarifa hizi:

Presentational grey line

Mazingira ya kazi sio mazuri vile - familia hizo zinabidi ziishi katika nyumba ndogo au mahema karibu na mashamba hayo, hakuna vyoo na kwasbabau uvunaji hufanywa usiku mara nyingine, hakuna muda maalum wa kulala na wa kuamka.

Na wakati wanawake wanapopata hedhi , inakuwa changamoto kubwa zaidi kwao.

Kutokana na hali duni ya usafi , wanawake wengi huishia kupata maamubukizi na wanaharakati wanaofanya kazi katika eneo hilo wanasema madkatari waliokosa maadili wanawahimiza kufanyiwa upasuaji usiohitajika hata wanapokwenda kwa tatizo dogo tu ambalo linaweza kutibiwa kwa dawa.

Kutokana na kwamba wanawake wengi katika enoe hili huolewa wakiwa wadogo, wengi huwana watoto angalau wawili au awatatu wanapotimia miaka 20.

Na kwasbaabu madkatari hawawaambii kuhusu matatizo wanayoweza kukabiliwanayo katika siku zijazo iwapo watatolewa kizazi, wengi huamini kwamba kufanya hivyo ni sawa.

Hili limevigueza vijiji vingi katika enoe hilo kuwa "vijiji vya wanawake wasio na vizazi".

This photograph taken on December 6, 2018 shows an Indian farmer harvesting sugarcane crop in a field on the outskirts of Ayodhya in northern Uttar Pradesh state

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Maelfu ya wanawake hufanya kazi katika mashamba ya miwa

Mwandishi kutoka BBC Marathi aliyekitembelea kijiji cha Vanjarwadi katika wilaya ya Beed amesema kuanzia Oktoba hadi Machi kila mwaka, 80% ya vijiji huhama kwenda kufanya kazi katika mashamba ya miwa.

Anaeleza kwamba nusu ya wanawake katika kijiji hicho wametolewa vizazi - wengi wao wakiwa ni wa chini ya umri wa miaka 40 na baadhi wakiwa bado katika umri wa miaka 20.

Wanawake wengi waliokutana nao wamesema afya zao zimedhoofika tangu wafanyiwe upasuaji huo.

Mwanamke mmoja aligusia kuhusu kupata 'maumivu yasiokwisha mgongoni, shingoni na kwenye magoti' na namna anvyoamka asubuhi mikono ikiwa imefura pamo jana uso na miguu.

Mwingine amelalamika kuhisi kisunzi saa zote na jinsi alivyoshindw akutembea hata masafa mafupi. Na matokeo yake, wote wamesema wamehsindwa kufanya kazi katika mashamba hayo ya miwa.

Taarifa ya pili, kutokajimbo la kusini la Tamil Nadu, pia lipo katika hali mbaya.

wanawake wanoafanya kazi katika kampuni tajiri ya thamani ya mabilioni ya dola wanatuhumu kwamba wamepewa tembe zisizo na jina kazini badala ya kupewa siku ya kupumzika, wakati wanapolalamika kupata maumivu ya hedhi.

Kwa mujibu wa ufichuzi wa wakfu wa Thomson Reuters uliotokana na mahojiano waliofanyiwa wanawake 100, ni aghalabu dawa hizo kutolewana madaktari na mafundi hao wa kushona wengi wanoatoka katika familia maskini wanasema hawawezi kukosa mshahara wa hata siku moja kazini kutokana na maumivu ya hedhi.

wanawake wote waliohojiwa wamesema walipokea dawa hizo na zaidi ya nusu yao wamesema kutokana na hilo waliathirika kiafya.

Maelezo ya video, Wasichana wanatumia vikopo vya hedhi kujisitiri

Wengi walisema hawakuambia jina la tembe hizo au kuonywa kuhusu madhara yake.

Wanawake wengi walilaumu dawa hizo kuwasababishia matatizo kiafya ikiwemo msongo wa mawazo, wasiwasi na hata maambukizi katika kibofu cha mkojo , uvimbe kwenye vizazi na wengine hata kupoteza uja uzito.

Ripoti hizo zimewalazimisha maafisa nchini kuchukua hatua. Tume ya kitaifa ya wanawake imetaja hali ya wanawake katika eneo la Maharashtra kuwa "mbaya mno" na kuiomba serikali ya jimbo hilo kuzuia maovu ya aina hiyo katika siku zijazo.

Serikali huko Tamil Nadu, imesema itakagua afya ya wanawake hao wanoafanya katika kampuni ya nguo.

Taarifa hizi zinatokea wakati jitihada zinachukuliwa duniani kuongeza ushiriki wa wanawake kazini kwa kuidhinisha sera zianzozingatia maslahai ya kijinsia.

Nchini Indonesia, Japan, Korea kusini na nchi nyingine kadhaa, wanawake wanaruhusiwa kupumzika kwa siku moja wakati wakiwa kweye hedhi.

Makampuni mengine mengi ya kibinfasi pia hutoa mapumziko ya aina hiyo kwa wanawake.