Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Mume aliyetoweka India apatikana kwenye video ya tiktok
Mwanamke mmoja nchini India amempata mumewe aliyetoweka kwa miaka mitatu, baada ya kumuona kwenye video ya mtandao wa kijamii TikTok.
Polisi wanasema mwanamume huyo aliyetoweka mnamo 2016 na tangu hapo alikuwa katika mahusiano na mwanamume aliyebadilisha jinsia na kuwa mwanamke.
Jamaa ya mke huyo alimuona kwanz akatika video hiyo na mwanamume huyo aliyejibadilisha jinsia , hatua iliyopelekea kuidhinishwa msako.
Polisi wanasema waliwashauri wapenzi hao ambao sasa wamerudiana.
Walimpata mume huyo , Suresh, huko Hosur - mji uliopo kuisni mwa jimbo la Tamil Nadu, mbali kutoka kwa mke wake anayeishi katika wilaya ya Viluppuram.
"Tuliwasiliana na shirika la watu wanaobadili jinsia katika wilaya hiyo waliotusaidia kumtambua mwanamke huyo kwenye video," Polisi wameiambia BBC Tamil.
Mkewe Suresh alikuwa amewasilisha ripoti ya kupotea kwa mumewake kwa polisi baada ya jamaa huyo kutoroka - lakini walishindwa kumpata wakati huo.
TikTok, ni mtandao wa kijamii kama Instagram au Snapchat unaoruhusu watumiaji kuweka na kusambaza video na una umaarufu mkubwa nchini India.
Ni app inayotumika pia na vijana Afrika mashariki, katika kuonyesha na kusambaza video za mzaha na furaha
Ina zaidi ya wafuasi milioni 120 India, lakini imeshutumiwa na baadhi pia kwa kuruhusu picha zisizofaa katika mtandao.
Mnamo Aprili mahakama ya Tamil Nadu iliagiza mtandao huo wa kijamii uondolewe kufuatia malalamiko kwamba unatumika kusambaza picha za ngono.
Lakini marufuku hiyo iligeuzwa wiki moja baadaye.