Ufilipino: Mataifa ya magharibi yanachochea uuzaji wa video za ngono za watoto

Theluthi mbili ya watoto ambao huingia katika biashara haramu ya ngono kupitia picha za video nchini Ufilipino hutumiwa na wazazi wao au watu wa familia zao, inadaiwa.
Sehemu kubwa ya biashara hiyo inaendeshwa na watu kutoka mataifa ya magharibi wanaowalipa watu wazima kutengeneza filamu -ambao wengi wanasema wanahitaji pesa ili kuishi.
Waathiriwa wa biashara hiyo nipamoja na watoto wadogo sana wenye umri hadi miezi sita, linasema shirika la kimataifa la haki - International Justice Mission.
Serikali ya Ufilipino inasema inafanya juhudi kupambana na unyanyasaji huo
Wengi miongoni mwa wanaonunua filamu hizo huelezea kile wanachotaka watoto wafanyiwe, na baadae hutengenezwa filamu ambazo hutumwa moja kwa moja mtandaoni au kutumwa kwenye mtandao kwa wanyanyasaji walioiagiza ambao huzitazama katika nyumba zao.
'Sauti za kamera'
Ripoti za visa vinavyoshukiwa vya unyanyasaji wa kingono wa mtandaoni wa watoto kote duniani inaonyesha kuwa visa hivyo vimeongezeka kutokazaidi ya 100,000 vilivyoripotiwa miaka mitano iliyopita na kufikia hadi zaidi ya milioni 18 mwaka jana , kulingana na idadi iliyotolewa na Kituo cha Watoto waliopotea na kutumiwa vibaya.
Ufilipino inaaminiwa kuwa ni kitovu cha tatizo.
Mshichana mmoja mwenye umri wa baraehe, kwa jina la bandia, Jhona - ameiambia BBC kuwa alipokuwa mtoto na rafiki yake walitumiwa vibaya kingonona bibi yake mzaa mama.
"Wakati mmoja, mimi na rafiki yangu tulipokuwa tunaoga, na baadaye kuanza kuvaa nguo zetu. Mama yake pia alikuwa chumbani na sisi.
"Tulidhani anaangalia kwenye Facebook, lakini tuligundua kuwa kulikuwa na sauti ya Kamera. Nilianza kujihisi vibaya.
"Rafiki yangu alimuuliza mama yake, 'Ni kwa nini unachukua picha?', na akajibu, 'Oh, hakuna lolote.'"
Jhona alisema kuwa baadaye aliambiwa na polisi kwamba picha zao zilionekana zikiuzwa kwenye mtandao.
"TWalisema zilitumwa kwa wateja kwenye mtandao katikanchi nyingine."

Shirika la - International Justice Mission, ambalo linafanya kazi na mashirika kama FBI na Shirika la kitaifa la kukabiliana na uhalifu la Uingereza , limesaidia kuwanusuru watoto wapatao 500 wa Ufilipino.
Linasema kuwa limekuwa likifanya shughuli za uvamizi na okoaji zaidi uliofanywa na polisi kwa zaidi ya miaka mitano - takriban watoto 150 kwa ujumla- na asilimiwa 69% ya visa walivyobaini viliwahusisha watoto ambao walitumiwa na wazazi au ndugu zao.
Mkurugenzi wa kitaifa wa shirika hilo, Sam Inocencio, alisema waathiriwa ni watoto zaidi.
"Takriban 50% wana umri wa miaka 12 au hata wadogo zaidi," alielezea. "Tumemuoko mtoto ambaye alikuwa na umri wa miezi sita.
"Kwa hiyo hapa tunazungumzia watoto wachanga, wasichana wadogo, ambao hawajafikia umri wa barehe ambao wananyanyaswa kingono kupitia mtandao."
Mwezi uliopita, Afisa wa zamaniwa jeshi la ingereza, ambaye alipanga kunyanyaswa kingono kwa watoto nchini Ufilipinohuku akiwatazama mtandaoni alifungwa jela.
'Dhamira huru'
Mama mmoja wa watoto watatu anayeishi nchini Ufilipino,ambaye hawezi kutambuliwa kutokana na sababu za kisheria aliiambia BBC kuwa ni kweli alisambaza video za unyanyasaji wa kingono wa watoto.
Alisema kuwa alifanya hivyo kwa dhamira huru, kwasababu sio yeye aliyezitengeneza video hizo.
"Nilimuuliza mgeni, 'Unataka watoto wa umri wa miaka 12 hadi 13?' Akasema anawataka hao," alieleza.
"Alichotaka tu kutoka kwangu ni kumtumia videoza watoto wakifanya ngono. Haikujalisha kwake ni wapi tendo hilo lilifanyika ."
Mwanamke huyo tayari amekwishashtakiwa na polisi kwa kuuza picha za aibu za mtoto wake mwenyewe.

Baadhi ya makanisa sasa yanaonywa kuangalia dalili za unyanyasaji wa kingono wa watoto kwenye wa kwenye mtandao.
Swala hilo linasemekana kuwa linachochewa na umaskini.
Lakini mchungaji wa kanisa moja lililopo eneo maskini viungani mwa mji mkuu Manila, Stephen Gualberto, amesema umaskini haupaswi kuwa kisingizio.
Alielezea wazazi wanaofanya biashara ya ngono ya watotot wao kama "wenye matatizo ya kiakili" , na akapuzilia mbali madai yanyayotolewa na baadhi ya watu kuwa wazazi hao hawana jinsi kwasababu ni maskini.
" Kuna mambo mengi ya kufanya, na hauhitaji kumuuza mtoto wako ili familia yako iishi."

Mapema mwaka huu , Polisi ya Ufilipino ilianzisha kituo cha unyanyasaji wa watoto katika mji mkuu Manila, kwa ajili ya kukabiliana na tatizo hilo linaloendelea kukua ikisaidiwa na ufadhili wa kifedha na mafunzo kutoka kwa polisi ya Uingereza na Australia.
Lakini naibu waziri anayehusika na tume, Lorraine Badoy, aliiambia BBC: "Sidhani tunafanya juhudi zozote zinazozaa matundakwasababu huu ni uhalifu uliojificha sana ."
Alisema kuwa "anahofia gharama ya jamii kwa kuwa na watoto wote hawa wenye majeraha".












