Je dunia inahitaji miujiza ya madini haya?

Afrika imerithi ardhi duni

Chanzo cha picha, Credit: Sibylle Grunze

Maelezo ya picha, Afrika imerithi ardhi duni
Muda wa kusoma: Dakika 6

Huwezi kupanda mazao bila mbolea ya phosphorus. Ili kuipata mara nyingi wakulima ,hutegemea mbolea hiyo ambayo ni ghali,na ambayo mara nyingi haipatikani. Lakini kunaweza kuwa na njia bora na rahisi zaidi.

Mjini Blantyre, Malawi, kikundi cha wakulima wamekusanyika karibu na rundo la mbolea vunde inayoweza kusaidia kubalidili hali ya baadae ya kilimo barani Afrika. Haionekani kama ni kitu kikubwa : rundo la mita mbili kwa mbili za mbolea mbadala ya kujitengenezea kama vile la mabua ya mahindi na mbolea ya kuku.

Lakini kwa zaidi ya wiki nane za utengenezaji wa mbolea ya kuozeshwa na bakteria imekuwa ni njia ya kuongeza rutba zaidi kwenye ardhi n kupunguza utegemezi wa mbolea inayotokana na madini, ambayo kwa kawaida ni ghali na wakati mwingine huwa adimu kabisa.

" Huu si uwanja wa kawaida wa kuozesha rundo la taka , ambapo unatupa uchagu wa chakula cha kuku ," anasema Johann van der Ham, ambaye anaendesha mradi wa kuwaelekeza wakulima, huku akiwatazama wanafunzi wake wakinyunyizia maji kwenye rundo jingine la mbolea kwenye mkokoteni.

"Ni kifaa kinachoozesha rundo hili la mbolea. Tunafndisha jinsi ya kujenga kwa mtindo unaofaa na kupima rundo kulingana na kiwango cha kila mkulima anachokihitaji.

Wakulima wanajifunza jinsi ya kutengeneza mbolea hii, na watu wengine katika jamii zao ambao wataleta taarifa hii kwao, ni wakulima wadogo.

"Kwao kushindwa kupata mavuno inamaanisha njaa na matatizo au hali mbaya,'' anasema van der Ham. "Hadi sasa kwao, kuboresha udongo si kuongeza, si kitu cha kujivunia. Ni jambo la kufa au kupona.

Johann van der Hamanaongoza kikundi cha wakulima katika karakana ya kutengeneza mbolea vunde mjini Blantyre Sibylle Grunze

Chanzo cha picha, Sibylle Grunze

Maelezo ya picha, Johann van der Hamanaongoza kikundi cha wakulima katika karakana ya kutengeneza mbolea vunde mjini Blantyre Sibylle Grunze

Hali ya baadae ya Mbolea.

Kiasi kikubwa cha ardhi ya Afrika hurithiwa ikiwa katika hali duni. Zaidi ya mamilioni ya miaka, ardhi change, yenye rutba imekuwa ikisombwa, na kuacha sehemy kubwa ya mashamba ya kale nje. Katika mataifa yaliyopo kusini mwa jangwa la sahara barani , kilimo cha mahindi cha muda mrefu katika ardhi moja , kimesomba rutuba ya ardhi kwa kiwango kikubwa.

Maelezo ya sauti, Viwavi wanavyotishia kilimo cha mahindi Kenya

Kwa mimea kukua vema huhitaji maji, mwanga wa jua na hewa. Pia inahitaji virutubisho kutoka kwenye udongo, yakiwemo madini ya nitrogen, potassium, na phosphorus. Yote haya ni muhimu- lakini phosphorus ni muhimu sana ,kwasababu inaathiri mimea katika maisha yake ya awali. Mime huihitaji kujenga mfumo wake wa mzizi.

Kurejesha phosphorus ndani ya ardhi ya Afrika kwa hiyo ni muhimu sana kwa wakulima :

Wafanyakazi wanane kati ya 10 wa Malawiwameajiriwa katika kilimo:

Siku hizi , kiwango kikubwa cha phosphorus katika kilimo kote duniani hutoka katika mbolea zitokanazo na madini. Lakini upatikanaji wa baadaye wa mbolea hiyo uko mashakani.

Bei iliyoshtua ya phosphorus ilikuwa ni yam waka 2008, wakati madini hayo yalipopanda bei kwa 800%.

"Hapo ndipo watu walipoanza kuamka ," anasema Dana Cordell, mtafiti katika Chuo Kikuu cha Sydney cha teknolojia na muasisi mwenza wa utafiti wa dunia kuhusu Phosphorus.

Leo, mbolea katika kilimo inayotumiwa katika kilimo inatokana na madini na huuzwa katika maduka kama hili la Blantyre

Chanzo cha picha, Sibylle Grunze

Maelezo ya picha, Leo, mbolea katika kilimo inayotumiwa katika kilimo inatokana na madini na huuzwa katika maduka kama hili la Blantyre

Lakini hata kama kungekuwepo na kiwango cha kutosha cha phosphorus cha kukidhi mahitaji kwa karne zilizopita, bado kuna matatizo ya utegemezi wake - kama vile ugumu wa usamabaji wake. "Vyanzo vya Phosphate ni vya kijiografia zaidi kuliko hata mafuta ," anasema Cordell. "Huku nchi zote na wakulima huhitaji kupata, ni asilimia 88% ya iliyobaki kwenye hifadhi ya madini ya phosphate ."

Morocco pekee inakadiriwa kuwa na 75% ya akiba ya dunia

Baadhi ya akiba iko katika eneo linalozozaniwa la Sahara maghari.

Kwa nchi zinazoiagiza kutoka nje, hukabiliwa na hatari ya kibiashara ya muda mfupi na hatari ya muda mrefu ya usalama wa chakula wa nchi, anaonya Cordell.

Tukirejea tena katika karakana , van der Ham anajaribu anajaribu kuelezea hali halisi ilivyo. "Ni watu wangapi wanaishi nchini Malawi?" anauliza. Jibu ni takriban watu milioni 19 million.

"Unaona ?" anasema kwa tabasamu, " Kuna viumbe wengi zaidi katika kijiko kidogo cha chai cha udongo wenye rutuba kuliko idadi yote ya watu wa Malawi."

Bwana Va anafundisha anachokitekeleza mwenyewe. Shamba lake halijatumia Phospherous.

Kurahisisha upatikanaji

Mwamba wa madini ya phosphate...ambao mbolea yake husambazwa kote duniani

Chanzo cha picha, Sibylle Grunze

Maelezo ya picha, Mwamba wa madini ya phosphate...ambao mbolea yake husambazwa kote duniani
Maelezo ya sauti, Mashamba ya Rwanda yameshambuliwa na viwavi jeshi.

Kuna faida nyingine pia ya matumizi ya mbolea vunde ukilinganisha na mbolea itokanayo na madini : upatikanaji wake ni rahisi.

Billy Bray anaongoza Shirika la Uholanzi lisilo la kiserikali nchini Malawi linalojulikana kama Taka(Waste), linaloangazia masuala ya usafi . " Tunahitaji kutengeneza thamani kutokana na taka taka," anasema , "ili tuweze kubuni vyanzo vipya vya mapatona kuacha kutupa ovyo takataka na tabia nyingineso . Na mbolea vunde ni bidhaa yenye thamani hapa ." Kikundi chake kinafanya kazi kwa ushirikiano wa karibu na serikali ya mji wa na kwa sasa wanatengeneza kituo cha kusafisha maji mjini Blantyre. "Wazo letu ni kupunguza hatari kwa wawekezaji wa ndani ya nchi ," anasema.

Nchini Malawi, wakulima hutegemea mbolea ya phosphorus inayoagizwa kutoka nje ya nchi

Chanzo cha picha, Sibylle Grunze

Maelezo ya picha, Nchini Malawi, wakulima hutegemea mbolea ya phosphorus inayoagizwa kutoka nje ya nchi

Lakini kuwaelekeza watu juu ya suala lenyewe halijawa suala rahisi.

Maelezo ya sauti, Kilimo bora cha kisasa kinaweje kuwafaidi wakulima Tanzania?

"Urejeshaji wa rutuba ni jambo ambalo haliko mawazoni kwa sasa ," anasema Emmanuel Kanjunjunju, Mkurugenzi wa huduma za afya na jamii katika jiji la Blantyre. "Wana matatizo mengine mengi . Lakini kama mji lazima tufikiria mbele. Huwezi kufanya kazi katika mzozo. Kila mara utashindwa.Mifumo hii lazima ipangwe miaka 10, wakati mwingine miaka 30 kabla.

Kwa sasa timu kutoka kwenye kikundi cha Taka kinajenga vitanda vya kukaushia mbolea. Mwishowe mtaka zilizokaushwa zitakuwa ni sawa na takriban 5% ya mpolea vunde iliyoozeshwa. Uchafu mwingine utatoka katika soko, kama vile matunda yaliyoharibika na mboga pamoja na mbolea ya kuku kutoka kwenye shamba la kuku lililopo karibu.

Kwasababu ya kemikali ya asidi ya udongo, madini ya phosphate hutoweka kwa ajili ya mimea baada ya kuwekwa shambani

Chanzo cha picha, Sibylle Grunze

Maelezo ya picha, Kwasababu ya kemikali ya asidi ya udongo, madini ya phosphate hutoweka kwa ajili ya mimea baada ya kuwekwa shambani

Lengo la shirika lisilo la kiserikali ni kuzalisha tani 1,000 za mbolea vunde kila mwa kutoka kwenye masoko ya jumla. "

"Utatuzi wa matatizo ya teknolojia pekee hautatatua tatizo la phosphorus ," anasema Johan Six, profesa wa chuo kikuu cha mifumo ya kudumu ya kilimo katika ETH Zürich.

Maelezo ya video, Mwamvula Mlangwa,Mkulim

Yeye na wenzake kwa sasa wana tathmini ni vipi njia za kiteknolojia kama kilimo cha kuchanganywa na upandaji wa miti, upandaji wa mimea tofauti shambani na uhifadhi wa kilimo unavyoweza kuathiri urutubishaji wa ardhi. "Tumefahamu kwa muda mrefu kuwa njia hizi zinaweza kuwa za maana kwa uwiano wa virutubisho katika ardhi," anasema Six.

Lakini hadi hivi karibuni, juhudi zimekuwa zimeelekezwa zaidi kuhusu hewa za nitrogen na carbon. "Upatikanaji wa Phosphorus ni vigumo zaidi kuipima na kwa kiasi fulani imekuwa ," anasema.

Kinyume na mbolea ya madini, mbolea vunde inaweza kutunza muundo wa udongo kwa kuongeza mbolea yenye bakteria wa uozo

Chanzo cha picha, Sibylle Grunze

Maelezo ya picha, Kinyume na mbolea ya madini, mbolea vunde inaweza kutunza muundo wa udongo kwa kuongeza mbolea yenye bakteria wa uozo

Nchini Malawi, Six na mwenzake Janina Dierks wanafanya utafiti juu ya athari za miti ya mikaritusi kwa mahindi. Wakulima wanapenda miti hii kwasababu matawi ya mimea yake hutoa kivuli kwa mimea wakati wa msimu wa mvua. Mikaritusi ina utajiri wa bakteria aina ya symbiotic mycorrhiza, wanaoishi katika mfumo wa mizizi. Uchunguzi wa Kilimo cha kwenye mahema(Greenhouse) ulionyesha kuwa viumbe hai wadogo sana husaidia kuchukua juu virutubisho kaa vile nitrogen na phosphorus sit tu kwa mmea uliowapokea, bali pia hata kwa mimea mingine.

Ili kudumisha uwepo wa phosphorus, lazima mtu azingatie mfumo mzima, wakiwemo wakulima wa nchi kama hawa katika kijiji cha Ndindi

Chanzo cha picha, Sibylle Grunze

Maelezo ya picha, Ili kudumisha uwepo wa phosphorus, lazima mtu azingatie mfumo mzima, wakiwemo wakulima wa nchi kama hawa katika kijiji cha Ndindi

.

Six na Dierks wanataka kubaini ikiwa ni kweli shambani pia inaweza kuwa hivyo na kwama ni kweli ni kwa umbali gani.

Hatimae, kudhibiti uwepo wa kudumu wa phosphorus, mtu anatakiwa kuzingatia mfumo mzima: kuanzia bakteria wadogo waliopo kwenye miti,wakulima wa eneo hadi watengenezaji wa mbolea, serikali za kikanda na wafanyabiashara.

"Na ili kuweza kufanikisha hili , unapaswa kujua ni kipi kinakwenda wapi ," anasema Profesa Frank Mnthambala, mwanafunzi wa PhD katika chuo cha Malawi Polytechnic katika Chuo Kikuu cha Malawi, ambaye anafanya kazi na Dana Cordell na wanasayansi wengine.

Mnthambala kwa sasa anafuatilia matumizi ya phosphorus kupitia mfumo wa Wamalawi. Anasema kuwa kuna vyanzo vingi vya phosphorus ambavyo havitumiwi katika mfumo. "Lakini hakuna mtu ambaye kamwe aliwahi kuelezea kiwango chake kabla ," anasema Mnthambala, na bila kufahamu ni kiwango gani , ni vigumu kuwa na kipaumbele cha chanzo cha kufuatilia.

Taka za soko ni mojawapo yavyanzo vya mbolea vunde

Chanzo cha picha, Sibylle Grunze

Maelezo ya picha, Taka za soko ni mojawapo yavyanzo vya mbolea vunde

Pale Mnthambala atakapobaini vyanzo vinavyoleta matumaini vya upatikanaji wa phosphorus, kutafuta njia za kuipata itakuwa ndio hatua itakayofuatia.

"Lengo letu ni kuifanya Malawi isitegemee zaidi uagizwaji wa bidhaa za ukulima," Mnthambala anasema. "Na kudhibiti virutubisho vyetu itatusaidia kufikia lengo hili."

Unaweza pia kutazama:

Maelezo ya video, Mitikasi 23.11.2018: Kubadilisha kilimo kuwa kitega uchumi