Magufuli: Wanajeshi wa Tanzania watabaki DRC, licha ya 30 kuuawa

Rais Magufuli amesema , Bwana Tshisekedi tayari amekwishafanya maridhiano na makundi kadhaa hasimu, na kuwafungua wafungwa wa kisiasa waliokuwa mahabusu

Chanzo cha picha, Ikulu ya rais/Tanzania

Maelezo ya picha, Rais Magufuli amesema , Bwana Tshisekedi tayari amekwishafanya maridhiano na makundi kadhaa hasimu, na kuwafungua wafungwa wa kisiasa waliokuwa mahabusu

Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli amemuhakikishia rais wa Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Kongo(DRC) Felix Tshisekedi kuwa Tanzania itayaondoa majeshi yake ya walinda amani kutoka DRC mara amani ya kudumu itakapopatika na katika nchi hiyo.

Walinda amani wa Tanzania wako DRC chini ya Kikosi cha walinda amani wa Umoja wa Mataifa cha kuimarisha amani kinachojulikana kama , 'Monusco.'

Umoja wa Mataifa una wanajeshi kutoka mataifa mbalimbali wanaolinda amani DR Congo wakiwemo Watanzania

Chanzo cha picha, AFP/GETTY

Maelezo ya picha, Umoja wa Mataifa una wanajeshi kutoka mataifa mbalimbali wanaolinda amani DR Congo wakiwemo Watanzania

Rais Magufuli ametoa hakikisho hilo katika Ikulu ya rais Jijini Dar es Salaam Alhamis, wakati alipokuwa katika sherehe rasmi za za kumpokea Bwana Tshisekedi ambaye yuko katika ziara ya kitaifa ya siku mbili nchini Tanzania.

Dkt. Magufuli amesema kuwa licha ya Tanzania kuwapoteza wanajeshi wake 30 wa kulinda amani nchini DRC, haitawaondoa wanajeshi wake huko.

Mwaka 2017 pekee walinda amani 12 wa Tanzania waliokuwa katika kikosi cha Umoja wa Mtaifa Monusco baada ya kambi yao kuvamiwa mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, kwamujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres.

" Walinda amani wa Tanzania wataendelea kubakia huko hadi amani kamili itakaporejea nchini. Rais wa nchi mbili ni majirani, marafiki, makaka na madada ,"alisema.

Rais Tshisekedi amesema ziara yake nchini Tanzania inalengo la kuzungumza na rais Magufuli juu ya namna ya kufikia amani ya kudumu nchini DRC
Maelezo ya picha, Rais Tshisekedi amesema ziara yake nchini Tanzania inalengo la kuzungumza na rais Magufuli juu ya namna ya kufikia amani ya kudumu nchini DRC

Kwa mujibu wa rais wa Tanzania , Bwana Tshisekedi tayari amekwishafanya maridhiano na makundi kadhaa hasimu, na kuwafungua wafungwa wa kisiasa waliokuwa mahabusu. Hii ni hatua muhimu katika kurejesha amani nchini DRC, alisema Magufuli.

"Tanzania inaunga mkono juhudi za amani kwasababu hazitasaidia tu katika kuleta hakikisho la amani na uthabiti ; amani pia itachochea maendeleo ya kiuchumi baina ya nchi za maziwa makuu na bara zima la Afrika kwa ujumla ," alisema.

Kwa mujibu wa rais wa Tanzania nchi mbili zina mahusiano ya kihistoria na ndio maana Tanzania ndio maana Tanzania ilikuwa mstari wa mbele kusaidia katika utatuzi wa matatizo yanayoikabili DRC.

" Kwa mfano, tuliwapokea na kuwasaidia wakimbizi ikufuatia mizozo ya mapigano iliyotokea katika miaka ya rupted 1990 na 2000 . Pia , Tanzania, South Africa na Malawi zilitoa askari wake kuchangia kikosi cha kulinda amani mwaka 2013 chini ya UN ," Alisema Dkt.Magufuli.

Ijumaa asubuhi Rais wa Kongo Felix Tshekedi anatarajia kutembelea bandari ya Tanzania akiwa na mwenyeji wake Rais wa Tanzania John Magufuli
Maelezo ya picha, Ijumaa asubuhi Rais wa Kongo Felix Tshekedi anatarajia kutembelea bandari ya Tanzania akiwa na mwenyeji wake Rais wa Tanzania John Magufuli

Kwa upande wake rais Tshisekedi amesema ziara yake nchini Tanzania inalengo la kuzungumza na rais Magufuli juu ya namna ya kufikia amani ya kudumu nchini DRC. Pia aliwashukuru walinda amani wa Tanzania wanaohudumu nchi yake chini ya mpango wa kikosi cha Umoja wa mataifa Monusco.

" Nimeongea na rais Magufuli kuhusu bandari ya Dar es Salaam port na Reli ya -Standard Gauge Railway (SGR) -ambayo imepangwa kufika Rwanda. Nilielezea kuhusu uwezekano wa kupanua zaidi mradi hadi DRC," alisema.

Marais wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC)
Maelezo ya picha, Rais Tshisekedi amefichua kuwa hivi karibuni DRC ilituma maombi ya uanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC)

Amesisitiza kuwa ushirikiano wa kiuchumi wa mataifa ya Afrika utakaoleta maendeleo ya kudumu utafikiwa kupitia uwekezaji na utekelezwaji wa miradi ya miundombinu ,izikiwemo leri, barabara na nishati.

Rais Tshisekedi amefichua kuwa hivi karibuni DRC ilituma maombi ya uanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), hatua ambayo inaiondolea nchi hiyo vikwazo vya kibiashara, na kuongeza shughuli za kiuchumi miongoni mwa nchi wanachama.

Unaweza pia kutazama:

Maelezo ya sauti, Rwanda,Uganda,Tanzania,Burundi na DRC kujadili jinsi ya kupambana na makundi ya waasi