Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Ethiopia: Mwanamke ajifungua mtoto na kufanya mtihani dakika 30 baadae
Mwanamke mmoja nchini Ethiopia awewashangaza baadhi watu baada ya kuamua kufanya mtihani hospitalini dakika 30 baada ya kujifungua.
Almaz Derese, 21, kutoka eneo la Metu magharibi mwa Ethiopia, alitarajia kufanya mtihani wake kabla ya kujifungua, lakini mitihani ya shule ya upili iliahirrishwa kwasababu ya mfungo wa mwezi wa Ramadan.
Alipata uchungu wa uzazi Jumatatu muda mfupi kabla ya mtihani kuanza.
Bi Almaz anasema kusoma ukiwa mjamzito haikuwa tatizo kwake ila hakutaka kusubiri mwaka mwingine mmoja ili aweze kuhitimu masomo yake.
Alifanya mitihani ya Kiingereza, Amharic na Hisabati akiwa siku ya Jumatatu na atafanya mitihani iliyosalia katika kito cha mitihani hiyo siku mbili zijazo.
"Kawasababu nilikua na harakisha kufanya mtihani, sikuchukua muda mrefu kujifungua," Bi Almaz aliiambia BBC Afaan Oromoo.
Mume wake, Tadese Tulu, anasema aliomba shule imruhusu kufanya mtihani huo akiwa hospitali.
Ni jambo la kawaida nchini Ethiopia, kwa wasichana kuacha shule ya sekondari na kurudi baadae kukamilisha masomo yao.
Bi Almaz sasa anataka kufanya kozi ya miaka miwili ambayo itamwezesha kujiandaa kwa masomo ua chuo kikuu.
Anasema kuwa amefurahia kuwa amefanikiwa kufanya mtihani wake na kwamba mtoto wake wa kiume pia yuko katika hali nzuri ya kiafya.