Marekani: Mwanamume ashtakiwa kwa mauaji ya wapenzi wa jinsia moja

Marchers wave Gay Pride flag during the 2018 San Francisco Pride Parade on June 24, 2018 in San Francisco, California

Chanzo cha picha, Arun Nevader/Getty Images

Mwanamume mmoja nchini Marekani amewapiga risasi na kuwaua watu watatu na kuwajeruhi wengine wawili kwa kuwa wapenzi wa jinsia moja, mwendesha mashtaka amesema.

Devon Robinson, 19, kutoka eneo la Detroit, ameshtakiwa kwa mashtaka matatu ya mauaji, na mawili ya kutumia silaha kuwajeruhi watu..

Waathiriwa wote ni wakaazi wa Detroit, wametambuliwa kuwa Alunte Davis, 21, Paris Cameron, 20, na Timothy Blancher, 20.

Bw. Robinson amekanusha mashtaka yote.

Katika taarifa kwa vyombo vya habari vya Marekani, mwendesha Kym Worthy alielezea"kusikitishwa" kwake na madai dhidi ya Robinson.

"Inasikitisha kuwa kisa hicho kilitokea mwezi ambao jamii inawasherehekea watu hao,"alisema. "Tunatakiwa kujitolea kutokomeza chuki dhidi ya wapenzi wa jinsia moja."

Polisi wanasema tukio hilo lilitokea siku ya makumbusho katika nyumba moja katika eneo la Detroit east side.

Kwa mujibu wa ofisi ya mwendesha mashtaka Davis na Bw. Blancher walikuwa wapenzi wa jinsia moja, na Bi Cameron alikuwa rafikia yao, vilisema vyombo vya habari vya Marekani.

Waendesha mashtaka wanasema waathiriwa walishambuliwa na Bw. Robinson kwa sababu ya jinsia yao, japo hajafunguliwa mashataka ya uhalifu wa chuki.

LGBTQ protest outside the Supreme Court

Chanzo cha picha, MLADEN ANTONOV/Getty Images

Waathiriwa wengine waliyopigwa risasi wameponea kifo.

Dada yake Davis, Dasha Robinsonamekiambia kituo cha televisheni chaWJBK-TV kuwa ndugu yake alikuwa mchangamfu "mpenda raha", iliripoti shirika la habari la Associated Press.

Kwa mujibu wa data ya hivi karibuni shirika la upelelezi la Marekani FBI, karibu 16% ya uhalifu wa chuki nchini humo unawalenga wapenzi wa jinsia moja .

Visa vingine 1.7% vilihusishwa na masuala ya kujitambulisha kijinsia .

Bw. Robinson amewekwa rumande na anatarajiwa kufikishwa mahakamani Juni 21.