Kwa picha: Mapambano ya fahali yanayovutia umati wa mashabiki Kenya

People cheering as two bulls go head-to-head in western Kenya

Chanzo cha picha, Duncan Moore

Katika jamii ya WaLuhya magharibi mwa Kenya, kuna utamaduni wa kupiganisha mafahali. Ulikuwa ni utamaduni uliotumika katika matukio muhimu kama mazishi, sasa mchezo huo umegeuzwa kuwa mashindano ambayo mara nyingine yana faida kubwa.

Mpiga picha Duncan Moore amesafiri kuelekea kuona namna jamii zinavyoshinikiza mchezo huu leo na kutaka utambulike rasmi.

People walking alongside a bull in western Kenya

Chanzo cha picha, Duncan Moore

Mapema Jumamosi asubuhi mpambanishaji wa fahali na kikosi chake kinaelekea katika uwanja ambapo atamkutanisha fahali wake na wa upinzani kutoka kijiji kingine.

People in western Kenya arriving to watch a bull fight playing musical instruments

Chanzo cha picha, Duncan Moore

Msafara huo unajumuisha wapigaji ngoma ya kitamaduni ya Isukuti ilio maarufu katika eneo hilo la magharibi na wanamsindikiza fahali kueleka kwenye mpambano, huku wakivutia umati wa watu njiani.

Children climb up trees in western Kenya to keep away from the bulls

Chanzo cha picha, Duncan Moore

Wakati umati unakusanyika, watoto wanakweqa mitini kupata taswira nzuri na kuwakwepa fahali hao wanaopita. Ijapokuwa hili ni tukio dogo kuna mapambano makubwa zaidi katika maeneo makuu yanayovutia idadi kubwa zaidi ya watu.

People look on at a bull in western Kenya

Chanzo cha picha, Duncan Moore

Watazamaji wanamkagua fahali, Misango, kabla ya pambano. Ni mdogo aliye na uwezo wa kukuwa, na mwenye thamani ya kiasi cha $800.

Bull chasing people in western Kenya

Chanzo cha picha, Duncan Moore

Fahali wa pili katika pambano hili ni, Tupa Tupa, anamshambulia mojawapo ya wanaume wanaojaribu kumsindikiza kwenda kwenye pambano hilo. wanaume wameshika fimbo wakiwashunga fahali hao, lakini wanapojaribu kutoroka, hakuna la kufanya.

People look on as a girl knocked over by a bull is carried away in western Kenya

Chanzo cha picha, Duncan Moore

Lililo hatari zaidi katika mchezo huu, hususan unapofanyika katika maeneo yasio rasmi, ni kutazama. hapa msichana anaondolewa baada ya kushambuliwa na fahali aliyeamua kutoroka badala ya kupambana.

Bulls starting to fight during a match in western Kenya

Chanzo cha picha, Duncan Moore

Baada ya kupimana nguvu na kutishiana kwa muda fulani , fahali hao husambuliana na mpambano huanza rasmi. wanaweza kupigana katika sehemu yoyote na mara hii hapa ilikuwa katika shamba la mahindi.

People cheer on the animals during a bull fight in western Kenya

Chanzo cha picha, Duncan Moore

Umati unafuatilia mpambano Kakamega na mara nyingine watu wanakimbia kuepuka kushambuliwa.

People cheer on the animals during a bull fight in western Kenya

Chanzo cha picha, Duncan Moore

Mashabiki wanakusanyika na kushangilia kwa nderemo mithili ya vita kati ya wapiganaji wawili.

Licha ya pingamizi kutoka kwa wateteaji haki za wanyama, wanaoshinikiza mchezo huo wanaeleza kwamba ni mchezo ulio na faida za kiuchumi na sehemu ya utamaduni wa jamii ya Waluhya.

Gerald Ashiono, chairman of the local Bull Owners Welfare group, looks on at a bull fight in western Kenya

Chanzo cha picha, Duncan Moore

Gerald Ashiono, mwenyekiti wa wamiliki fahali anatazama. Kundi hilo huhakikisha mashindano yanasajiliwa, na fahali wanashughulikiwa na viwanja sahihi vinatumika kwa mashindano hayo.

Bulls fighting - head-to-head - in western Kenya

Chanzo cha picha, Duncan Moore

Pembe zinagongana, Misango (kushoto) naTupa Tupa (kulia) wanapambana. Bwana Ashiono anasema ni utamaduni muhimu wa jamii katika eneo hilo: "babu yangu alimiki fahali, babangu pia na sasa mimi."

People scuffling as bulls fight in western Kenya

Chanzo cha picha, Duncan Moore

Jamaa wawili wanaomiliki fahali wazozana. mara nyingine huwa kuna wasiwasi mkubwa katika mashindano haya kutokana na kuhusishwa kamari katika mpambano huu.

People cheering on bulls during a fight in western Kenya

Chanzo cha picha, Duncan Moore

Hatahivyo Ashiono anasema aina hii ya mapambano ya fahali ni ya huruma na tofuati na yanayoshuhudiwa katika nchi kama Uhispania: "Fahali anaweza kuamua , kama hataki kupambana siku hiyo, huwezi kumlazimisha."

Crowds walk with defeated bull Tupa Tupa in western Kenya

Chanzo cha picha, Duncan Moore

Tupa Tupa na mmiliki ake wanarudi nyumbani baada ya kushindwa. Wakati fahali wanaoshindwa mara nyingi huishia kuuzwa kwa ajili ya nyama yao, tofauti na mapambano ya fahli Kenya ni kuwa hakuna anayeuliwa katika mapambano hayo.

People walk with victorious bull Misango in western Kenya

Chanzo cha picha, Duncan Moore

Misango, mshindi aliyefanikiwa kumfanya Tupa Tupa alazimike kutoweka, anasindikizwa kijijini kwa mmiliki wake na wafuasi lukuki.

Gerald Ashiono, chairman of the local Bull Owners Welfare group, looks on at his prize bull Imbongo in western Kenya

Chanzo cha picha, Duncan Moore

Kumfuga fahali wa kushiriki katika mapambano hayo sio jambo rahisi. Wanyama hao hutendekezwa na kupewa chakula maalum vikiwemo virutubishi na miti shamba.

Ashiono, anayeonekana hapa na fahali wake mshindi Imbongo, anasema: "kwetu, ni utamaduni, tukio la kijamii na mchezo wenye ufuasi mkubwa. Kuna matumaini makubwa katika mashindano ya mapambano ya fahali."

Picha za Duncan Moore