Vazi la waziri Mkuu wa Fiji lawashangaza wakenya Mitandaoni

Mkuu wa Fiji Frank Bainimarama wakati alipohudhuria Mkutano wa Shirika la Umoja wa mataifa la makazi mjini Nairobi alipata fiursa ya kumtembelea rais wa Kenya Uhuru kenyatta

Chanzo cha picha, Ikulu ya rais Kenya

Maelezo ya picha, Mkuu wa Fiji Frank Bainimarama wakati alipohudhuria Mkutano wa Shirika la Umoja wa mataifa la makazi mjini Nairobi alipata fiursa ya kumtembelea rais wa Kenya Uhuru kenyatta
Muda wa kusoma: Dakika 2

Wakenya kwenye mitandao ya kijamii wameonyesha kupigwa na butwaa na vazi alilovaa Waziri mkuu wa Fiji Frank Bainimarama wakati alipohudhuria Mkutano wa Shirika la Umoja wa mataifa la makazi mjini Nairobi.

Waziri mkuu Bainimarama ambaye ni mwanamume alikuwa amevalia suti ya sketi na viatu vya wazi (sandozi) wakati alipopata fursa ya kutembelea mradi wa ujenzi wa makazi nafuu katika eneo la Ngara jijini Nairobi.

Ruka X ujumbe, 1
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa X ujumbe, 1

Vazi alilovalia ni maarufu nchini kwa wanaume wa Fiji likifahamika kama na jina Suti ya Sulu.

Suti ya Sulu inachukuliwa kama vazi la kitaifa la Fiji na huangaliwa kama utambulisho wa jamii ya Wafiji . Vazi hili ambalo huwa wakati mwingine sketi yake inakatwa katwa upande wa chinihuvaliwa na wanaume na wanawake wa Fiji.

Sulu pia ni vazi rasmi la ofisini na huvaliwa katika sherehe za kitaifa pamoja na kanisani

Chanzo cha picha, Mtandao wa Twitter wa serikali ya Fiji

Lakini Sulu ya wanawake hufahamika kama Sulu-i-ra.

Urefu wa vazi hili unategemea na mtu apendavyo kuanzia chini ya magoti au urefu wa kufika kwenye kisigino.

Zamani ulikuwa unavaliwa mkanda tumboni. Hata hivyo wanaume wa kisasa wanaweza kukutumia pini.

Baadhi ya Wakenya walitoa maoni haya kwenye ukurasa wa Twitter:

Ruka X ujumbe, 2
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa X ujumbe, 2

Ruka X ujumbe, 3

Mwisho wa X ujumbe, 3

Ruka X ujumbe, 4

Mwisho wa X ujumbe, 4

Sulu zilivaliwa na watu wa Fiji Tangu enzi za ukoloni katika katika karne ya kumi na tisa. Mwanzo zililetwa na wamishonari waliokuwa wakitoka Tonga na katika kipindi hiki sketi hizi zilikuwa zikivaliwa na Wafiji kuonyesha kuwa wamejiunga na ukristo.

Sulu za wanawake zinazovaliwa kila siku hufahamika kama sulu-i-ra, na Sulu ndefu wanazovaa rasmi au wakati wa matukio ya sherehe hufahamika kama sulu jaba.

Sulu za wanaume wanazovaa rasmi huitwa -sulu vakataga.

Vazi la sulu pia huvaliwa kama sare rasmi ya polisi na jeji nchini Fiji

Chanzo cha picha, Mtandao wa Twitter wa serikali ya Fiji

Maelezo ya picha, Vazi la sulu pia huvaliwa kama sare rasmi ya polisi na jeji nchini Fiji

Sulu zilizoshonwa na mifuko huvaliwa kawaida kama vazi la ofisi na rasmi pamoja na shati na viatu vya wazi (sandozi) na upande wa juu huvaa koti na tai.

Katika hali fulani, mtu anapoingia na Sulu kanisani huonekana kama mtu mwenye heshima nchini Fiji.

Sulu zilizoshonwa pia huvaliwa kama sare za polisi na jeshi.

Vazi rasmi la sulu huwana na urefu wa hadi chini ya magoti na hukatwa kwa mathalani umbo la pembe tatu.

Huku uvaaji wa Sulu mara nyingi huwa ni wa lazima kwa Wafiji wakati fulani, baadhi ya jamii wakati mwingine hukatazwa kuzivaa.