Mwanamuziki Mose Fan Fan aliyeimba wimbo 'papa lolo' amefariki akiwa na miaka 75

Mwanamuziki Mose Fan Fan
Muda wa kusoma: Dakika 1

Mwanamuziki maarufu nchini DR Congo Mose Fan Fan amefariki akiwa na umri wa miaka 75.

Mwanamuziki huyo alifariki kutokana na kile kinachodaiwa huenda ni shtuko wa moyo nyumbani kwake karibu na barabara kuu ya Thika jijini Nairobi.

Mtunzi huyo wa wimbo 'Papa Lolo' uliotia fora alikuwa mjini Nairobi katika mradi wa kurekodi nyimbo mpya na wanamuziki wa Nairobi akiwemo Paddy Makani na Disco Longwa.

''Mose alikuwa akicheza Gita na bendi ya Franco Ok Jazz mwaka 1972. Ninamtambua kuwa mchezaji Gita na mwandishi mzuri wa nyimbo barani Afrika . Amekuwa akizuru nairobi mara kwa mara tangu 2015 akishirikiana na na bendi ya Ketebul Music na tabu Osusa'' , alisema mshindi wa tuzo ya kuchora wanasesere paul Kelemba aka Mado kulingana na gazeti la The standard nchini Kenya.

Na mashabiki wa mwanamuziki huyo waliomboleza kifo chake muda tu habari zake zilipoanza kusambaa katika vyombo vya habari

Ruka X ujumbe, 1
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa X ujumbe, 1

Ruka X ujumbe, 2

Mwisho wa X ujumbe, 2

Ruka X ujumbe, 3

Mwisho wa X ujumbe, 3

Mose alipenda sana Nairobi na amekuwa akitembea Kenya kila mwaka katika kipindi cha miaka mitatu iliopita kutoka London anakoishi.

''Tumeshangazwa na kifo chake na tunafanya mipango ya kumpeleka katika chumba kizuri cha kuhifadhi maiti huku tukiwasiliana na familia yake'', alisema Osusa.