Kaumwa na nyoka na kuwindwa: Maisha ya kasuku asiye wa kawaida

Chanzo cha picha, Courtesy of Ilair Dettoni
Freddy Krueger sio kasuku wa kawaida.
Na sio kwasababu alifanikiwa kurudi nyumbani katika bustani ya wanyama Cascavel huko kusini mwa Brazil, siku tatu baada ya kuibwa na wezi waliojihami kwa bunduki.
Alipatakana katika kizimba alimokuwa akiishi miaka minne iliyopita.
Aliibiwa alipokuwa anapata matibabu kutokana na kile wahudumu katika bustani hiyo wamesema ni kuumwa na nyoka - alivuja damu nusra afariki.
Lakini sio hayo tu.
Kabla ya kuanza kuishi katika bustani hiyo, aliishi katika ngome ya walanguzi wa madawa ya kulevya.
Alipewa jina la Freddie Krueger- jina la muigizaji katika filamu ya kutisha na pia kutokana na kwamba sura yake iliharibika mnamo 2015 baada ya kupigwa risasi usoni wakati wa operesheni ya polisi.
Alipoteza uwezo wa kuona kupitia jicho lake la kulia na sehemu ya mdomo wake ulivunjika kutokana na jeraha hilo.

Chanzo cha picha, Getty Images
Huenda sio jambo la kushangaza kwamba kasuku huyo hakuwa na urafiki alipoibiwa.
Majeraha yake hayakumzuia kuishi maisha kama kasuku mwingine.
Kw amfano licha ya sehemu ya mdomo wake kuharibika, bado alikuwa anaweza kuchambua magamba ya njugu na kula matunda.
Biashara haramu yenye faida
Polisi wanaamini kwamba huenda Freddy aliachiliwa huru na wezi baada ya kugunuda majeraha yake.
"Huenda ingekuwa vigumu kumuuza, na pengine angetambulika kwa urahisi kwasababu ni rahisi kumtambua Freddy ," Ilair Dettoni, msimamizi mkuu wa bustani hiyo ya wanyama ameiambia BBC.
Usafirishaji haramu wa wanyama ni mojawapo ya biashara haramu zenye faida kubwa nchini Brazil.
Wataalamu kutoka Renctas, shirika lisilo la serikali linalojihusisha na masuala ya biashara haramu ya wanayama, linakadiria kwamba biashara hiyo ina thamani ya $3bn kwa mwaka nchini humo

Chanzo cha picha, Courtesy of Ilair Dettoni
Msimamizi huyo anaeleza wamegundua damu ya binaadamu karibu na kituo cha afya alipokuwa kasuku huyo akipokea matibabu, anayoamini ni ushahidi kwamba kasuku huyo aliwashambulia wezi hao.
Matumaini ya kupata wageni zaidi
Kutekwa kwa Freddy sio tukio la kwanza linalohusisha wanyama katika mji huo wa Cascavel.
Mamba, na kasuku wengine pia wamewahi kuibia kutoka bustani, hiyo kutokana na kutokuwana fedha za kutosha kuweka mfumo thabiti wa ulinzi.
"Pengine masaibu ya Freddy yatawafanya watu watake kufahamu zaidi katika shughuli za bustani hiyo ya wanyama , na tunakaribisha wageni zaidi," amekiri Dettoni.













