Wanaume wasioweza kumuacha mjane kula peke yake

Eleanor with Jamario and his friends

Chanzo cha picha, Jamario Howard

"Mwanamke huyu amebadili muonekano wa maisha yangu."

Mwanaume mwenye umri wa miaka 23 alienda kula chakula cha jioni na marafiki, aligundua kuwa mwanamke mzee aliyekuwa amekaa karibu nao alikuwa peke yake .

"sitaki tena kula peke yangu," Jamario Howard alisema. " Mimi ni mtu wa watu, hivyo niliamua kuanza kuongea naye."

Bi. Pensioner Eleanor Baker, huwa anatembelea mgahawa huo mara moja kwa wiki, alimuangalia sura yake kwa karibu.

Jamario alisogea karibu yake na kujitambulisha yeye ni nani na kumuomba akae pamoja na mama huyo, walianza kuzungumza moja kwa moja.

Mara mama huyo alimwambia kuwa mume wake alifariki na siku inayofuata ni siku ya kusheherekea ndoa yao miaka 60.

Aliona ni vyema kumkaribisha mama huyo kula pamoja na marafiki.

" Alifurahi sana kukaa pamoja nasi na sisi pia tulifurahi sana na kuanza kumuuliza maswali ."

Yeye na marafiki zake walianza kuzungumzia watoto, wajukuu na mbwa na kupeana namba za simu .

Presentational white space

Hapo baadae walipoweka picha waliyopiga wakati wakila pamoja na bibi huyo katika Facebook, Picha ilisambaa kwa wengi kwenye mitandao ya kijamii na kuonekana kuwa ile ilikuwa mbinu nzuri ya kuonyesha ukarimu

Shirley writes 'She needed a friend and gained three' and Chris writes 'You are angels. God bless you.'

Chanzo cha picha, Shirley Carroll/Chris Burke

Presentational white space

"Umekuwa ni wakati furaha kwangu, maelfu wameguswa lakini nimefurahi pia kujuana na watu, mimi ni mtu wa watu ambaye naweza kuongea hata na ukuta"Jamario alisema.

Presentational grey line
Presentational grey line

Kwenye ukarasa wake wa twitter aliandika "bibi huyo hajui tu namna gani amegusa mioyo ya baadhi ya watu.

Presentational white space

Mama yake na familia yake walifurahia kitendo chake na wana matumaini kuwa jambo alilolifanya litawahamasisha watu wengi zaidi kukaa karibu na watu ambao ni wapweke na wanahitaji watu wa kuongea nao.

"Ninataka watu waone kuwa ni sawa mtu kuwa mkarimu na jambo la namna hiyo lina maana kubwa katika jamii.

Ukarimu hauna kikomo cha umri. Fuata kile ambacho moyo wako inataka kukifanya na ujumbe wangu kuwa mkarimu kila wakati", Jamario alisisitiza.