R. Kelly ashindwa kesi kwa kutohudhuria mahakamani

Chanzo cha picha, Reuters
Mwanamuziki nyota wa R&B , R.Kelly ameshindwa kesi baada ya kushindwa kuhudhuria mahakamana kusikiliza kesi inayomkabili ya unyanyasaji wa kingono.
Kellly alishindwa kutokea mahakamani huko Chicago, na kupelekea hakimu kutoa hukumu dhidi yake.
Mwanamke aliyetambulika kama HW alimshtaki Kelly kwa kufanya naye mapenzi mara kadhaa wakati alipokuwa na umri chini ya miaka 18.
Mwanamke huyo ni mmoja kati ya wanawake wanne ambao walimshtaki Kelly kwa kesi tofauti tofauti za unyanyasaji wa kingono.
Na tuhuma zote mwanamuziki huyo alidai kuwa hana hatia.
Kesi hii ambayo ameshindwa sasa inamuhusisha mwanamuziki huyo kuwa na mahusiano na HW , miaka 20 iliyopita wakati mwanamke huyo alikuwa na umri wa miaka 16.
Mwezi ujao, Jaji ataweza kusema ni kiasi gani Kelly atapaswa kulipa.
HW alimshitaki mwanamuziki huyo mwezi Februari , siku moja baada ya Kelly kukamatwa kwa mashtaka 10 ya unyanyasaji wa kingono.
Wakili aliyekuwa anamuwakilisha Kelly katika mashtaka yake amesema haruhusiwi kueleza chochote kwa sasa.

Chanzo cha picha, Getty Images
Mwendesha mashitaka wa Chicago alimfungulia Kelly mashtaka 10 yanayohusiana na makosa ya unyanyasaji wa kingono, huku yakihusisha waathirika wanne ambao watatu kati hao walifanyiwa unyanyasaji wakiwa na umri chini ya miaka 18
R kelly alisisitiza kutokuwa na hatia kwa mashtaka yote yanayomkabili na sasa yuko nje ya gereza kwa dhamana.
Kama atapatikana na hatia, mwanamuziki huyo atatakiwa kufungwa kati ya miaka mitatu hadi sita kwa kila kosa.














