Ulimwengu una hasira na sonona, ripoti ya Gallup inasema

Stressed woman

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Utafiti huo umebaini kwamba viwango vya sonona vimeongezeka juu zaidi kuwahi kushuhudiwa

Watu ulimwenguni wana hasira, sonona na wasiwasi kwa mujibu wa ripoti mpya ya kimataifa.

Kati ya watu 150,000 waliohojiwa katika nchi 140 , thuluthi moja yao wamesema wamekabiliwa na sonona au msongo wa mawazo huku angalau mmoja kati ya watu watano akisema amewahi kuhuzunika au kuwa na hasira.

Ripoti ya kila mwaka Gallup Global Emotions imewauliza watu kuhusu mazuri au mabaya walioyapitia.

Nchi iloeleza kukabaliwa na hisia mbaya ni Chad, ikifuatwa na Niger. Na ilio eleza kupitia mazuri ni Paraguay, ripoti hiyo imeeleza.

Watafiti wamegusia hisia walizopitia watu siku moja kabla ya utafiti huo kufanyika.

Walioshiriki waliulizwa maswali kama "Je ulitabasamu au ulicheka sana jana?" na pia "uliheshimiwa?" katika kujaribu kupata undani katika wanayoyapitia watu kila siku.

Takriban 71% ya watu wamesema walihisi furaha kwa kiasi fulani kwa siku hiyo kabla ya utafiti.

Utafiti huo umegundua kwamba viwango vya sonona vipo juu kuwahi kushuhudiwa, huku wasiwasi na huzuni ukiwa pia umeongezeka.

39% ya waliohusishwa katika utafiti huo wamesema wamekuwa na wasiwasi siku moja kabla ya utafiti huo, huku 35% wakikabiliwa na sonona.

line

Nchi tano za juu zenye kiwango cha juu cha kuhisi vizuri

  • Paraguay
  • Panama
  • Guatemala
  • Mexico
  • El Salvador

Nchi tano za juu zenye kiwango cha juu cha kutohisi vizuri

  • Chad
  • Niger
  • Sierra Leone
  • Iraq
  • Iran
line

Mataifa ya Marekani kusini ikiwemo Paraguay, Panama na Guatemala zilikuwa juu ya orodha ya mataifa yalio na kiwango cha juu cha watu kuhisi vizuri, ambako watu wameelezea "kuwa na hisia nyingi za matumaini, na nzuri kila siku."

Utafiti huo umedai kwamba matokeo yanadhihirisha utamaduni katika eneo hilo la Marekani kusini "kulenga mazuri tu maishani".

Chad ni miongoni mwa nchi zenye watu wasiohisi vizuri. Zaidi ya watu 7 kati ya 10 nchini humo wanapata tabu kupata chakula kwa wakati fulani katika mwaka uliopita.

Takriban 61% ya watu nchini ihumo wamesema wamewahi kuumia.

Nchi hiyo inakabiliwa na uhaba wa miundo mbinu na mzozo wa ndani ya nchi, huku hali ya afya na kijamii zikiwa hazilingani na hali ilivyo katika maeneo mengine

Licha ya Chad kuorodheshwa juu kuwa miongoni mwa matiafa yasiohisi vizuri, raia nchini Marekani na Ugiriki walikuwa na msongo wa mawazo kuliko raia wa Chad.

Ugiriki ndio taifa lenye idadi kubwa ya watu walio na sonona duniani huku 59% wakisema wamekabiliwa na msongo wa mawazo, siku moja kabla ya utafiti huo.

Takriban 55% ya watu wazima Marekani wamesema wana sonona.