Picha za kwanza za shimo jeusi angani zatolewa

Shimo jeusi

Chanzo cha picha, EHT Collaboration

Maelezo ya picha, Picha ya kwanza ya shimo jeusi . limezungukwa na gesi inayovutwa ndani na shimo hilo
    • Author, Na Pallab Ghosh
    • Nafasi, Ripota wa Sayansi, BBC News

Wanaanga wamefanikiwa kuchukua picha za kwanza kuhusu shimo jeusi ambalo linapatikana katika sayari ilio mbali.

Shimo hilo lina ukubwa wa kilomita bilioni 40 kwa upana ikiwa ni mara milioni 3 zaidi ya dunia na limetajwa na wanasayansi kuwa 'dubwana'.

Shimo hilo jeusi lipo umbali wa kilomita milioni 500 na lilipigwa picha na jumla ya darubini nane kote duniani.

Maelezo yamechapishwa katika jarida la wananaga la Astrophysical .

Maelezo ya video, Shimo Jeusi lililogunduliwa angani

Profesa heino Falcke wa chuo kikuu cha radboud nchini Uholanzi , ambaye alipenedekeza jaribio hilo, alimbia BBC kwamba shimo hilo lilipatikana katika sayari kwa jina M87.

Kile tunachokiuna ni kikubwa zaidi ya mfumo wote wa jua, alisema.

Jinsi picha hizo zilivyopigwa

Shimo hilpo lina uzito mara bilioni 6.5 zaidi ya Jua. na ni mojwawapo ya mashimo meusi ambayo tunadhani yapo. Ni dubwana kwa kweli, likiwa ndio shimo lenye uzito mkubwa zaidi ya yote ulimwenguni.