Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Tyler Barriss amefungwa jela kwa kupiga simu za uongo polisi
Mwanamume mmoja wa California- nchini Marekani amefungwa miaka 20 jela kwa kuwapigia simu za uongo polisi, ikiwemo simu moja mbayo ilisababisha kuuawa kwa mwanaume mwingine asiye na hatia.
Tyler Barriss alifanya kile kinachoitwa "swatting" ambapo simu bandia hupigwa kwa polisi kwa ajili ya kuwaagiza polisi kutumia silaha na mbinu maalumu hutumiwa na polisi kuivamia nyuma au makazi yanayolengwa...akidai kuwa alikuwa ameiteka familia yake.
Polisi walipofika eneo la tukio alipowaelekeza, walimpiga risasi baba wa watoto wawili Andrew Finch.
Barriss alikiri kupifa simu baada ya kuhusika katika mzozo juu ya mchezo wa video wa kuwaita polisi na wanaume wengine wawili.
Casey Viner mwenye umri wa miaka 18-kutoka Ohio na Shane Gaskill mwenye umri wa miaka 20-kutoka Wichita kwa pamoja wanasubiri kesi yao juu ya uhusika wao katika tukio hilo.
Tarehe 28 Disemba Barriss aliwaambia polisi kuwa alikuwa amempiga risasi baba yake na kuiteka familia yake.
Aliipatia polisi anuani ya Kansas ili hali anuani hiyo ilikuwa Los Angeles, umbali wa maili 1,400.
Polisi waliojihami kwa silaha walikwenda kwenye makazi hayo na kumpiga risasi Andrew Finch mwenye umri wa miaka 28- ambaye hakuwa na hatia wala kuhusika katika mzozo wa mchezo wa video wa kuwaita polisi.
Polisi imesema kuwa afisa wake alimpiga risasi Bwana Finch, baada ya kusogeza mikono kwenye nyonga yake.
Barriss pia alikiri kupiga simu nyingine za uongo, ikiwemo simu kuhusu tisho la ugaidi kwenye makao makuu ya shirika la ujasusi la Marekani FBI.
"Ninatumai kwamba mashtaka haya na ukubwa wa hukumu vinatuma ujumbe ambao utamaliza mchezo wa 'kuwapigia polisi simu za dharura za uongo ' katika jamii zenye mchezo huo, na pia dhana nyingine za aina hiyo ," Alisema mwanasheria wa Kansas- Stephen McAllister katika kauli yake.