Namna ya kujenga hoja vyema:namna bora ya kuonyesha kutokubaliana na namna ya kushinda

Chanzo cha picha, Getty Images
Je kuna namna nzuri ya kutokukubaliana hoja na watu wengine? Unaweza kuwa na hoja za kujenga?
Tofauti na imani ambayo imekuwepo kuwa hakuna haja ya kuepuka mgongano wa hoja-mgongano wa hoja mzuri unaweza ukazaa majibu mazuri, anasema Timandra Harkness.
Hoja iliyojengwa vizuri inaweza kuwa chanya kwako na kuleta faida ambazo hazikutegemea, hivyo jambo muhimu ni kuwa ni kwa namna gani utalifanikisha hilo.
katika ''namna ya kutokukubaliana: Muongozo kwa watu wanaoanza'', Harkness anatazama namna gani migongano ya maslahi , maono na migogoro kuhusu ukweli na hata maoni tofauti kuhusu filamu gani ya kutazama inaweza ikashughulikiwa kwa mafanikio makubwa.
Unataka kujifunza kujenga hoja vizuri? hizi ni dondoo kwa namna gani utaweza kufanikisha hilo.
1. Sikiliza wengine wanasema nini

Chanzo cha picha, Getty Images
Katika hali ya kutaka kutoa ujumbe wetu -mara nyingi tunakataa kusikiliza mawazo ya mwingine.Lakini usipuuze mpinzani wako anachotaka kukisema.
''kumekuwa na mawazo kuwa,hoja za upande wa pili hazina maana hivyo zitupiliwe mbali,kwamba tusijihusishe nazo,''anasema mtaalamu Claire Fox.
Lakini, hakika kila hoja ina angalau pande mbili, na kwa kuwasikiliza wengine unapata ufahamu na kufunguliwa, pia kubadilisha, kuboresha msimamo wako.
Fox anapenda sana nguvu ya hoja na mpaka amekuwa mmoja kati ya waratibu kwenye mambo yanayozua mjadala, mashindano ya hoja na hualika wanafunzi wa Shule nchini Uingereza kushiriki.
2.Jaribu kuwa mwenye huruma

Chanzo cha picha, Getty Images
Si kuwa muhimu pekee kuwasikiliza wengine-Unapaswa kusikiliza haswa wanasema nini pia.
Kris De Meyer, Daktari wa mishipa katika chuo cha Kings jijini London, anasema mara nyingi''watu huchukua msimamo na kujiweka kwenye nafasi hiyo'' hivyo mjadala ''huishia kwenye mgogoro na ugomvi''
lakini hali hii inaweza kuikwepa kwa kuonyesha huruma.
''Tunaweza kuwa na mtazamo kuwa ni vipi wao wangekua sisi tungependa kufanyiwa hivyo?anaeleza Claire Fox
''Jaribu kufikiria kwa nini wanafikiria kwa namna wanavyofikiria, na huwezi jua, unaweza hata kubadili msimamo wako.''
3.Rejea watu wengine walichokisema

Chanzo cha picha, Getty Images
''Mara nyingi mvutano huja kwa sababu ya kutoelewana,'' anasema Kris De Meyer.
Lakini kuna namna nzuri ya kushughulikia hilo: ''Inasaidia kama ukirudia kile kilichosemwa na wengine,'' Kris anaeleza, mpaka ''mpinzani wako aseme 'Ndio, hicho ndicho nilichomaanisha''.
''Kitendo cha kurudia, kinaweza kuondoa misuguano.''
4. Pambana na suala la mgongano wa maslahi

Chanzo cha picha, Getty Images
Mgogoro kati ya majirani kuhusu mpaka wa makazi, upanuzi wa majengo unaweza kuwa mbaya na wa kudumu muda mrefu
''Gundua mapema dalili za mgogoro'',anasema Liz Stokoe , Profesa wa masuala ya kijamii.
Anasema njia nzuri ni kuchukua hatua mapema, kabla ya maoni.
Na mara zote inasaidia kuchukua hatua kwa upole iwapo utakabiliwa na jirani, anasema Liz, kwa sababu ''hatimaye huwafikisha kwenye sehemu nzuri''.
5.Fanyia kazi mlichokubaliana

Chanzo cha picha, Getty Images
Inaweza kuonekana kitu kigeni, lakini kuwa na hoja zilizofanikiwa,sharti uweke wazi unajenga hoja kuhusu nini
''Ikiwa hatutakuwa na maadili kimsingi, basi haitawezekana kujihusisha na mjadala wa aina yeyote,'' anasema mkufunzi wa masomo ya filosofia, Clare Chambers.
Kutumia muda zaidi kufanyia kazi ile misimamo ambayo mnafanana nayo wakati wa mjadala itasaidia.''
Unaweza kwenda dukani kisha mkabishana kuhusu aina ya jibini mtakayonunua.Lakini ikiwa haijajulikana kama wote mnataka jibini, basi mvutano wenu hauwezi kuwafikisha popote.
6. Usifanye mashambulizi binafsi dhidi ya mwingine

Chanzo cha picha, Getty Images
Mgongano usiwafanye mkagombana-kuwa na mjadala wenye kujenga unapaswa kuepuka mvutano binafsi dhidi ya mwingine.
Mitandao ya kijamii imekua ikiruhusu mashambulizi kutoka kwa mtu asiyetambulika, lakini kwenye mjadala wenye kuhitaji mafanikio masuala haya hayaruhusiwi.
Jaribu kuuzuia ulimi wako, vuta pumzi nyingi, kisha jadili.

Chanzo cha picha, Getty Images
7. Kubali kosa
Sehemu ya kuwa na mjadala ni kukubali kuwa, wakati mwingine unaweza kuwa mwenye kosa
''Unahitaji watu ambao wako tayari kusonga mbele wakikosa hoja,'' anaeleza Mkurugenzi wa Global Innovation, Geoff Mulgan.
''Inaonyesha kuwa una moyo na umepevuka, na hakuna haja ya kujisikia vibaya kwamba ulikosea jambo fulani.
Tuwe na mtazamo kuwa kuna nafasi ya kurekebisha na kujifunza vitu vipya.












