Kimbunga Idai: Msumbiji, Malawi na Zimbabwe zimeathiriwa
Kimbunga Idai kimesababisha uharibifu mkubwa katika baadhi ya maeneo nchini Msumbiji, Malawi na Zimbabwe katika kile ambacho Umoja wa mataifa unasema huenda ni janga baya zaidi la hali ya hewa kuwahi kushuhudiwa kusini mwa Afrika.
Mamilioni ya watu walikuwa kwenye njia ya moja kwa moja na kimbunga hicho huku mji wa pwani wa Beira nchini Msumbiji ukiathirika zaidi.

Chanzo cha picha, Reuters
Idadi ya waliyofariki nchini Msumbiji kufikia sasa ni watu 200 lakini rais Filipe Nyusi anahofia idadi hiyo huenda ikawa juu zaidi.
Watu 100,000 wanahitaji kuokolewa katika mji wa pwani wa Beira (hapo juu), kwa mujibu wa serikali ya Msumbiji.

Chanzo cha picha, Getty Images
Mamia ya watu bado hawajulikani walipo huku jamaa zao wakijaribu kupekua vifusi kuwatafuta wapendwa wao.

Chanzo cha picha, Getty Images
Nchini Zimbabwe (hapo chini), waathiriwa wanabeba jeneza la mmoja wa wanafamilia aliyefariki kuelekea katika kambi ya muda karibu na mto Ngangu.

Chanzo cha picha, Getty Images
Watu wanachimba makaburi ya kuwazika waathiriwa pamoja:

Chanzo cha picha, Getty Images
Katika mto Umvumvu, hapo chini, wakaazi wanangalia kwa mshangao jinsi daraja la kuvuka mto huo lilivyoporomoka.

Chanzo cha picha, Reuters

Chanzo cha picha, Getty Images
Wafanyikazi wa Shirika la chakula la Umoja wa mataifa wanasema mji wa Beira (hapo juu) umeathiriwa vibaya na kimbunga hicho: "Hakuna umeme. Hakuna huduma za mawasiliano. Barabara zimeszibwa na milingoti ya umeme iliyoanguka."

Chanzo cha picha, Getty Images
Baada ya majengo mengi katika yakiwa yameharibiwa na mengine kuporomoka, watu wanakabiliana na makali ya baridi na hali mbaya ya hewa.

Chanzo cha picha, EMIDIO JOSINE
Nyumba zingine ziling'olewa mapaa kufuatia upepo mkali na iliyoandamana na mvua kubwa.

Chanzo cha picha, ADRIEN BARBIER
Barabara kati ya Beira na Chimoio imeharibika, hali ambayo imezifanya mashirika ya kutoa misaada kushindwa kuwafikishia waathiriwa misaada.

Chanzo cha picha, Getty Images
Wanafunzi wa Shule ya St Charles Luanga nchini Zimbabwe, hapo juu waliokolewa na majeshi. Walijitahidi kuepuka tope lillilo funga barabara kuu wanayotumia kwenda shule

Chanzo cha picha, Getty Images
Watu ambao mali yao yote imepotea sasa wanategemea misaada kutoka kwa mashirika ya kutoa misaada ya kibinadamu.
Picha iliyopigwa kutoka angani inaonesha uharibifu mkubwa uliyosababishwa na mafuriko yaliyosomba mimea shambani na nyumba na baadhi ya watu kupoteza maisha yao:

Chanzo cha picha, EPA
Picha zote zina haki miliki.















