Kimbunga Ida: Watu 65 wafariki nchini Zimbabwe

Watu 65 wamekufa Mashariki mwa Zimbabwe kutokana na eneo hilo kukumbwa na kimbunga Ida hata hivyo kati ya watu waliopoteza maisha katika shule mbili ambapo tufani hiyo iliwakumbwa usiku wa manane wakiwa wamelala.
Kimbunga hicho kimesababisha uharibifu wa miundo mbinu katika jimbo la Manicaland karibu na mpaka za Zimbabwe na Msumbiji.
Jitihada za uokoaji zinaendelea huku mamia ya watu wakiwa hawajulikani walioko,hali inahofiwa kwamba huenda inaweza ongeza idadi ya waliopoteza maisha.

Chanzo cha picha, ZINYANGE AUNTONY
Rais Emmerson Mnangagwa amelazimika kusitisha ziara yake mashariki ya kati ili kurejea nchini mwake kutokana na janga hili.
Hata hivyo kasi ya kimbunga hicho inapungua,japo kuwa tayari kimesababisha madhara makubwa huku takribani watu 200 wakiwa hawajulikani walipo.
Famia nyingi zinasubiria kupatiwa msaada baada ya nyumba zao kuondoshwa na maji japo kuwa uharibifu wa miundo mbinu zikiwemo barabara zinaongeza ugumu wa kuwafikia watu hao na kuwasaidia.
Raia wa Zimbabwe wameungana pamoja na kuendelea kufanya changizo za fedha,mablanketi na chakula kwaajili ya wahanga wa janga hilo.
Hata hivyo nchini Msumbiji na Malawi Kimbunga hiki Ida kimesababisha vifo vya watu 120.
Hali ya tahadhali imetangazwa nchini Zimbabwe katika maeneo yaliyoathiriwa na kimbunga hicho kilichoya kumba maeneo hayo kikiwa na mwenda kasi wa kilomita 177 kwa saa.














