Ghana: Taifa ambalo kila mmoja anatarajiwa kuchelewa

Msanii wa Ghana akitengeneza saa

Chanzo cha picha, AFP

Ni jambo la kawaida kwa maafisa wa serikali kuchelewa kufika katika shughuli zozote rasmi kwa sababu wanatarajiwa kuchelewa.

Waziri wa Japan wa olimpiki Yoshitaka Sakurada alipolazimishwa kuomba radhi kwa kuchelewa kwa dakika tatu kufika katika mkutano wa bunge, baadhi ya watu nchini humo walijiuliza ni mawaziri wangapi wangeliomba msamaha.

''Ni mwenendo ambao umekita mizizi katika jamii yetu kwasababu nilipokuwa waziri nilikuwa nikifika katika mkutano muda uliyowekwe kwenye ratiba na watiu walikua wanashangaa sana'' alisema Elizabeth Ohene.

Aliongeza kuwa ikiwa raisi rais angelifika kwa wakati katika mkutano, hiyo ingelisaidia sana kubadilisha mtazamo wa watu kuhusiana na suala la kuzingatia muda.

Tabia ya kutozingatia muda uliyowekwa imeathiri sehemu kubwa ya maisha ya watu nchini Ghana.

'Msomango mkubwa wa magari'

Mkutano uliyopangwa kufanyika saa nne huchelewa kwa dakika 45 hadi saa moja.

Msongamano mkubwa wa magari katika miji mikuu imetajwa kuwa sababu mojawapo inayowafanya watu kuchelewa na mara nyingi hutumiwa kama kisingizio cha kuchelewa.

Mwanamume akiangalia saa yake ya kidijitali

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Mikutano mingi nchini Ghana hucheleweshwa kwa dakika 45

Lakini msongamano wa magari haiwezi kumfanya mtu kufika saa kumi za jioni katika hafla ya chakula cha mchana ambayo ilikuwa imepangwa kuanza saa sita na nusu za mchana

Wale wanaokosoa tabia ya kuchelewa wanahoji kwanini mwenyeji wako akualike kwa chakula cha mchana lakini aishie kupakua chakula karibu saa mbili na nusu baadae.

Wakati wa kuapishwa kwake rais Nana Addo Dankwa Akufo-Addo, alilalamikia sasana suala la mikutano kucheleweshwa.

Aliahidi kuwa mstari wa mbele katika suala la kuzingatia wakati.

Wapanga ratiba wake walizindua mpango wa kuhakikisha anafika mapema katika mikutano ya hadhara.

''Nakumbuka wakati mmoja rais alifika katika mkutano kwa muda uliyowekwa na viongozi walibabaika kwasababu hawakuwa tayari'' alisema mmoja wa wapanga ratiba ya rais.

Rais wa Ghana Nana Addo Dankwa Akufo-Addo, na mtangulizi wake John Kufuor (R) -wakiwa katika mkutano wa kampeini

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Rais Nana Akufo-Addo (Kushoto) na mtangulizi wake John Kufuor (Kulia) wamejaribu kuimarisha suala la kuzingatia wakati

Anasema wajumbe walilazimika kukimbilia viti vyao huku rais Kufuor akiwaangalia kwa mshangao.

''Tumejitolea kuhakikisha kuwa rais anafika katika shughuli rasmi kwa muda uliyowekwa katika juhudi za kuwafanya watu kuelewa umuhimu wa kuzingatia wakati''

Kutoka wakati huo rais Akufo Addo amefanya kila juhudi kufikia lengo hilo kwa kufika mapema katika mikutano.

Lakini juhudi hizo hazijaleta mabadiliko makubwa kama ilivyotarajiwa.

'Ni vigumu kubaini ibada kanisani itakamilika saa ngapi nchini Ghana'

Ibada ya kanisa mjini Accra Ghana - picha ya maktaba

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Ni vigumu kubaini ibada ya kanisa itakamilika saa ngapi nchini Ghana

Hali ya kutozingatia muda limeathiri karibu kila sekta nchini.

Kwa mfano kanisa linaweza kuweka tangazo kuwa litaandaa ibada kuanzia saa tatu asubuhi lakini muda wa kukamilika kwa ibada hiyo haijumuishwi katika tangazioo husuka.

Mmoja ya wale waliyohudhuria ibada hiyo anasema kuwa alijipata ameshinda kanisani karibu siku nzima.

''Ni vyema kuzingatia wakati wako mwenyewe katika hali kama hizo'', alisema.

Hata hivyo suala la kuzingatia muda linasalia kuwa kitendawili kigumu kukitegua nchini Ghana.