Wanamgambo walijificha kwenye majengo Mogadishu

Vikosi vya usalama nchini Somalia vinapambana na watu waliokua na silaha waliokuwa wamejificha kwenye jengo mjini Mogadishu, saa kadhaa baada ya shambulio la kujitoa muhanga lililotekelezwa kwenye gari katika eneo la mtaa uliokuwa na pilikapilika na kusababisha vifo vya watu takriban saba.
Shambuli hilo lilitokea siku ya Alhamisi lililotekelezwa na watu wanaoshukiwa kuwa wanamgambo wa al-Shabab katika eneo lililokuwa na hoteli, maduka na migahawa.
Watu waliokuwa na silaha baadae walizungukwa na vikosi vya usalama
Majibizano ya risasi yaliendelea usiku mzima mjini Mogadishu.

Watu takribani 60 wamejeruhiwa na saba wamepoteza maisha, msemaji wa huduma ya gari za kubeba wagonjwa aliiambia BBC.
Watu kadhaa waliokolewa kutoka ndani ya jengo hilo, ripoti zimeeleza.Kuna wasiwasi kuwa idadi ya wanaoelezwa kupoteza maisha huenda ikaongezeka.
''Bado kuna watu wenye silaha ndani ya jengo,'' Afisa wa polisi Ibrahim Mohamed alinukuliwa siku ya Ijumaa asubuhi na shirika la habari la Ufaransa, AFP
Katibu mkuu wa umoja wa waandishi wa habari wa Somalia Mohamed Moalimuu alikuwa ndani ya Hoteli ya Maka al-Mukarama akiwa na mwezie waliposikia milio ya risasi ikifuatiwa na mlipuko.
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe
Kundi la al-Shabab, lenye mahusiano na al-Qaeda, wamefurumushwa kutoka nje ya Mogadishu mwaka 2011 lakini wameendelea kutekeleza mashambulizi mfululizo mjini humo.
Marekani imezidisha mashambulizi ya anga dhidi ya kundi hio, tangu rais Donald Trump alipoingia madarakani.
Marekani imesema al-Shabab inadhibiti maeneo mengi makubwa ya Somalia na kundi hilo lina uwezo wa kufanya mashambulizi makubwa kwa kutumia watu wa kujitoa muhanga, vilipuzi nasilaha ndogo na kubwa.












