Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu kushtakiwa makosa ya rushwa

Benjamin Netanyahu kulia na Mwendesha mashtaka mkuu Avichai Mandelblit

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Benjamin Netanyahu kulia na Mwendesha mashtaka mkuu Avichai Mandelblit

Mwanasheria mkuu nchini Israel anakusudia kumfungulia rasmi mashtaka Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu kwa makosa ya rushwa.

Bwana Nyetanyahu anakabiliwa na mashtaka ya rushwa, ufisadi na kuvunjwa uaminifu katika kesi tatu tofauti.

Waziri mkuu huyo anadaiwa kupokea zawadi kutoka kwa mfanyabiashara tajiri na kukubali upendeleo wa kupata nafasi ya kuchapishiwa taarifa zake.

Bwana Nyetanyahu ambaye anakabiliwa na uchaguzi, akizungumza katika Televisheni kwamba kesi hiyo dhidi yake itavunjika.

Madai mengine anayoshtakiwa nayo bwana Nyetanyahu ni kupokea zawadi ya kiasi cha dola za Marekani 264,100 kutoka kwa msanii wa Hollwood mwenye asili ya Israel Arnon Milchan na pamoja na bilionea wa Australia James Packer.

Waziri mkuu wa Israel na mkewe ambaye pia aliwahi kushtakiwa

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Waziri mkuu wa Israel na mkewe ambaye pia aliwahi kushtakiwa

Zawadi kutoka kwa Bwana Milchan, ni madai ya kutaka amsaidie kupata visa ya Marekani na pia katika masuala ya kodi.

Hata hivyo Milchan na Packer wameyakana mashtaka yao.

Mwanasheria mkuu wa serikali Avichai Mandelblit amesema atazingatia mashtaka ya ufisadi na kuvunja uaminifu, pamoja na rushwa.

Navyo vyama vya upinzani nchini humo, vimesema Netanyahu hawezi kuendelea na nafasi yake hiyo ya Uwaziri Mkuu, iwapo atashtakiwa.

Mwanasheria mkuu wa serikali amesema mahakama kuu ndio itakayoamua kama lazima ajiuzulu.

Isreal inatarajia kufanya uchaguzi mkuu April 9, na Waziri mkuu Benjamin Netanyahu ni mmoja ya wagombea.