Bwana mmoja Marekani aua Simba aliyemvamia mbugani

Mountain lion

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Mashambulizi ya Simba i ya nadra nchini Marekani.
Muda wa kusoma: Dakika 2

Bwana mmoja nchini Marekani amemuua Simba wa milimani ambaye alimshambulia ghafla mbugani.

Simba huyo dume alimvamia kwa nyuma bwana huyo ambaye hakutajwa jina lake katika Hifadhi ya Wanyama ya Colorado.

Maafisa wanyamapori wamethibitisha kutokea kwa tukio hilo siku ya Jumatatu ambapo mwanaume huyo amepata majeraha makubwa usoni na kwenye kiganja cha mkono.

Bwana huyo alikuwa akifanya mazoezi kwenye ukanda maalum kwenye mbuga hiyo ambao hupendelewa kutumiwa na wakimbiaji wakati tukio hilo lilipomkuta.

Maafisa wanasema aligeuka nyuma baada ya kusikia mnurumo nyuma yake nap apo hapo simba huyo akamrukia usoni.

"Simba alimrukia mkimbiaji huyo, na kumng'ata usoni na kiganjani. Lakini alifanikiwa kujinasua kutoka kwenye makucha yake na kisha kumuua," taarifa rasmi ya hifadhi hiyo imeeleza.

Ruka X ujumbe, 1
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa X ujumbe, 1

Presentational white space

Baada ya kumuua Simba huyo, bwana huyo alifanikiwa kuondoka eneo la tukio mwenyewe na kwenda kuomba msaada.

"Majeraha aliyopata usoni, mikononi, miguuni na mgongoni ni makubwa lakini si ya kutishia uhai wake," taarifa hiyo imeongeza.

Meneja wa hifadhi hiyo, Mark Leslie amesema kuwa katika tukio hilo mkimbiaji alitumia uwezo wake wote kujilinda dhidi ya Simba aliyemvamia.

"Alitumia ubavu wake wote kujiokoa. Ikitokea umevamiwa na Simba yakupasa utumie nguvu na maarifa yako yote kama bwwana huyu kujiokoa," amesema.

Ruka X ujumbe, 2
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa X ujumbe, 2

Presentational white space

Simba huyo ni wa milimani aina ya Cougar ambao hupatika katika mabara ya Amerika kuanzia eneo la British Colombia nchini Canada mpaka nchini Argentina.

Majina yao mengine maarufu ni Panther na Puma.

Hata hivyo, Simba aliyefanya shambulizi hilo alikuwa bado ni mdogo na alikuwa na uzani wa kilo 30.

The Horsetooth Mountain Open Space is a popular hiking spot outside Fort Collins

Chanzo cha picha, larimer.org

Maelezo ya picha, Eneo lilipotokea shambulio hilo ni maarufu kwa wakimbiaji na wapanda milima.

Mashambulio ya Simba kwa binaadamu Amerika ya Kaskazini na machache sana, na katika mbuga hiyo, ni watu chini ya 12 ambao wameuawa na Simba katika kipindi cha miaka 100 iliyopita.

Maafisa wanyamapori nchini humo wanawashauri watu kutokimbia pale wanapokutana na Simba na badala yake wawakabili.

"Ukikimbia, utamfanya Simba akuone kuwa wewe ni sehemu ya mawindo na atakukimbiza na akushambulie," taarifa ya wahifadhi inaeleza; "Unachotakiwa kufanya ni kumuonesha kuwa wewe ni hatari kwake ili akimbie. Watu wamewakabili Simba kwa kuwarushia mawe, fimbo ama mikono yao na kuwashinda."

Mwezi Mei mwaka jana waendesha baskeli wawili walishambuliwa na simba hao katika jimbo la Washington, mmoja alifariki na mwengine aliponea chupu chupu.

Mwezi Septemba mpanda milima katika jimbo la Oregon alipatikana akiwa mfu katika tukio ambalo mamlaka zinaamini ni la kwanza kwenye jimbo hilo kwa Simba kuua binadamu.

Presentational grey line